Wakati mlinda mlango wa Coastal Union, Fikirini Selemeni, akiingia uwanjani leo uwanja mzima ulisema hawezi kufanya kitu. Hata mlinda mlango wa Simba, Ivo mapunda alimkebehi 'Dogo utaweza' Fikirini alicheka tu na kuangalia chini kwa aibu. Ila kilichofuata baada ya mechi kila mmoja alitaka kupiga nae picha.
Danny Lyanga, winga wa Coastal Union alikuwa mwiba kwa mabeki wa pembeni wa Simba siku ya leo.
Winga wa Coastal Union, Kenneth Masumbuko aakitafuta mbinu za kumtoka mchezaji wa Siba katika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam leo, mechi iliisha kwa ushindi kwa Wagosi wa bao 1-0.
Kiungo wa Coastal Union, Behewa Sembwana akiwa amewekwa mtu kati na wachezaji wa Simba leo.
Mwamuzi wa leo alishindwa kujizuia alipoona golikipa wa Simba, Ivo Mapunda ameweka taulo kubwa kwenye nyavu za lango lake.
Danny Lyanga akikimbizana na mchezaji wa Simba, Jonas Mkude huku Joseph Owino wa Simba akiwa tayari kumpa msaada Mkude.
Suleiman Kassim 'Selembe', akitafuta mbinu za kumtoka mchezaji wa Simba katika uwanja wa taifa leo.
Hali ilikuwa tete kocha Simba na msaidizi wake.....
Kenneth Masumbuko leo alipiga kazi mpaka bukta yake ikapasuka..... Upo juu winga wetu.
Kocha wa Magolikipa Coastal Union, meja akionyesha matunda ya kazi yake, Mansour Alawi, kulia na Fikirini Selemeni kushoto. Baada ya mechi kuisha.
Mwenyekiti Hemed Hilal, alisindwa kujizuia akamuinua golikipa wa Coastal Union ambae ni kijana mdogo aliefanya maajabu makubwa uwanja wa Taifa leo.
Bao pekee la dakika ya 44 lililoingizwa kimiani na beki Hamadi Juma, baada ya kupokea pasi ya mwisho kutoka kwa Razak Khalfan ndilo lililopeleka kilio mtaa wa Msimbazi baada ya bao hilo kudumu mpaka dakika ya 90.
Coastal Union ambayo ilikuwa na wachezaji chipukizi ilionyesha uhai kwa dakika zote 45 za awali mpaka kupata bao dakika moja kabla ya filimbi ya mapumziko.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi upande wa Simba, ambapo mshambuliaji Ramadhan Singano 'Messi' ndie pekee alionekana hatari lakini umakini wa golikipa Fikirini, alieonekana mpya machoni mwa wengi ulisaidia kuiondoa Coastal Union kichwa chini katika uwanja wa ugenini leo.
Aidha beki wa kati Yusuf Chuma aliyumia vema urefu wake kwa kuokoa mipira mingi ya juu, huku Kibacha, Hamadi na Banda wakizuia kwa nguvu kuhakikisha ngome ya wagosi inaendelea kuwa iara.
Kikosi cha leo kilichoanza dhidi ya Simba ni: Fikirini Suleiman, Hamadi Juma, Abdi Banda, Yusuf Chuma, Mbwana Kibacha, Razak Khalfan, Ally Nassor ‘Ufudu’, Behewa Sembwana, Suleiman Kassim ‘Selembe’, Kenneth Masumbuko, Danny Lyanga.
Wachezaji wa akiba ni: Mansour Alawi, Ayoub Masoud, Marcus Ndeheli, Ayoub Semtawa, Mohammed Miraji, Crispian Odula, na Mohammed Kipanga.
Baadae Kocha aliwatoa Ally Nassor, Hamadi Juma na Suleiman Kassim, wakaingia Mohammed Miraji, Ayoub Masoud na Marcus Ndeheli.
Kwa matokeo hayo Coastal Union imevuna point tatu na kufikisha jumla ya point 30, na kupaa hadi nafasi ya saba ikisubiri kucheza na Mtibwa Sugar katika uwanja wa Manungu mjini Morogoro.
COASTAL UNION
23 MARCH, 2014
DAR ES SALAAM, TANZANIA