Ikiwa hakutakuwa na mabadiliko yoyote kutoka Shirikisho la
soka nchini (TFF), mechi saba za Coastal Union zilizobaki msimu huu zitakuwa ni
dhidi ya Ashanti United Machi 8, 2014 uwanja wa Mkwakwani Ifikapo Machi 12
katika uwanja wa Taifa jiji Dar es Salaam Wagosi wa Kaya watacheza na Simba, wakati Machi 15 katika
uwanja wa Azam Complex Chamazi, Wagosi watakipiga na Azam FC katika mechi ya 22
ligi kuu ya Vodacom.
Aidha ifikapo Machi 23 mwaka huu Wagosi wa Kaya watasafiri
mpaka Manungu kumenyana na Mtibwa Sugar, na Machi 30 Coastal Union itafunga
mwezi dhidi ya Mgambo JKT katika uwanja wa Mkwakwani Tanga huku Wagosi wakiwa
wageni wa Mgambo.
Ifikapo Aprili 14, 2014 Coastal Union itakutana na JKT Ruvu katika
uwanja wa Mkwakwani huku ikikamilisha ratiba ya Ligi kwa mechi dhidi ya Kagera
Sugar katika uwanja wa Mkwakwani tarehe 27 April, mwaka huu.
Mpaka sasa Coastal Union imecheza mechi 19 tangu ligi ianze,
imeambulia point 25 katika nafasi ya sita nyuma ya Yanga point 38, Azam (36),
Mbeya City (35), Simba (32) na Kagera Sugar (26).
MSEMAJI- COATAL UNION
TANGA, TANZANIA
FEB 23, 2014
No comments:
Post a Comment