Juma Mgunda akipozi huku anakula njugu, enzi zake huo mwili ulikuwa tishio sana kwa mabeki dhaifu.
Hussein Mwakuluzo Ruga akiwa na familia yake nchini Uingereza anakosihi kwa sasa baada ya kustaafu soka.
Mkurugenzi wa ufundi Coastal Union Nassor Ahmed 'Binslum' ametangaza donge nono kwa shabiki ama mtu yoyote atakaye fanikiwa kuleta mshambuliaji mwenye uchu wa magoli katika kikosi cha wagosi wa kaya.
Alizungumza hayo jana wakati wa kuchangia picha ya mshambuliaji hatari wa timu hiyo Juma Mgunda iliyowekwa katika ukurasa wa facebook na mwanahistoria wa Wagosi Ally Kiraka, ambapo alionyesha kuunga mkono maneno ya mwanandinga mwingine wa zamani wa timu hiyo Hussein Mwakuluzo aliyesikitishwa na viwango vya uchezaji kwa sasa barani ulaya.
"Tokea ligi imeisha natafuta 'striker' mmoja tu na mpaka sasa sijapata si hapa kwetu wala Kenya au Uganda, mmoja tu wa ukweli anayejua kufunga japo nusu ya mgunda sijaona...........sasa natoa nafasi miongoni mwetu Kama kuna striker unafikiri unamjua atakae tufungia goli 15 TU tuletee na wewe utakayetuletea bakhsish juu utapata, haya tusaidiane wadau...!!!!," alisema Binslum.
Awali akichangia mada katika picha hiyo Hussein Mwakuluzo Ruga aliyewika na kikosi kilichotwaa ubingwa wa soka Tanzania mwaka 1988 ambaye kwa sasa anaishi nchini Uingereza na familia yake alisema:
"Mimi nasikia uchungu nikiwaangalia hawa wachezaji wanaosifiwa huku, Wakati uwezo wao ni Wa kawaida sana, wanalipwa hela za ajabu, wanaishi maisha ya ajabu! Wanaendesha magari ya ajabu na wanakaa kwenye nyumba hazina mfano....
Uwezo wao ni Wa kawaida sana Nassor , mchezaji hata kuzuia mpira hawezi! Yaani ....IF I HAD A CHOICE, I WOULD'VE LIKE TO PLAY NOW....THAN IN THE PAST!!," alisisitiza Ruga.
Kutokana na kumfahamu sana Mgunda, Ruga alileta historia fupi ya mchezaji huyo ambaye alikuwa kama ndugu yake maana kila siku alikuwa akienda naye kwa barabara ya sita Tanga na familia ya kina Ruga ilimchukulia kama ndugu yao hasa ikizingatiwa alikuwa mgeni mjini Tanga.
"Juma Mgunda !!!!! Alitokea cda ya Dodoma bonge la mchezaji alikuwa na vitu vyote alikuwa ana nguvu, anapiga mashuti na ni hodari Wa kupiga vichwa! Pamoja na yote hayo huyu jamaa ni mstaarabu sana ndani na nje ya uwanja, naona ni hadhi kubwa kuweza kucheza na huyu kaka.
"Mimi nimeshaona mechi nyingi hapa England na nimeona wachezaji wanaosifiwa kwamba ni wazuri na wanalipwa mamilioni ya paundi, lakini kila nikiwaangalia hawamfikii huyu jamaa. Ni bahati mbaya kazaliwa Afrika hivi jamani nisaidieni iwapo wellbeck anachezea Man United na England, na kwa maoni yangu hamfikii Juma hata nusu. Na ninathubutu kusema angekuwa Coastal ile ya kwetu miaka ile huyu wellbeck asingepata nafasi ya kupangwa....." Ruga.
Katika hatua nyingine Coastal Union imeshafanya usajili wa nguvu wa wachezaji wanane wanaotokea timu za hapa nyumbani, ingawa kwa maelezo ya Mwenyekiti wa timu hiyo Hemed Hilal 'Aurora, wamebakisha nafasi mbili tu za kusajili ambapo wanatafuta striker na kiungo mshambuliaji.
COASTAL UNION
costalunion@gmail.com
18 June, 2013
DAR ES SALAAM, TANZANIA
No comments:
Post a Comment