MENEJA WA TIMU YA COASTAL UNION,AKIDA MACHAI KUSHOTO AKIMKABIDHI JEZI WINGA WA KULIA MPYA WA COASTAL UNION,IBRAHIM TWAHA "MESSI"MARA BAADA YA KUSAINI MKATABA WA MIAKA MIWILI WA KUITUMIKIA TIMU HIYO |
Wednesday, July 29, 2015
MESSI WA SIMBA ATUA COASTAL UNION,ASEMA AMEAMUA KURUDI NYUMBANI.
Monday, July 27, 2015
NAMNA WANACHAMA WA TAWI LA MNARANI JIJINI TANGA WALIVYOWAPONGEZA WAJUMBE WA KAMATI YA UTENDAJI WAPYA WA COASTAL UNION
MWENYEKITI WA TAWI LA MNARANI JIJINI TANGA,SHABENGA AKIZUNGUMZA KABLA YA KUMKARIBISHA KATIBU WA COASTAL UNION,KASSIM EL SIAGI
KATIBU MSAIDIZI WA COASTAL UNION,SALIM BAWAZIRI AMBAYE PIA NI MWENYEKITI WA KAMATI YA USAJILI NA MWENYEKITI WA BARAZA LA WAZEE LA KLABU HIYO AKIZUNGUMZA KATIKA HALFA HIYO |
MENEJA WA KLABU YA COASTAL UNION,AKIDA MACHAI AKIZUNGUMZA WAKATI WA HALFA HIYO YA KUWAPONGEZA WAJUMBE WALIOCHAGULIWA KUTOKA TAWI LA MNARANI JUZI |
KATIBU WA TAWI LA MNARANI YENYE MASKANI YAKE MABANDA YA PAPA AKIZUNGUMZA KABLA YA KUANZA SHEREHE HIZO ZA KUWAPONGEZA WAJUMBE WA KAMATI YA UTENDAJI WALIOCHAGULIWA KWENYE UCHAGUZI MKUU ULIOPITA. |
MWENYEKITI WA COASTAL UNION AKUTANA NA KAMATI MBALIMBALI
MWENYEKITI WA COASTAL UNION,DR.AHMED TWAHA AKIZUNGUMZA NA KAMATI ZA KLABU HIYO MWISHONI MWA WIKI KULIA NI KATIBU MKUU KASSIM EL SIAGI NA KUSHOTO NI MAKAMU MWENYEKITI SALIM AMII |
MWENYEKITI WA COASTAL UNION DR.AHMED TWAHA AKIONGEZA MPANGO MKAKATI WA KLABU HIYO UTAKAOTUMIKA KATIKA KIPINDI CHA UONGOZI WAKE |
MENEJA WA KLABU YA COASTAL UNION,AKIDA MACHAI AKISISITIZA JAMBO KWENYE MKUTANO HUO AMBAO ULIMUISHA KAMATI ZOTE ZILIZOUNDWA NA MWENYEKITI HUYO |
WAJUMBE WA KAMATI MBALIMBALI WAKIMSIKILIZA MWENYEKITI WA COASTAL UNION,DR.AHMED TWAHA WAKATI WA KIKAO HICHO |
\PICHA YA PAMOJA MWENYEKITI WA COASTAL UNION NA WAJUMBE WA KAMATI MBALIMBALI |
MWENYEKITI WA KLABU YA COASTAL UNION,DR.AHMED TWAHA AKIWA KWENYE PICHA YA PAMOJA NA KAMATI YA MIPANGO NA FEDHA.
UONGOZI wa
Klabu ya Coastal Union umeitaka kamati ya ulinzi na usalama kuhakikisha
inatimiza wajibu wake ipasavyo ikiwemo kuhakikisha vitendo vitakavyoweza
kuigharimu timu hiyo wakati wa michuano ya Ligi kuu soka Tanzania bara
vinazibitiwa.
Akizungumza
mara baada ya kumalizika kwa kikao baina ya Kamati ndogo ndogo zilizoundwa,Mwenyekiti
wa Klabu ya Coastal Union,Dr.Ahmed Twaha alisema kuwa kumekuwa na vitendo vingi
ambavyo vinajitokeza kwenye michuano ya Ligi kuu Tanzania bara na kuigharimu
timu yetu na kulazimika kulipa faini ambayo ingeweza kufanya mambo mengine ya
maendeleo.
Alisema
kutokana na kuwepo kwa tatizo hilo ndio sababu pekee iliyopelekea kuundwa
kamati hiyo ili kuweza kukabiliana na vitendo vinayoweza kuisababisha hasara
ndani ya klabu hiyo kwani vinakwamisha juhudi za kupiga maendeleo.
“Ukiangalia msimu uliopita tulipata hasara
ya shilingi milioni 3 kwa makosa ya uwanjani na hii inasababishwa na mashabiki
kitendo ambacho kinaharibu sura ya mkoa hivyo lazima kamati hii italisimamia
suala hilo “Alisema Mwenyekiti huyo.
Aidha
Mwenyekiti huyo aliitwisha mzigo mengine kamati ya Nidhamu na Maadili
kuhakikisha watu wanaotukana kwenye mitandaa ya kijamii ikiwemo Facebook,
Twiter na mengineyo watachukuliwa hatua kali za kisheria ili kukomesha vitendo
hivyo.
Hata hivyo
alisema kuwa kamati hiyo itakuwa na jukumu kubwa la kuhakikisha ulinzi na usalama
unaimarishwa wakati wa timu hiyo itakapokuwa ikicheza mechi zake kwenye
michuano ya Ligi kuu soka Tanzania bara.
“Lakini pia zamani wapo watu walikuwa
wakitengeneza vitabu vya tiketi na kufanya mapato kuwa madogo licha ya uwepo wa
watu wengi hivyo huu ndio mwisho wao kamati hii pia itasimamia suala hilo kwani
hali hii iliifanya klabu kukosa mapato “Alisema Mwenyekiti huyo.
Mwenyekiti
huyo alisema kuwa wameweka mipango mizuri ya kuhakikisha timu hiyo inafungua
matawi kwenye mikoa yote timu hiyo itakapokuwa ikienda kushiriki michuano ya
Ligi kuu hapa nchini.
Thursday, July 23, 2015
HIVI NDIVYO MWENYEKITI MPYA WA COASTAL UNION,DR.AHMED TWAHA ALIVYOFURAHIA USHINDI WAKE NA WANACHAMA WA COASTAL UNION
MWENYEKITI WA KLABU YA COASTAL UNION,DR.AHMED TWAHA AKIWA NA WANACHAMA WA KLABU HIYO MARA BAADA YA KUMALIZIKA UCHAGUZI MKUU AMBAPO ULIMCHAGUA KUONGOZA KLABU HIYO |
MWENYEKITI MPYA WA COASTAL UNION DR.AHMED TWAHA KUSHOTO AKISHIKANA MKONO NA MAKAMU MWENYEKITI WAKE,SALIM AMIRI KULIA NI MJUMBE WA KAMATI YA COASTAL UNION |
MWENYEKITI MPYA WA COASTAL UNION DR.AHMED TWAHA AKINYANYULIWA JUU NA WANACHAMA WA TIMU HIYO MARA BAADA YA KUIBA KIDEDEA KWENYE UCHAGUZI HUO |
MWENYEKITI MPYA WA COASTAL UNION DR.AHMED TWAHA AKIFUATILIA MATUKIO YA MKUTANO HUO |
COASTAL YAMNASA KIPA KUTOKA VILLA SC YA UGANDA”
UONGOZI
wa Klabu ya Coastal Union umeingia mkataba wa miaka miwili na aliyekuwa mlinda
mlango wa timu ya Villa SC ya nchini Uganda, Jackson Sabweto ili kuitumikia timu
hiyo katika msimu mpya wa Ligi kuu soka Tanzania bara utakaoanza mwezi Septemba
mwaka huu.
Utiliaji
saini huo ulifanyika juzi makao makuu ya klabu hiyo yaliyopo barabara kumi na
moja jijini Tanga na kushuhudiwa na viongozi mbalimbali akiwemo Katibu Mkuu,
Kassim El Siagi.
Akizungumza , Katibu wa Coastal Union, Kassim El Siagi alisema kuwa nia ya kumsajili
kipa huyo ni kuimarisha nafasi hiyo kwenye timu hiyo kabla ya kuanza michuano
ya Ligi kuu soka Tanzania ili waweze kushiriki kwa mafanikio makubwa na tija.
El
Siagi alisema kuwa usajili ambao umefanywa na klabu umepanga kuhakikisha msimu
ujao kombe la Ligi kuu linatua kwenye viunga vya mitaa ya barabara ya kumi na
moja jijini Tanga ili kurudisha historia yao ya muda mrefu tokea walipotwaa
kombe hilo mwaka 1988.
“Niseme tu usajili tulioufanya ni nzuri na
utakuwa chachu ya kurejesha makali yetu ya mwaka 1988 wakati tulipochukua
Ubingwa wa Ligi kuu hapa nchini “Alisema El Siagi.
Hata
hivyo aliwataka wachezaji ambao hawajawasili mkoani hapa kuungana na wenzao
kwenye mazoezi yanayoendelea kwenye viwanja vya shule ya sekondari Popatlaly
chini ya Kocha Mkuu, Jackson Mayanja kuhakikisha wanawasili haraka
iwezekanavyo.
NAMNA COASTAL UNION ILIVYOINGIA MKATABA NA KOCHA MKUU MAYANJA NA KOCHA WA MAKIPA FREDY LUMU
KOCHA WA MAKIPA WA COASTAL UNION,FREDY LUMU AKISAINI MKATABA WA KUWAFUNDISHA MAKIPA WA TIMU HIYO HIVI KARIBUNI KULIA NI KATIBU MKUU WA COASTAL UNION,KASSIM EL SIAGI |
KATIBU MKUU WA COASTAL UNION,KASSIM EL SIAGI AKIMUONYESHA SEHEMU YA KUSAINI KOCHA MPYA WA COASTAL UNION,JACKSON MAYANJA MARA BAADA YA KUTUA MKOANI TANGA TAYARI KUKINOA KIKOSI HICHO. |
KUSHOTO NI KOCHA MKUU MPYA WA COASTAL UNION,JACKSON MAYANJA AKIMKABIDHI MKATABA WAKE KATIBU MKUU WA COASTAL UNION MARA BAADA YA KUUSAINI TAYARI KUITUMIA TIMU HIYO |
Subscribe to:
Posts (Atom)