Friday, December 27, 2013

Safari na mechi ya Ifakara dhidi ya Techfort...




 Kutoka kushoto, Katibu wa Coastal Union, Kassim Siagi, Kocha msaidizi Ally jangalu, Kocha Mkuu Yusuf Chipo na meneja wa U20 Abdul Ubinde.

 Mwalimu Yusuf Chipo, akizungumza na meneja wa U20, Abdul Ubinde kabla ya mechi kuanza..


 Abdullah Othman 'Sheikh Dullah' akijaribu kumtoka beki wa Techfort.



 Bao la kwanza lilianzia hapa, Danny alipenyezewa mpira, akamzidi nguvu beki wa Techfort, na kufunga.

 Bao la kwanza liliingua kimiani dakika ya 53 kipindi cha pili, liliingizwa kimiani na Danny Lyanga.

                        Masumbuko Kenneth katika moja ya harakati zake uwanjani juzi.

 Mohammed Miraji akishangilia bao la pili lililoingia dakika ya 90.



Baada ya mechi, wakazi wa Ifakara walilizunguka gari Coastal Union kuona wachezaji.........
 
Desemba 25, Coastal Union ilishuka dimbani kucheza mechi ya kujipima nguvu na Techfort FC, mabingwa wa Soka Mkoa wa Morogoro. Matokeo ni ushindi kwa Coastal Union 2-0. Mabao yalifungwa na Danny Lyanga na Mohammed Miraji.

Baada ya hapo timu ilirejea leo mjini Tanga, ambapo leo saa tisa Alasiri katika uwanja wa Gymkana timu itaendelea na mazoezi. Nawashauri walio mjini Tanga waende kuwaangalia vijana wamekuwa vizuri sana.

Aidha jana mwalimu Yusuf Chipo akishirikiana na mwalimu msaidizi Ally Jangalu, walimteua Juma Said Nyosso 'Baba Moza' kuwa nahodha mpya wa Coastal Union akishirikiana na Mbwana Khamis Kibacha.

Uteuzi huo umeanza mara moja siku ya juzi, na kuhusu nahodha wa zamani Jerry Santo, hakuna uhusiano wowote kati ya kuchelewa kwake kuwasili kambini na kuvuliwa unahodha. Bali mwalimu ameona Nyoso, kwa kipindi hiki anafaa kuwa nahodha kutokana na uzoefu wake katika ligi ya Tanzania na ana ufahamu mkubwa kwa wachezaji wa timu nyingine hasa katika masuala ya uwanjani.

Kutowasili kambini kwa Haruna Moshi 'Boban' na Jerry Santo, mwalimu na uongozi mzima wa Coastal Union unazo taarifa. Na wachezaji hao waliomba ruhusa kwa uongozi kuwa watachelewa kwa sababu za kifamilia na uongozi unafahamu hivyo na umewakubalia.

Wataungana na timu ziku yoyote kuanzia kesho kujiandaa na safari ya Oman, ambayo imepangwa kufanyika kabla ya taerehe 6 Januari. Timu itakaa huko kwa siku 14. Itacheza mechi si chini ya tano lakini si zaidi ya sita kwa muda wote watakaokaa huko.

Baada ya hapo watarejea nchini kabla ya Januari 25, ambapo watakuwa na mechi ya ufunguzi wa Ligi mzunguko wa pili dhidi ya Oljoro JKT katika uwanja wa Mkwakwani saa kumi alasiri.

HAFIDH KIDO
MSEMAJI- COASTAL UNION
27 DEC, 2013
TANGA, TANZANIA

No comments:

Post a Comment