Shirikisho la soka Tanzania (TFF) limerudisha
nyuma siku moja mechi kati ya Coastal Union na Azam iliyokuwa ichezwe jumamosi
na sasa itachezwa ijumaa kwenye uwanja wa Mkwakwani Tanga.
Ofisa habari wa TFF, Boniface Wambura alisema
awali mechi hiyo namba 168 ilikuwa ichezwe Aprili 27, lakini imerudishwa nyuma kwa
siku moja ili kuipa nafasi Azam FC kujiandaa kwa mechi ya marudiano ya raundi
ya pili ya kombe la shirikisho dhidi ya AS FAR Rabat ya Morocco itakayochezwa
kati ya Mei 3, 4 au 5 nchini Morocco.
Katika mchezo huo wa ugenini Azam inahitaji
ushindi wa aina yoyote au sare ya mabao kufuzu kwa hatua ya 16 bora katika
michuano hiyo yenye heshima kubwa barani Afrika.
Katika hatua nyingine mechi ya pili ya
Coastal Union itakayochezwa Mei 1, katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam
dhidi ya Yanga, ndiwo mchezo utakaoamua hatma ya ubingwa wa Yanga kwa msimu huu
baada ya kushinda mechi iliyopita dhidi ya JKT Ruvu na kujizolea point 56 hivyo
kubakisha point moja tu kufikisha point 57 ambazo hakuna timu yoyote
itakayoweza kufikisha point hizo.
Hivyo ili kulinda heshima ya timu kutogeuka
daraja la kuwapa watu ubingwa lazima vijana wa Tanga kucheza mpira wa uhakika
ili kuwanyamazisha Yanga kama walivyofanya Mgambo
JKT kutoka Tanga wiki iliyopita uwanja wa Mwakwani.
Baada ya mchezo na Azam halafu Yanga, timu ya
Coastal Union yenye point 33 katika nafasi ya sita itabakisha mchezo mmoja
dhidi ya Polisi Morogoro utakaochezwa katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro
mwezi wa tano.
COASTAL UNION
23 April, 2013
No comments:
Post a Comment