INAWEZEKANA
bahati haijakuwa yetu ama wachezaji hawajakuwa tayari kuipa furaha Coastal
Union katika msimu huu.
Suluhu tasa ya
leo dhidi ya Mgambo JKT, inazidi kudidimiza ndoto za Wagosi wa kaya kumaliza
mzunguko wa kwanza wa ligi wakiwa katika nafasi nzuri, ili katika mzunguko wa
pili wawe wamejipanga zaidi.
Dakika ya
pili tu ya mchezo wa leo Masumbuko Keneth wa Wagosi alipokea pasi akiwa upande
wa kulia, akawazidi ujanja mabeki wa Mgambo akaingia nao kwenye box na kukunjuka shuti kali lakini likaenda
fyongo.
Kama hiyo
haitoshi Masumbuko huyohuyo katika dakika ya 22 kipindi cha kwanza akiwa winga
ya kushoto alipokea pasi kutoka kwa Uhuru Suleiman ambaye alipiga mpira mrefu
ukatua miguuni mwa Masumbuko, akawekwa mtu kati na mabeki wawili wa Mgambo
lakini akawazidi mbio, kwa kujiamini akapiga shuti kwa mguu wa kushoto lakini
likatoka nje mita chache na kugonga nyavu ndogo.
Mgambo walionekana
wamechanganyoikiwa kutokana na kasi ya Wagosi wakaanza kupoteza mwelekeo. Mnamo
dakika ya 24, Danny Lyanga alipokea pasi akiwa nje kidogo ya box, akapiga
chenga na kuingia nao ndani kwa kasi kubwa mpaka katika box dogo lakini
akapoteza mwelekeo na shuti lake halikuleta madhara.
Mambo yalizidi
kuwa mabaya kwa upande wa Mgambo, mashabiki wa Coastal Union wakaanza kushangilia
kwa nguvu wakiamini mchezo wa leo watashinda mabao mengi kutokana na mchezo
kuwa wa kasi sana.
Danny huyohuyo
ilipofika dakika ya 28 almanusura aipatie bao Coastal Union baada ya kuminyana
na mabeki wa Mgambo ambao tayari walishakubali kuwa wamezidiwa nguvu. Akaingia mpaka
kwenye box dogo lakini kadhalika shuti lake halikuzaa matunda. Akaanza kuzomewa
na mashabiki wake.
Mpaka timu
zinakwenda mapumziko hakuna aliyeona lango la mwenzake. Aidha Mgambo walitoka
kichwa chini wakiamini mchezo wa leo hawana bahati nao.
Kipindi cha
pili mwalimu Joseph Lazaro, alifanya mabadiliko akawatoa Suleiman Kassim ‘Selembe’
na Danny Lyanga wakaingia Haruna Moshi na Yayo Kato.
Ilipotimu dakika
ya75 Mgambo walipata bao, lakini mwamuzi wa leo Geofrey Tumaini kutoka Dar Es
Salaam akasema wameotea.
Baadaye hali
ilizidi kuwa mbaya kwa upande wa Coastal Union ambapo Mgambo walishambulia kwa
kasi wakitaka kupata bao la kuongoza lakini mabeki wa Coastal Union walikuwa
makini.
Mpaka kipyenga
cha mwisho wachezaji wa Coastal Union walipewa kadi za njano tatu ambapo Hamad
Juma, Jerry Santo na Juma Nyosso walionyeshwa kadi moja moja kwa kucheza
madhambi.
Kutokana na
matokeo hayo ya suluhu ya bila kufungana Coastal Union imeambulia point 16
tukiendelea kushikilia nafasi ya nane, mchezo wa mwisho dhidi ya JKT Ruvu
katika uwanja wa Chamazi siku ya jumatano wiki ijayo itamaliza utata juu ya
nafasi watakayomaliza wagosi katika mzunguko wa pili.
Kikosi cha
leo: Shaaban, Kado, Hamadi Juma, Othamna Tamim, Mbwana Kibacha, Juma Nyosso,
Jerry Santo, Uhuru Suleiman, Crispian Odula, Masumbuko Keneth, Danniel Lyanga, Suleiman
Selembe.
Sub: Said
Lubawa, Haruna Moshi, Abdi Banda, Mohammed Sudi, Razakh Khalfan Marcus Ndehele,
na Yayo Kato.
COASTAL
UNION
2 SEPTEMBA,
2013
TANGA,
TANZANIA
No comments:
Post a Comment