UONGOZI
wa Klabu ya Coastal Union umeingia mkataba wa miaka miwili na aliyekuwa mlinda
mlango wa timu ya Villa SC ya nchini Uganda, Jackson Sabweto ili kuitumikia timu
hiyo katika msimu mpya wa Ligi kuu soka Tanzania bara utakaoanza mwezi Septemba
mwaka huu.
Utiliaji
saini huo ulifanyika juzi makao makuu ya klabu hiyo yaliyopo barabara kumi na
moja jijini Tanga na kushuhudiwa na viongozi mbalimbali akiwemo Katibu Mkuu,
Kassim El Siagi.
Akizungumza , Katibu wa Coastal Union, Kassim El Siagi alisema kuwa nia ya kumsajili
kipa huyo ni kuimarisha nafasi hiyo kwenye timu hiyo kabla ya kuanza michuano
ya Ligi kuu soka Tanzania ili waweze kushiriki kwa mafanikio makubwa na tija.
El
Siagi alisema kuwa usajili ambao umefanywa na klabu umepanga kuhakikisha msimu
ujao kombe la Ligi kuu linatua kwenye viunga vya mitaa ya barabara ya kumi na
moja jijini Tanga ili kurudisha historia yao ya muda mrefu tokea walipotwaa
kombe hilo mwaka 1988.
“Niseme tu usajili tulioufanya ni nzuri na
utakuwa chachu ya kurejesha makali yetu ya mwaka 1988 wakati tulipochukua
Ubingwa wa Ligi kuu hapa nchini “Alisema El Siagi.
Hata
hivyo aliwataka wachezaji ambao hawajawasili mkoani hapa kuungana na wenzao
kwenye mazoezi yanayoendelea kwenye viwanja vya shule ya sekondari Popatlaly
chini ya Kocha Mkuu, Jackson Mayanja kuhakikisha wanawasili haraka
iwezekanavyo.
No comments:
Post a Comment