Hiki ni kipande cha gazeti la leo Jumatano Januari 1,2014 gazeti Mtanzania kuhusu habari za Boban.
Haruna Moshi, akimiliki mpira katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha wakati akiitumikia CUSC kwenye mechi yake ya kwanza ligi kuu na Wagosi wa Kaya. Ilikuwa ni mechi dhidi ya Oljoro JKT, ambapo CUSC iliibuka na ushindi wa mabao 2-0.
Ndugu zangu,
WIKI hii
kumekuwa na habari za upotoshaji juu ya kutimuliwa kwa kiungo mshambuliaji wa
Coastal Union ‘Wagosi wa Kaya’, Haruna Moshi ‘Boban’.
Ninaziita habari
za upotoshaji kwasababu hazina ukweli, na mara nyingine mtu anaweza kuenda
mbali zaidi na kufikiri kuwa kuna hujuma zinafanyika dhidi ya timu yetu ili
wachezaji wasicheze kwa moyo wakati wa mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Tanzania
Bara, unaotarajiwa kuanza Januari 25 mwaka huu.
Gazeti moja
la michezo, jina tunalihifadhi limeripoti likimnukuu kiongozi mmoja wa Wagosi
wa Kaya, jina pia tunalihifadhi kutokana na heshima yake; kuwa Coastal Union
haina mpango wa kumuongezea mkataba ‘Boban’ baada ya kumalizika miezi sita
ijayo kwasababu za utovu wa nidhamu.
Habari hizo
hazina ukweli kwasababu hakuna kikao kilichokaliwa kujadili mustakabali wa
mchezaji huyo. Ni kweli Boban, hajaripoti kambini mpaka sasa; lakini uongozi wa
juu akiwemo meneja wa timu unazo taarifa za mchezaji huyo.
Kuwa na nidhamu
ama kutokuwa na nidhamu, kumtimua ama kumuacha mchezaji, wanaoamua hayo ni
uongozi wa juu kupitia kamati zake ndogondogo kama za mashindano, usajii na
nidhamu. Na si mtu mmoja mmoja.
Hivyo kwa
niaba ya Mwenyekiti wa Coastal Union, Hemed Hilal ‘Aurora’ timu inaomba radhi
wanachama wa CUSC, kutokana na kuumizwa kwa namna moja ama nyingine na taarifa
hizo za upotoshwaji.
Wagosi wa
Kaya, bado wana mkataba wa miezi sita na Boban, kuongezewa ama kutoongezewa
mkataba suala hilo litajadiliwa kati ya mchezaji na viongozi pale utakapofika
ukingoni.
HAFIDH A.
KIDO
MSEMAJI CUSC
JANUARI 1,
2014
DAR ES
SALAAM, TANZANIA