Baada ya ushindi wa leo katika mechi kati ya Rhino Rangers
na Coastal Union kwenye uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora, ambapo Jerry
Santo aliipatia Coastal Union bao la mapema dakika ya pili, sasa tumepanda
mpaka nafasi ya tano.
Kwa mujibu wa msimamo wa ligi, Coastal Union kabla ya
ushindi wa leo walikuwa na point 19 katika nafasi ya saba. Baada ya Mtibwa
Sugar kupoteza mchezo wake dhidi ya Mbeya City, wameendelea kubaki na point 22,
ambazo Coastal pia wamezifikia hivyo kuwafanya kushuka nafasi moja chini
kutokana na tofauti ya mabao ya kushinda na kushindwa.
Hivyo habari njema kwa mashabiki wa Coastal Union, ni kuwa
kwa sasa tunaendeleza wimbi la ushindi ili kujeweka katika nafasi nzuri hasa
ikizingatiwa kocha ameamua kufanya mabadiliko ya kikosi chake ili kupata
ushindi kila mechi inayokuja.
Anaeshika nafasi ya kwanza ana point 36, na sisi kutokana na
mechi tisa tulizobakisha ikiwa tutashinda zote tutakuwa na jumla ya point 49.
Kwa maana hiyo uwezekano wa kumaliza nafasi tatu za juu upo ikiwa tutafanya
vizuri katika mechi tisa tulizobakisha ambazo ni dhidi ya:
Simba, Kagera Sugar, Azam FC, Mgambo JKT, JKT Ruvu, Ruvu
Shooting, Ashanti, Mtibwa Sugar na Mbeya City.
Ikumbukwe kuwa mechi tatu za awali kabla ya leo kukutana na
Rhino Rangers tulivaana na JKT Oljoro (1-1), Yanga (0-0) na Tanzania Prisons
(0-0).
Kikosi leo kilichokutana na Rhino Rangers kilikuwa hivi: Shaaban
Kado, Mbwana Kibacha, Othman Tamim, Yusuf Chuma, Juma Nyoso, Jery Santo,
Suleiman Selembe, Mohammed Sudi, Crispian Odula, Haruna Boban na Danny Lyanga.
Na huu ndio msimamo wa ligi Kuu Tanzania Bara baada ya mechi
za leo jioni.
Pos.
|
Logo
|
Club
|
P
|
W
|
D
|
L
|
GF
|
GA
|
GD
|
Pts
|
1
|
|
16
|
10
|
6
|
0
|
29
|
10
|
19
|
36
|
|
2
|
|
16
|
10
|
5
|
1
|
34
|
12
|
22
|
35
|
|
3
|
|
17
|
9
|
7
|
1
|
23
|
13
|
10
|
34
|
|
4
|
|
17
|
8
|
7
|
2
|
32
|
15
|
17
|
31
|
|
5
|
|
17
|
4
|
10
|
3
|
11
|
7
|
4
|
22
|
|
6
|
|
17
|
5
|
7
|
5
|
23
|
21
|
2
|
22
|
|
7
|
|
17
|
5
|
7
|
5
|
17
|
18
|
-1
|
22
|
|
8
|
|
15
|
4
|
7
|
4
|
16
|
16
|
0
|
19
|
|
9
|
|
15
|
6
|
0
|
9
|
13
|
19
|
-6
|
18
|
|
10
|
|
16
|
3
|
4
|
9
|
15
|
27
|
-12
|
13
|
|
11
|
|
17
|
3
|
4
|
10
|
8
|
27
|
-19
|
13
|
|
12
|
|
16
|
2
|
6
|
8
|
10
|
25
|
-15
|
12
|
|
13
|
|
16
|
2
|
5
|
9
|
9
|
20
|
-11
|
11
|
|
14
|
|
14
|
1
|
7
|
6
|
6
|
16
|
-10
|
10
|
Coastal Union
9 Februari, 2014
No comments:
Post a Comment