Aliyempa jina la Messi hajakosea, mtoto huyu ana uwezo mkubwa wa kuondoka na kijiji na katibu tarafa wake.
Kocha wa Taifa Stars, Kim Poulsen ametangaza
timu ya pili ya Taifa (Young Taifa Stars) atakayoitumia kuangalia wachezaji
ambao baadaye anaweza kuwajumuisha kwenye timu ya wakubwa.
Akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam jumanne
Aprili 23, Kim amesema timu hiyo ni sehemu ya mpango wa maendeleo wa Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) uliozinduliwa Aprili 4 mwaka huu ukilenga
kuendeleza wachezaji.
“Huu ni mpango wa kuendeleza vipaji Tanania na timu
hii inajumuisha wachezaji ambao wamepita umri wa kuchezea timu ya Taifa ya
vijana wenye umri chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes) na wakubwa ambao
hawajapata fursa ya kuingia Taifa Stars, lakini nitatumia Young Taifa Stars kuangalia
uwezo wao.
“Timu hii ni kiungo kati ya vijana na wakubwa.
Wengi wa wachezaji watakuwa vijana, lakini wakubwa wachache watapata fursa ya
kuwemo ili kuangalia uwezo wao hata kama huko
nyuma waliwahi kuchezea Taifa Stars. Lakini timu hii vilevile ni changamoto kwa
wachezaji wa Taifa Stars kuwa wapo wanaosubiri wazembee ili wachukue nafasi
zao,” amesema.
Young Taifa Stars yenye wachezaji 30 itakuwa na
kambi ya siku tano jijini Dar es
Salaam kuanzia Mei 2 hadi 6 mwaka huu.
Wachezaji walioitwa ni Aishi Manula (Azam),
Hussein Shariff (Mtibwa Sugar) na Ali Mustapha (Yanga) ambao ni makipa. Mabeki
ni Kessy Hassan (Mtibwa Sugar), Kennan Ngoma (Barnsley FC, Uingereza), Himid
Mao (Azam), Ismail Gambo (Azam), David Mwantika (Azam), Miraji Adam (Simba),
Mohamed Hussein (Kagera Sugar), Waziri Salum (Azam), Samih Nuhu (Azam) na Emily
Mgeta (Simba).
Viungo ni Haruna Chanongo (Simba), Edward
Christopher (Simba), Mudathiri Yahya (Azam), William Lucian (Simba), Jonas
Mkude (Simba), Hassan Dilunga (Ruvu Shooting), Jimmy Shoji (JKT Ruvu), Abdallah
Seseme (Simba), Ramadhan Singano (Simba), Farid Mussa (Azam) na Vicent Barnabas
(Mtibwa Sugar).
Washambuliaji ni Hussein Javu (Mtibwa Sugar),
Jerome Lambele (Ashanti United), Zahoro Pazi (JKT Ruvu), Twaha Hussein (Coastal
Union), Abdallah Karihe (Azam) na Juma Luizio (Mtibwa Sugar).
Akizungumza na blog ya Coastal Union Ibrahim
Twaha ‘Messi’ alisema anashukuru sana
kuona juhudi zake zinatambuliwa na kocha Kim, kwani hakutegemea kabisa kuitwa
katika kikosihicho cha wachezaji 30.
“Kwanza
nimshukuru Mwenyezi Mungu kwa hatua niliyofikia, ni ndoto zangu za siku nyingi
kucheza timu ya Taifa ya wakubwa, tayari nimeshachezea timu ya wadogo na sasa
ni wakati wangu kuonyesha uwezo. Nitahakikisha nafanya vema na nitaingia rasmi
timu ya wakubwa,” alisema Twaha.
Kutoka Coastal Union wawakilishi wa wachezaji
chini ya umri wa miaka 20 walikuwa ni Ibrahim twaha na Ramadhan Shame ‘Batista’,
lakini kwa bahati mbaya ‘Batista’ hajapata bahati ya kuingia kwenye kikosi
hicho.
COASTAL UNION
APRILI 23, 2013
DAR ES SALAAM ,
TANZANIA
</
No comments:
Post a Comment