Saturday, February 22, 2014

Coastal Union 2-0 Mbeya City

 Mashabiki wa Coastal Union wakishangilia baada ya kuingia bao la pili dakika chache kabla ya mpira kuisha.

 Kiungo mshambuliaji wa Coastal Union, Mkongwe Haruna Moshi Boba akitafuta mbinu za kumtoka nahodha wa Mbeya City katika mchezo wa leo.

 Ally Nassor 'Ufudu' akitumia mbinu za kumkinga golikipa wa Mbeya City katika moja ya kona zilizopigwa kwenye mchezo wa leo ulioisha kwa mshindi mnono wa bao 2-0.

Danny Lyanga akikokota mpira huku mchezai wa Mbeya City akitafuta mbinu za kumdhibiti.

 Yusuf Chipo akiwahimiza wachezaji wake wapande juu wasikabe.


Haruna Moshi 'Boban', akifanya vitu vyake uwanjani leo kuwaonyesha vijana kwamba bado yumo.

 Winga wa Coastal Union Danny Lyanga akiambaa na mpira huku akitafuta mbinu za kupiga krosi.

                                                                Danny Lyanga akiminyana.
 Mlinzi wa pembeni Coastal Union, Abdi Banda akimiliki mpira bila ya wasiwasi wowote.

Mohammed Miraji 'aliebebwa' akishangilia bao la kwanza mnamo dakika ya 79 kipindi cha pili.

mlinda mlango wa Costal Union Shaaban Kado, alishindwa kujizuia nae alikuja kushangilia bao la kwanza.


 Mashabiki wa Mbeya City wakiwa hawaamini wanachokiona namna vijana wa Chipo walivyofanya mambo.


 Mashabiki wa Caostal Union katika furaha kwenye uwanja wa nyumbani Mkwakwani.

                                                                Shaaban Kado.

 Kutoka kushoto Juma Nyoso, Mohammed Miraji na Kenneth masumbuko wakishangilia bao la pili lililofungwa na Moammed Miraji.

Mohammed Miraji akilia kwa uchungu baada ya kuweka historia ya kuwapiga mabao mawili peke yake Mbeya City.

 Mbeya City kawaida yao hufanya mazoezi baada ya mechi, lakini Mkwakwani walifanya kidogo na kuacha.


                                    Mashabiki wa Coastal Union wakishangilia baada ya mechi.

HATIMAE historia imeandikwa kwatika jiji la Tanga baada ya Coastal Union ‘Wagosi wa kaya’ kuwa timu ya pili kuifunga Mbeya City katika Ligi Kuu, lakini vilevile ni ya kwanza kuifunga mabao mengi.
Bao la kwanza liliingizwa kimiani mnamo dakika ya 79 baada ya Mohammed Miraji, kuunganisha pasi ya Danny Lyanga ambae alipokea mpira uliorushwa na Abdi Banda.
Mohammed, aliruka juu na mchezaji wa Mbeya City akapiga kichwa kilichopaa na kurudi langoni kama masihara ukisindikizwa na beki wa Mbeya City. Baada ya bao hilo Coastal Union waliendelea kulisakama lango la Mbeya City kwa takriban dakika tano.
Aidha bao la pili lilikuwa juhudi binafsi za mchezaji chipukizi Mohammed Miraji ‘Muddy Magoli’ ambapo alipokea pasi nyuma kidogo ya 18, akamzidi nguvu kiungo wa Mbeya City akapiga chenga mbili na kuinua macho kumtazama Burhani, golikipa wa Mbeya City. Akakunjuka shuti kali kwa mguu wa kulia lililomzidi nguvu Burhani na kuandika bao la pili dakika mbili kabla ya mwamuzi wa leo Zacharia Jacob, kutoka Pwani kumaliza mchezo.
Hata hivyo Wagosi wa Kaya walinza mpira wa leo kwa kusuasua ambapo kipindi cha kwanza walitengeneza nafasi nyingi lakini hawakuambulia kitu. Mpaka kipindi cha kwanza kinakamilika Wagosi walicheza chini ya kiwango hali iliyowanyima raha mashabiki wa Wagosi huku ikiwaamsha mashabiki wachache wa Mbeya City waliosafiri na timu kutoka jijini Mbeya.
Kocha wa Wagosi Yusuf Chipo, alifanya mabadiliko kwa kuwatoa Ally Nassor ‘Ufudu’ akaingia Kenneth masumbuko, baadae akamtoa Ayoub Semstawa akaingia Yayo kato halafu akakamilisha mabadiliko ya leo kwa kumtoa Crispian Odula na kumuingiza Mohammed Miraji ambae alikuwa mfalme wa echi ya leo.
Mabadiliko hayo yalileta uhai kwa timu hasa winga Masumbuko alipoingiza mipira mingi lakini Yayo kato na Haruna Moshi ‘Boban’ walishindwa kuzitendea haki krosi za winga huyo msumbufu.
Katika hatua nyingine Mbeya City, walifanya mashambulizi mengi katika lango la Wagosi lakini uimara wa mabeki Abdi banda, Nyoso, Kibacha na Chuma ulimsaidia golikipa Shaaban Kado kupata muda mzuri wa kudaka kwa kujiamini.
Kutokana na matokeo hayo Coastal Union wamepaa mpaka nafasi ya sita wakitoka nafasi ya saba huku wakijizolea point 25.
Kikosi cha leo: Shaaban Kado, Mbwana Kibacha, Abdi Banda, Yusuf Chuma, Juma Nyoso, Jery Santo, Dany Lyanga, Ally Nassor ‘Ufudu’, Ayoub Semtawa, Haruna Moshi ‘Boban’ na Crispian Odula.
Wachezaji wa akiba walikuwa ni: Mansour Alawi, Suleiman Kassim ‘Selembe’, Kenneth Masumbuko, Mohammed Miraji, Yayo kato, Behewa Sembwana na Ayoub Masoud.
COASTAL UNION
22 FEBRUARI, 2014
TANGA, TANZANIA

No comments:

Post a Comment