Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imeifanyia marekebisho ratiba ya
Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) ambapo sasa itamalizika Aprili 19 mwaka huu badala ya
Aprili 27 mwaka huu.
Marekebisho hayo yamefanyika ili kutoa fursa kwa timu ya Taifa (Taifa
Stars) kujiandaa kwa mechi za mchujo la Kombe la Afrika 2015 ambapo itacheza
raundi ya awali Mei mwaka huu.
Kutokana na marekebisho hayo, Yanga itacheza na Prisons (Uwanja wa
Taifa) Machi 26 mwaka huu katika mechi ya raundi ya 17 wakati Machi 19 mwaka
huu kwenye uwanja huo huo ni Yanga na Azam.
Machi 15 mwaka huu kutakuwa na mechi mbili; Azam na Coastal (Azam
Complex), na Mtibwa Sugar itacheza na Yanga (Jamhuri). Mgambo na Azam zitacheza
Machi 26 mwaka huu Mkwakwani, na Aprili 9 mwaka huu Yanga itaialika Kagera
Sugar (Taifa).
Raundi ya 22 itaanza Machi 22 mwaka huu kwa mechi kati ya Kagera vs
Prisons (Kaitaba), JKT Ruvu vs Mbeya City (Azam Complex), na Rhino vs Yanga
(Ali Hassan Mwinyi). Machi 23 mwaka huu ni Simba vs Coastal (Taifa), Mgambo vs
Mtibwa (Mkwakwani), Ruvu Shooting vs Ashanti (Mabatini) na Azam vs Oljoro (Azam
Complex).
Machi 29 mwaka huu itaanza raundi ya 23 kwa mechi kati ya Ashanti
vs Oljoro (Azam Complex) wakati Machi 30 ni Mbeya City vs Prisons (Sokoine),
Kagera vs Ruvu Shooting (Kaitaba), Mtibwa vs Coastal (Manungu), JKT Ruvu vs
Rhino (Azam Complex), Azam vs Simba (Taifa), na Mgambo vs Yanga (Mkwakwani).
Raundi ya 24 inaanza Aprili 5 mwaka huu kwa Kagera vs Simba
(Kaitaba), Ashanti vs Mbeya City (Azam Complex). Aprili 6 mwaka huu ni Coastal
vs Mgambo (Mkwakwani), Oljoro vs Prisons (Sheikh Kaluta Amri Abeid), Rhino vs
Mtibwa (Ali Hassan Mwinyi), Ruvu Shooting vs Azam (Mabatini) na Yanga vs JKT
Ruvu (Taifa).
Aprili 12 mwaka huu inaanza raundi ya 25 kwa Mtibwa vs Ruvu Shooting
(Mabatini), Coastal vs JKT Ruvu (Mkwakwani), Prisons vs Rhino (Sokoine). Aprili
13 mwaka huu ni Mgambo vs Kagera (Mkwakwani), Simba vs Ashanti (Taifa), Mbeya
City vs Azam (Sokoine) na Oljoro vs Yanga (Sheikh Kaluta Amri Abeid).
Raundi ya 26 ni Aprili 19 mwaka huu kwa Rhino vs Ruvu Shooting (Ali
Hassan Mwinyi), Mbeya City vs Mgambo (Sokoine), Prisons vs Ashanti (Jamhuri,
Morogoro), JKT Ruvu vs Azam (Azam Complex), Oljoro vs Mtibwa (Sheikh Kaluta
Amri Abeid), Coastal vs Kagera (Mkwakwani) na Yanga vs Simba (Taifa).
COASTAL UNION
TANGA, TANZANIA
12 MARCH, 2014
No comments:
Post a Comment