Krossi ya Masumbuka ikipenya kwenye kifua cha mchezaji wa Ashanti...
Mganda, Yayo Kato akiwa ndani ya box la Ashanti lakini uwepo wake haukuleta madhara yoyote.
Uhuru Suleiman akimimina majaro ndani ya box la Ashanti lakini hakuna mchezaji wa Coastal Union kuweza kupokea majaro hiyo.
Nahodha Jerry Santo wa Wagosi wa Kaya akikokota mpira huku mchezaji wa Ashanti akimnyemelea.
Atupele Green akigombania mpira na mchezaji wa Ashanti United katika kipindi ha pili.
Shaaban Kado wa Coastal Union akiokoa moja ya hatari zilizosababishwa na mchezaji wa zamani wa Wagosi, Joseph Mahundi ambaye amekuwa msaada mkubwa kwa Ashanti United.
Kocha wa Coastal Union, Hemed Moroco akibishana na mwamuzi wa jana Anthony Kayombo, baada ya bao la pili la Ashanti kuingia kwa utata. Baadaye Moroco alitolewa nje ya uwanja.
Mashabiki wa Wagosi wakiwa kimya baada ya bao la pili kuingia kwa utata.
Wachezaji wa Ashanti United, wakiwa na furaha baada ya mchezo wa jana kuisha kwa ushindi wa 2-1. Huo ndiwo ushindi wa kwanza wa Ashanti tangu ligi ianze. Na pia ndiwo mchezo wa kwanz akwa Coastal Union kuupoteza.
BAO la pili lililofungwa na Tumba Sued, wa
Ashanti United lilitosha kuwanyong’onyeza wachezaji wa Coastal Union na kukiri
kuwa mchezo umeshaisha kwa mabao 2-1.
Ilikuwa ni dakika ya 85 baada ya mwamuzi
Anthony Kayombo, kutoka Rukwa kupuliza filimbi akimaanisha mlinda mlango wa
Wagosi wa Kaya amechezewa madhambi, lakini wakati walinzi wa Wagosi wakisubiri
Kado apige mpira mara akatokea Tumba wa Ashanti na kuutumbukiza mpira wavuni,
mwamuzi akasema ni bao.
Kulitokea rabsha kwa dakika kadhaa ambapo
wachezaji waliokuwa eneo la tukio walibishana na mwamuzi, kadhalika kocha wa
Wagosi alianza kumshutumu mwamuzi hatimaye aliamuliwa kutoka uwanjani.
Aidha kipindi cha kwanza Ashanti walicheza
soka la nguvu lakini kwa bahati mbaya ilipofika dakika ya pili mmoja wa wachezaji
wao aliunawa mpira katika eneo la hatari. Mwamuzi akasema ni penati na nahodha
Jerry Santo akaitendea haki likaandikwa bao la kwanza.
Lakini kabla ya kipindi cha kwanza kuisha
mchezaji wa Ashanti aliangushwa katika eneo la hatari na mwamuzi akasema ipigwe
penati dakika ya 21, beki wa Ashanti Tumba Sued akasawazisha hivyo mpaka timu
zinakwenda mapumziko ubao ulisomeka 1-1.
Kipindi cha pili Ashanti walishambulia kwa
kasi kiasi wakawachanganya Coastal Union, mshambuliaji wa pembeni Joseph
Mahundi alionekana mwiba kwa mabeki wa Coastal Union, hali iliendelea hivyo
mpaka dakika ya thamanini lilipotokea zahma la bao la utata.
Tathmini ya mpira wa jana ni wazi wachezaji
wa Wagosi wa kaya walizidiwa uwezo na timu inayoshika mkia Ashanti United.
Katika hatua nyingine kabla ya mchezo
kuanza kulitokea utata wa jezi baada ya Ashanti United kutokeza uwanjani wakiwa
na jezi nyeupe huku Coastal Union nao wakiwa na jezi nyeupe, kutokana na sheria za mchezo mwenyeji ndiye
anayeamua jezi ya kuvaa hivyo mgeni alitakiwa kubadili.
Kwa bahati mbaya jezi nyekundu za Wagosi wa
Kaya hazikuwa uwanjani, ukatolewa ushauri kuwa wavae jezi nyeupe halafu
waongeze jezi za mazoezi ambazo ni nyekundu lakini zimekatwa mikono.
Kwa matokeo hayo Coastal Union itaendelea
kubaki na point 11 na kuna uwezekano ikashuka zaidi kutoka nafasi ya saba
kutokana na matokeo ya jana na leo katika viwanja vya michezo nchini. Ambapo
Simba wameendelea kujikita kileleni kwa kuvuna point 18 katika mechi ya jana na
Yanga kukwea mpaka nafasi ya pili wakiwa na point 15.
COASTAL UNION
OKTOBA 12, 2013
DAR ES SALAAM, TANZANIA
No comments:
Post a Comment