MZUNGUKO wa kwanza wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara
umekamilika leo baada ya Coastal Union kukubali kipigo cha bao 1-0 dhidi ya
maafande wa JKT Ruvu, kwenye uwanja wa Chamazi jijini Dar es Salaam.
Kipindi cha kwanza kilianza kwa Wagosi kusuasua na kuwapa
nafasi Ruvu kuutawala mchezo ambapo ndani ya dakika ya kwanz awalikosa bao na
kupata kona.
Hali iliendelea hivyo kwa wachezaji wa Wagosi kupoteza
mwelekeo ambapo katika dakika ya tisa Ruvu walikosa bao la wazi baada ya
beki Wagosi Juma Nyoso alichelewa kufika
baada ya Ruvu kupiga krosi na mchezaji wao kuingia nao lakini golikipa wa
Wagosi Shaaban Kado alikuwa makini langoni.
Ilipofika dakika ya 34 Ruvu waligongeana pasi ndani ya box la
Wagosi, ambapo kutokana na walinzi kukosa umakini Bakari Kondo wa Ruvu
aliipatia bao la kuongoza timu yake.
baada ya hali kuwa hivyo kocha Joseph Lazaro wa Wagosi
alifanya mabadiliko na kuwatoa Hamad aliyeumia na kumuingiza Marcus Ndeheli.
Halafu akamtoa Othman Tamim na kumuingiza Abdi Banda.
Aidha timu zilienda mapumziko Ruvu JKT wakiwa mbele kwa bao
moja.
Kipindi cha pili, mchezo ulianza kwa Coastal Union kutawala uwanja, na kuonyesha nguvu ya kutaka
kukomboa bao lililopatikana kipindi cha kwanza.
Baadaye alitolewa Suleiman Kassim ‘Selembe’ na kuingia
Daniel Lyanga. Lakini hakuna kilichobadilika mpaka daika tisini.
Mwamuzi wa leo Hasheem Abdallah kutoka Dar es Salaam,
alimaliza mchezo akiwa anazomewa na mashabiki wachache wa Coastal Union
waliojitokeza leo wakimshutumu kuchezesha hovyo.
Kwa hali hiyo Coastal Union itaendelea kushikilia nafasi ya
saba ikiwa na point 16.
1.Kado
2.Hamad (Out)
3.Othman Tamim (Out)
4.Kibacha
5.Nyoso
6.Razakh
7.Uhuru
8.Odula
9. Boban
10.Masumbuko
11.Selembe. (Out)
Sub:
1.Lubawa
2.Banda (In)
3.Marcus (In)
4.Sudi,
5.Yaya
6.Danny lyanga (In)
7.Philip
2.Hamad (Out)
3.Othman Tamim (Out)
4.Kibacha
5.Nyoso
6.Razakh
7.Uhuru
8.Odula
9. Boban
10.Masumbuko
11.Selembe. (Out)
Sub:
1.Lubawa
2.Banda (In)
3.Marcus (In)
4.Sudi,
5.Yaya
6.Danny lyanga (In)
7.Philip
COASTAL UNION
SEPTEMBA 6, 2013
DAR ES SALAAM, TANZANIA
No comments:
Post a Comment