Mwenyekiti wa Coastal Union, Hemed Hilal akifuatilia mechi kwa umakini uwanja wa Chamazi leo, ambapo Wagosi wa kaya walilala 4-0.
Coastal Union , Nyumba wakifuatilia mchezo wa leo uwanja wa Azam Complex, Chamazi.
Wachezaji walichelewa kuingia uwanjani, hivyo iliwapasa kupasha viungo harakaharaka.
Kocha alianza kuudhika mapema kutokana na ubovu wa utaratibu uliotumika kuwapeleka wachezaji uwanjani.
Abdi Banda kiminyana na mchezajiwa Azam, huku Kenneth Masumbuki akiwa tayari kumpa msaada.
Danny Lyanga akituliza mpira mbele ya mchezaji wa Azam leo.
Kenneth Masumbuko.
Mashabiki wa Azam leo walikuwa na furaha kupita kiasi.
Danny Lyanga akitafuta mbinu za kumtoka mchezaji wa Azam ili amimine krosi katika lango la timu hiyo.
Haruna Msohi Boban na Danny Lyanga wakisubiri kona ipigwe na Abdi Banda huku golikipa wa Azam, Mwadini Ally akiwa makini kuhakikisha hakutokei hatari yoyote.
Kocha wa Azam akionyesha ishara ya vidole viwili kwa wachezaji wake akimaanisha Man to Man.
Kocha wa Simba nae alikuwepo kuangalia mechi ya Coastal ili mechi ijayo ambapo Simba inacheza na sisi.
Zamil Khalfan, shabiki wa Coastal Union aliamua hasira zake za kuchapwa nne kimya, akae peke yake.
It was indeed a bad experience at Chamazi.
Yusuf Chipo, akiwa hana la kufanya.
Kocha akizungumza na Danny Lyanga walau abadilishe mchezo lakini hakuna kilichofanyika.
Mara nyingine unaweza kuamua kucheka uchungu ili usiumie sana.
kikosi cha leo: Said Lubawa, Hamadi Juma, Abdi Banda, Mbwana Kibacha, Juma Nyoso, Jerry Santo, Danny Lyanga, Ally Nassor, Kenneth Masumbuko, Haruna Moshi, Mohammed Miraji.
Baadae walitoka Ally Nassor, Kenneth Masumbuko na Mohammed Miraji wakaingia, Yayo Kato, Behewa Sembwana na Ayoub Semtawa.
Mabao ya leo yalifungwa na Kipre Tchetche dakika za 23 na 38 kipindi cha kwanza. Na kipindi cha pili John Bocco dakika ya 64 bao la nne likamaliziwa na Kelvin dakika ya 90. Mabao yote ni makosa ya mabeki.
COASTAL UNION
15 MARCH, 2014
DAR ES SALAAM, TANZANIA
No comments:
Post a Comment