Danny Lyanga akiminyana na wachezaji wa Mgambo Shooting katika game ya jana uwanja wa Mkwakwani Tanga ambapo Mgambo waliibuka na ushindi wa mabao 2-0.
Hamadi Juma akimimina majaro langoni mwa Mgambo Shooting jana.
Mohammed Miraji wa Coastal Union akitafuta mbinu za kumchomoka mchezaji wa Mgambo jana.
Yayo Kato Lutimba akiwa katikati ya wachezaji wa Mgambo jana uwanja wa Mkwakwani.
Yayo Kato akiwa katika harakati zake.
Suleiman Kassim 'Selembe' akiwania mpira na chezaji wa Mgambo katika uwanja wa Mkwakwani jana.
Danny Lyanga jana alikuwa na jezi ya peke yake haina tangazo la Pembe... Why?
Danny Lyanga akicheza pembezoni mwa chaki huku mchezaji wa Mgambo akitafuta mbinu ya kumuibia mpira.
Kwa matokeo hayo Mgambo wamesogea kidogo kujiepusha na kushuka daraja, na Coastal Union imebaki na point 29 ikiwa nafasi ya 8 katika msimamo. Mechi mbili zilizobaki za nyumbani ni kati ya JKT Ruvu na Kagera Sugar.
COASTAL UNION
7 APRIL, 2014
TANGA TANZANIA
Sunday, April 6, 2014
Sunday, March 23, 2014
Simba 0-1 Coastal Union
Kabla ya mechi kuanza katika kambi ya Coastal Union, viongozi walikusanyika kuwapa somo wachezaji. Hapa anaonekana Mwenyekiti wa klabu Hemed Hilal, 'Aurora' akisisitiza jambo huku Makamu wake Steven Mnguto akifuatilia kwa makini.
Wakati mlinda mlango wa Coastal Union, Fikirini Selemeni, akiingia uwanjani leo uwanja mzima ulisema hawezi kufanya kitu. Hata mlinda mlango wa Simba, Ivo mapunda alimkebehi 'Dogo utaweza' Fikirini alicheka tu na kuangalia chini kwa aibu. Ila kilichofuata baada ya mechi kila mmoja alitaka kupiga nae picha.
Danny Lyanga, winga wa Coastal Union alikuwa mwiba kwa mabeki wa pembeni wa Simba siku ya leo.
Winga wa Coastal Union, Kenneth Masumbuko aakitafuta mbinu za kumtoka mchezaji wa Siba katika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam leo, mechi iliisha kwa ushindi kwa Wagosi wa bao 1-0.
Kiungo wa Coastal Union, Behewa Sembwana akiwa amewekwa mtu kati na wachezaji wa Simba leo.
Mwamuzi wa leo alishindwa kujizuia alipoona golikipa wa Simba, Ivo Mapunda ameweka taulo kubwa kwenye nyavu za lango lake.
Danny Lyanga akikimbizana na mchezaji wa Simba, Jonas Mkude huku Joseph Owino wa Simba akiwa tayari kumpa msaada Mkude.
Suleiman Kassim 'Selembe', akitafuta mbinu za kumtoka mchezaji wa Simba katika uwanja wa taifa leo.
Hali ilikuwa tete kocha Simba na msaidizi wake.....
Kenneth Masumbuko leo alipiga kazi mpaka bukta yake ikapasuka..... Upo juu winga wetu.
Kocha wa Magolikipa Coastal Union, meja akionyesha matunda ya kazi yake, Mansour Alawi, kulia na Fikirini Selemeni kushoto. Baada ya mechi kuisha.
Mwenyekiti Hemed Hilal, alisindwa kujizuia akamuinua golikipa wa Coastal Union ambae ni kijana mdogo aliefanya maajabu makubwa uwanja wa Taifa leo.
Bao pekee la dakika ya 44 lililoingizwa kimiani na beki Hamadi Juma, baada ya kupokea pasi ya mwisho kutoka kwa Razak Khalfan ndilo lililopeleka kilio mtaa wa Msimbazi baada ya bao hilo kudumu mpaka dakika ya 90.
Coastal Union ambayo ilikuwa na wachezaji chipukizi ilionyesha uhai kwa dakika zote 45 za awali mpaka kupata bao dakika moja kabla ya filimbi ya mapumziko.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi upande wa Simba, ambapo mshambuliaji Ramadhan Singano 'Messi' ndie pekee alionekana hatari lakini umakini wa golikipa Fikirini, alieonekana mpya machoni mwa wengi ulisaidia kuiondoa Coastal Union kichwa chini katika uwanja wa ugenini leo.
Aidha beki wa kati Yusuf Chuma aliyumia vema urefu wake kwa kuokoa mipira mingi ya juu, huku Kibacha, Hamadi na Banda wakizuia kwa nguvu kuhakikisha ngome ya wagosi inaendelea kuwa iara.
Kikosi cha leo kilichoanza dhidi ya Simba ni: Fikirini Suleiman, Hamadi Juma, Abdi Banda, Yusuf Chuma, Mbwana Kibacha, Razak Khalfan, Ally Nassor ‘Ufudu’, Behewa Sembwana, Suleiman Kassim ‘Selembe’, Kenneth Masumbuko, Danny Lyanga.
Wachezaji wa akiba ni: Mansour Alawi, Ayoub Masoud, Marcus Ndeheli, Ayoub Semtawa, Mohammed Miraji, Crispian Odula, na Mohammed Kipanga.
Baadae Kocha aliwatoa Ally Nassor, Hamadi Juma na Suleiman Kassim, wakaingia Mohammed Miraji, Ayoub Masoud na Marcus Ndeheli.
Kwa matokeo hayo Coastal Union imevuna point tatu na kufikisha jumla ya point 30, na kupaa hadi nafasi ya saba ikisubiri kucheza na Mtibwa Sugar katika uwanja wa Manungu mjini Morogoro.
COASTAL UNION
23 MARCH, 2014
DAR ES SALAAM, TANZANIA

Wednesday, March 19, 2014
Coastal Union mwendo mdundo.
Wachezaji wa Coastal Union wakiwa mazoezini uwanja wa De Souza, leo asubuh.
Kocha wa Coastal Union, Yusuf Chipo akiangalia vijana wake hawapo pichani.
Katibu wa Coastal Union, Mwalimu Kassim Siagi akibadilishana mawazo na Kocha Chipo katika mazoezi ya timu leo asubuhi mjini Tanga.
Kocha masaidizi wa Coastal Union, Ally Jangalu akiangalia vijana wake wakifanya amzoezi ya kumiliki mpira na kutoa pasi fupi katika uwanja wa De Souza leo asubihi mjini Tanga.
Kocha Chipo akiwa na Kit Manager Mohammed baada ya amzoezi mjini Tanga leo asubuhi.
19 March, 2014
Tanga, Tanzania

Saturday, March 15, 2014
Azam FC Vs Coastal Union
Mwenyekiti wa Coastal Union, Hemed Hilal akifuatilia mechi kwa umakini uwanja wa Chamazi leo, ambapo Wagosi wa kaya walilala 4-0.
Coastal Union , Nyumba wakifuatilia mchezo wa leo uwanja wa Azam Complex, Chamazi.
Wachezaji walichelewa kuingia uwanjani, hivyo iliwapasa kupasha viungo harakaharaka.
Kocha alianza kuudhika mapema kutokana na ubovu wa utaratibu uliotumika kuwapeleka wachezaji uwanjani.
Abdi Banda kiminyana na mchezajiwa Azam, huku Kenneth Masumbuki akiwa tayari kumpa msaada.
Danny Lyanga akituliza mpira mbele ya mchezaji wa Azam leo.
Kenneth Masumbuko.
Mashabiki wa Azam leo walikuwa na furaha kupita kiasi.
Danny Lyanga akitafuta mbinu za kumtoka mchezaji wa Azam ili amimine krosi katika lango la timu hiyo.
Haruna Msohi Boban na Danny Lyanga wakisubiri kona ipigwe na Abdi Banda huku golikipa wa Azam, Mwadini Ally akiwa makini kuhakikisha hakutokei hatari yoyote.
Kocha wa Azam akionyesha ishara ya vidole viwili kwa wachezaji wake akimaanisha Man to Man.
Kocha wa Simba nae alikuwepo kuangalia mechi ya Coastal ili mechi ijayo ambapo Simba inacheza na sisi.
Zamil Khalfan, shabiki wa Coastal Union aliamua hasira zake za kuchapwa nne kimya, akae peke yake.
It was indeed a bad experience at Chamazi.
Yusuf Chipo, akiwa hana la kufanya.
Kocha akizungumza na Danny Lyanga walau abadilishe mchezo lakini hakuna kilichofanyika.
Mara nyingine unaweza kuamua kucheka uchungu ili usiumie sana.
kikosi cha leo: Said Lubawa, Hamadi Juma, Abdi Banda, Mbwana Kibacha, Juma Nyoso, Jerry Santo, Danny Lyanga, Ally Nassor, Kenneth Masumbuko, Haruna Moshi, Mohammed Miraji.
Baadae walitoka Ally Nassor, Kenneth Masumbuko na Mohammed Miraji wakaingia, Yayo Kato, Behewa Sembwana na Ayoub Semtawa.
Mabao ya leo yalifungwa na Kipre Tchetche dakika za 23 na 38 kipindi cha kwanza. Na kipindi cha pili John Bocco dakika ya 64 bao la nne likamaliziwa na Kelvin dakika ya 90. Mabao yote ni makosa ya mabeki.
COASTAL UNION
15 MARCH, 2014

Wednesday, March 12, 2014
Mabadiliko ya ratiba, Ligi Kuu Tanzania Bara.
Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imeifanyia marekebisho ratiba ya
Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) ambapo sasa itamalizika Aprili 19 mwaka huu badala ya
Aprili 27 mwaka huu.
Marekebisho hayo yamefanyika ili kutoa fursa kwa timu ya Taifa (Taifa
Stars) kujiandaa kwa mechi za mchujo la Kombe la Afrika 2015 ambapo itacheza
raundi ya awali Mei mwaka huu.
Kutokana na marekebisho hayo, Yanga itacheza na Prisons (Uwanja wa
Taifa) Machi 26 mwaka huu katika mechi ya raundi ya 17 wakati Machi 19 mwaka
huu kwenye uwanja huo huo ni Yanga na Azam.
Machi 15 mwaka huu kutakuwa na mechi mbili; Azam na Coastal (Azam
Complex), na Mtibwa Sugar itacheza na Yanga (Jamhuri). Mgambo na Azam zitacheza
Machi 26 mwaka huu Mkwakwani, na Aprili 9 mwaka huu Yanga itaialika Kagera
Sugar (Taifa).
Raundi ya 22 itaanza Machi 22 mwaka huu kwa mechi kati ya Kagera vs
Prisons (Kaitaba), JKT Ruvu vs Mbeya City (Azam Complex), na Rhino vs Yanga
(Ali Hassan Mwinyi). Machi 23 mwaka huu ni Simba vs Coastal (Taifa), Mgambo vs
Mtibwa (Mkwakwani), Ruvu Shooting vs Ashanti (Mabatini) na Azam vs Oljoro (Azam
Complex).
Machi 29 mwaka huu itaanza raundi ya 23 kwa mechi kati ya Ashanti
vs Oljoro (Azam Complex) wakati Machi 30 ni Mbeya City vs Prisons (Sokoine),
Kagera vs Ruvu Shooting (Kaitaba), Mtibwa vs Coastal (Manungu), JKT Ruvu vs
Rhino (Azam Complex), Azam vs Simba (Taifa), na Mgambo vs Yanga (Mkwakwani).
Raundi ya 24 inaanza Aprili 5 mwaka huu kwa Kagera vs Simba
(Kaitaba), Ashanti vs Mbeya City (Azam Complex). Aprili 6 mwaka huu ni Coastal
vs Mgambo (Mkwakwani), Oljoro vs Prisons (Sheikh Kaluta Amri Abeid), Rhino vs
Mtibwa (Ali Hassan Mwinyi), Ruvu Shooting vs Azam (Mabatini) na Yanga vs JKT
Ruvu (Taifa).
Aprili 12 mwaka huu inaanza raundi ya 25 kwa Mtibwa vs Ruvu Shooting
(Mabatini), Coastal vs JKT Ruvu (Mkwakwani), Prisons vs Rhino (Sokoine). Aprili
13 mwaka huu ni Mgambo vs Kagera (Mkwakwani), Simba vs Ashanti (Taifa), Mbeya
City vs Azam (Sokoine) na Oljoro vs Yanga (Sheikh Kaluta Amri Abeid).
Raundi ya 26 ni Aprili 19 mwaka huu kwa Rhino vs Ruvu Shooting (Ali
Hassan Mwinyi), Mbeya City vs Mgambo (Sokoine), Prisons vs Ashanti (Jamhuri,
Morogoro), JKT Ruvu vs Azam (Azam Complex), Oljoro vs Mtibwa (Sheikh Kaluta
Amri Abeid), Coastal vs Kagera (Mkwakwani) na Yanga vs Simba (Taifa).
COASTAL UNION
TANGA, TANZANIA
12 MARCH, 2014
Saturday, March 8, 2014
Coastal Union 0-0 Ashanti UTD
Kocha wa Ashanti UTD, Abdallah King Kibadeni akifuatilia mchezo wa jana, baada ya mechi alisema amefurahishwa na suluhu kwani aliipokea timu ikiwa taaban kazi yake ni kuhakikisha haishuki daraja ili ajipange kwa msimu ujao.
Vifaa hivi vya Wagosi, kutoka kushoto Haruna Moshi 'Boban', Mbwana Kibacha, Abdi Banda, Juma Nyoso, Jerry Santo na Shaaban Kado.
Mamaaaa Aminaaaaaa '...'
Crispian Odula akipiga shuti langoni mwa Ashanti, huku Danny akijiandaa kuenda kuleta mishemishe langoni.
Mwamuzi wa jana Alex Mahagi akimwangalia Ally Nassor 'Ufudu' na mchezaji wa Ashanti wakiminyana katika uwanja wa Mkwakwani jana.
Kenneth Masumbuki akitafuta mbinu za kumtoka mchezaji wa Ashanti jana.
"Niachie bwanaaaa" Danny Lyanga
Haruna Moshi 'Boban' akiwa amevurugwa jana.
Mkurugenzi wa Ufundi Coastal Union Nassor Binslum(mwenye kofia) akionyeshwa kitu na Katibu wa timu hiyo Kassim Siagi uwanja wa Mkwakwani jana.
Mwenyekiti wa Coastal Union (kushoto) akiwa na mwenyekiti wa chama cha soka Dar es Salaam, ambae pia ni shabiki mkubwa wa Ashanti UTD, Almas Kasongo jana Mkwakwani.
Masumbuuukooo... in the move.
Abdi Banda akiwa na mpira huku akiwa hajui afanye nini, apige pasi ama aombe Mungu.

TIMU ya soka
Tanzania Coastal Union ‘Wagosi wa Kaya’ wamelazimisha suluhu ya bila kufungana
na Ashanti UTD katika dimba lao la kujidai la Mkwakwani jijini Tanga.
Katika
mchezo huo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Wagosi walionekana kuwa makini kuanzia
dakika ya kwanza baada ya kipyenga cha mwamuzi kutoka Mwanza, Alex Mahagi
kupulizwa huku mashabiki wa timu hiyo wakiwa na hamasa ya ushindi.
Aidha,
kudhihirisha Wagosi walikuwa na nia ya kuwaumiza vijana wa Ilala Ashanti UTD
iliyoanzishwa mwaka 2004, dakika ya kwanza walipata kona iliyochongwa na winga
hatari Danny Lyana lakini kwa bahati mbaya haikuzaa matunda.
Mchezo wa
jana uliendelea hivyohivyo kwa Wagosi kulisakama lango la Ashanti, huku
wapinzani wao wakifanya mashambulizi ya kushtukiza lakini umakini wa mabeki
wazoefu na uimara wa golikipa Shaaban Kado, alietoka kuitumikia nchi yake
nchini Namibia uliwanyima mabao Ashanti.
Ilipotimu
dakika ya 33, kipindi cha kwanza beki wa kati wa Wagosi, Juma Nyoso alipata
pasi muru akutoka kwa Abdi Banda ambae nae alikuwa nchini Namibia katika kikosi
cha Taifa Stars waliotoka suluhu ya 1-1. Nyoso aliupokea vizuri mpira huo na
kuwazidi ujanja mabeki wa Ashanti akabaki na golikipa akaupiga kiufundi lakini
ulipaa juu sentimeta chache mashabiki wa Wagosi wakainuka.
Dakika chache
baadae Haruna Moshi ‘Boban’ alikosa bao la wazi baada ya kuwekewa na Crispian
Odula lakini shuti lake alilolipiga kiufundi lilitoka nje.
Hata hivyo
baada ya mishemishe nyingi katika lango la Ashanti ambazo hazikuzaa matunda,
vijana hao wa Ilala walibadilika na kuanza kulisakama lango la Wagosi ambapo
walipata nafasi tatu za harakaharaka lakini ilikuwa bahati tu wala si ufundi wa
Kado uliosaidia kutotikisika nyavu katika lango la Wagosi walioonyesha kuishiwa
mbinu.
Kipindi cha
kwanza kiliisha hivyo bila timu yoyote kuona lango la mwenzake. Wachezaji
walikwenda mapumziko wakisindikizwa na makocha wao King Abdallah Kibaden wa
Ashanti na Yusuf Chipo wa Coastal Union.
Kipindi cha
pili Coastal Union walifanya mabadiliko kwa dakika tofauti ambapo walitoka Crispian
Odula na Ally Nassor ‘Ufudu’, na kuingia Yayo kato na Mohammed Mtindi.
Mabadiliko
hayo yaliamsha ari ya ushambuliaji lakini dakika ya 49 kipindi cha pili Danny
Lyanga aliwanyima furaha mashabiki wa Coastal Union, baada ya kushindwa
kumalizia kazi nzuri na Kenneth Masumbuko aliewazidi mbio mabeki wawili wa
Ashanti na kupiga krosi muru iliyomkuta Danny yeye na golikipa wa Ashanti
lakini akapiga fyongo.
Hali
iliendelea kuwa ya piga nikupige mpaka ilipotimu dakika ya 65 golikipa wa
Wagosi Shaaban Kado aligongana na mchezaji wa Ashanti akaumia mkono hivyo
kushindwa kuendelea na mchezo akaingia golikipa namba mbili Said Lubawa, ambae
alimudu kulinda lango hilo.
Kosa kosa
zilikuwa nyingi kwa pande zote mbili ambapo Yayo Kato alishindwa kucheka na nyavu mara mbili akiwa eneo la hatari.
Kwa matokeo
hayo ya 0-0, Ashanti watoto wa jiji wameambulia point moja na kuendelea
kudunduliza point zao ambapo kwa sasa wana point 18, katika nafasi ya 12
wakigombania kutoshuka daraja.
Wagosi wa
Kaya nao wameshuka mpaka nafasi ya saba kutoka ya sita baada ya kuambulia point
26, wakiwa nyumba ya Kagera Sugar wenye point 29 nafasi ya tano, huku Ruvu
Shooting wakikwea mpaka nafasi ya sita kutoka ya nane baada ya kuwachapa
Tanzania Prisons, bao 1-0 mjini Mbeya jana na kujizolea point 28.
Mechi ijayo
Wagosi watasafiri mpaka Dar es Salaam, kumenyana na Simba katika uwanja wa
Taifa. Lakini mpaka sasa haijajulikana mechi hiyo itachezwa lini ambayo katika
ratiba inaonyesha ni Jumatano Machi 12, lakini zipo taarifa kuwa viongozi wa
Simba na Coastal Union wameiomba TFF kupitia kamati ya ligi, kuwa meci hiyo
isogezwe mpaka Jaumamosi Machi 15 kwa lengo la kupata mashabiki wengi.
COASTAL
UNION
TANGA,
TANZANIA
9 MACHI,
2014
Subscribe to:
Posts (Atom)