MWENYEKITI WA COASTAL UNION,DR.AHMED TWAHA AKIZUNGUMZA NA KAMATI ZA KLABU HIYO MWISHONI MWA WIKI KULIA NI KATIBU MKUU KASSIM EL SIAGI NA KUSHOTO NI MAKAMU MWENYEKITI SALIM AMII |
MWENYEKITI WA COASTAL UNION DR.AHMED TWAHA AKIONGEZA MPANGO MKAKATI WA KLABU HIYO UTAKAOTUMIKA KATIKA KIPINDI CHA UONGOZI WAKE |
MENEJA WA KLABU YA COASTAL UNION,AKIDA MACHAI AKISISITIZA JAMBO KWENYE MKUTANO HUO AMBAO ULIMUISHA KAMATI ZOTE ZILIZOUNDWA NA MWENYEKITI HUYO |
WAJUMBE WA KAMATI MBALIMBALI WAKIMSIKILIZA MWENYEKITI WA COASTAL UNION,DR.AHMED TWAHA WAKATI WA KIKAO HICHO |
\PICHA YA PAMOJA MWENYEKITI WA COASTAL UNION NA WAJUMBE WA KAMATI MBALIMBALI |
MWENYEKITI WA KLABU YA COASTAL UNION,DR.AHMED TWAHA AKIWA KWENYE PICHA YA PAMOJA NA KAMATI YA MIPANGO NA FEDHA.
UONGOZI wa
Klabu ya Coastal Union umeitaka kamati ya ulinzi na usalama kuhakikisha
inatimiza wajibu wake ipasavyo ikiwemo kuhakikisha vitendo vitakavyoweza
kuigharimu timu hiyo wakati wa michuano ya Ligi kuu soka Tanzania bara
vinazibitiwa.
Akizungumza
mara baada ya kumalizika kwa kikao baina ya Kamati ndogo ndogo zilizoundwa,Mwenyekiti
wa Klabu ya Coastal Union,Dr.Ahmed Twaha alisema kuwa kumekuwa na vitendo vingi
ambavyo vinajitokeza kwenye michuano ya Ligi kuu Tanzania bara na kuigharimu
timu yetu na kulazimika kulipa faini ambayo ingeweza kufanya mambo mengine ya
maendeleo.
Alisema
kutokana na kuwepo kwa tatizo hilo ndio sababu pekee iliyopelekea kuundwa
kamati hiyo ili kuweza kukabiliana na vitendo vinayoweza kuisababisha hasara
ndani ya klabu hiyo kwani vinakwamisha juhudi za kupiga maendeleo.
“Ukiangalia msimu uliopita tulipata hasara
ya shilingi milioni 3 kwa makosa ya uwanjani na hii inasababishwa na mashabiki
kitendo ambacho kinaharibu sura ya mkoa hivyo lazima kamati hii italisimamia
suala hilo “Alisema Mwenyekiti huyo.
Aidha
Mwenyekiti huyo aliitwisha mzigo mengine kamati ya Nidhamu na Maadili
kuhakikisha watu wanaotukana kwenye mitandaa ya kijamii ikiwemo Facebook,
Twiter na mengineyo watachukuliwa hatua kali za kisheria ili kukomesha vitendo
hivyo.
Hata hivyo
alisema kuwa kamati hiyo itakuwa na jukumu kubwa la kuhakikisha ulinzi na usalama
unaimarishwa wakati wa timu hiyo itakapokuwa ikicheza mechi zake kwenye
michuano ya Ligi kuu soka Tanzania bara.
“Lakini pia zamani wapo watu walikuwa
wakitengeneza vitabu vya tiketi na kufanya mapato kuwa madogo licha ya uwepo wa
watu wengi hivyo huu ndio mwisho wao kamati hii pia itasimamia suala hilo kwani
hali hii iliifanya klabu kukosa mapato “Alisema Mwenyekiti huyo.
Mwenyekiti
huyo alisema kuwa wameweka mipango mizuri ya kuhakikisha timu hiyo inafungua
matawi kwenye mikoa yote timu hiyo itakapokuwa ikienda kushiriki michuano ya
Ligi kuu hapa nchini.
No comments:
Post a Comment