COASTAL
Union imelala bao 1-0 dhidi ya Ruvu
Shooting kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara jana alasiri.
Bao hilo
lililofungwa dakika ya 80 kwa kichwa na Said Dilunga alieunganisha mpira wa
kona uliomshinda nguvu mlinda mlango wa Wagosi, Shaaban Kado.
Mchezo wa
jana ulianza kwa Ruvu Shooting kuchezewa mpira wa nguvu kwa dakika 15 za awali
hali iliyoamsha ari ya mashabiki wa Wagosi waliohudhuria kwa uchache lakini
kelele zao zilizizima uwanja mzima na kuwafanya maafande wa Jeshi la Kujenga
Taiafa kujikunyata mithili ya kuku alienyeshewa na mvua.
Hali
ilibadilika ilipofika dakika ya 17 baada ya Ruvu kufanya shambulizi la
kushtukiza hali iliyowashtua mashabiki wa Wagosi na kigoma kuzima hafla, lakini
uimara wa Shaaban Kado uliwasaidia kuendelea kushangilia.
Dakika ya
30, Kocha Yusuf Chipo alifanya mabadiliko akamtoa Mohammed Sudi na kuingia Abdi
Banda. Dakika mbili baadae Haruna Moshi Boban, almanusra awainue mashabiki wa
Wagosi baada ya kubaki yeye na golikipa lakini akagongesha mwamba wa juu na
mpira kudakwa kuilaini na mlinda mlango wa Ruvu.
Kabla ya
mchezo kuisha mwamuzi wa jana Hashim Abdallah kutoka Dar es Salaam alimuonyesha
kadi ya njano Boban bada ya akupishana nae kauli. Dakika moja kabla ya
mapumziko mwamuzi alimuonyesha kadi ya njano Danny Lyanga baada ya kucheza
madhambi lakini Danny alionyesha kukerwa na kadi hiyo akawa anabishana na
mwamuzi, lakini hafla akatoa kadi nyingine ya njano kwa Abdi Banda kwa madai
kuwa alimtolea kauli chafu.
Hivyo
kipyenga cha mapumziko kilipopulizwa mashabiki wa Wagosi walimjia juu mwamuzi
wa leo wakimshutumu kwa kufanya maamuzi mabaya hali iliyowavunja nguvu
wachezaji wao.
Kipindi cha
pili dakika ya 52 mwalimu Chipo alimtoa Yayo kato akaingia Kenneth Masumbuko,
ambae kwa kiwango kikubwa aliubadilisha mchezo ukawa na kasi iliyosaidia
kuingia kwenye lango la Ruvu ingawa bahati haikuwa ya Wagosi.
Dakika ya
60, Wagosi walipata kona iliyochongwa na Othman Tamim ambao uliguswa kidogo na
mchezaji wa Wagosi ukagonga mwamba wa juu na kugusa mstari, kulitokea mabishano
ya sekunde chache lakini mwamuzi akasema si bao.
Ilipotimu
dakika ya 70, Kocha Chipo alimtoa Suleiman Kassim ‘Selembe’ akaingia Ayoub
Semtawa ambae alijitahidi kumiliki mpira ili kupunguza presha ya wachezaji wa
Ruvu wlaioonekana mwiba katika ngome ya Wagosi.
Aidha baada
ya bao kuingia Wagosi walijitahidi kujitutumua ili kusawazisha lakini mabeki wa
Ruvu walikuwa makini kuhakikisha hawapotezi nafasi ya kurudi juu kwenye ligi.
Kutokana na
matokeo hayo Wagosi watashuka nafasi mbili chini kutoka ya tano mpaka ya saba,
kwasababu timu nne zilizofungana point yaani Coastal Union, Ruvu Shooting, Kagera
Sugar na Mtibwa Sugar jana zilishuka dimbani.
Wagosi
wamepoteza mchezo wa jana hivyo wamebaki na point zao 22, Mtibwa Sugar nao
wamepoteza dhidi ya Tanzania Prisons na kubakia na point 22, huku Kagera Sugar
waliotoka sare na Ashanti wakiambulia point moja hivyo kupata point 23.
Ruvu Shooting
wamekuwa nafasi ya tano wakijizolea point 25, ya sita inashikiliwa na Kagera
Sugar wakiwa na point 23, Coastal Union nafasi ya saba point 22 na Mtibwa Sugar
kutupwa nafasi ya nane point 22.
Mechi ijayo
ya Coastal Union, itachezwa katika uwanja wa Mkwakwani siku ya Jumamosi
Februari 22 dhidi ya Mbeya City.
Kikosi cha
jana: Shaaban Kado, Mbwana Kibacha, Othman Tamim, Juma Nyoso, Yusuf Chuma,
Jerry Santo, Dany Lyanga, Mohammed Sudi, Yayo Kato, Haruna Moshi ‘Boban’ na
Suleiman Kassim ‘Selembe’.
Sub: Said
Lubawa, Abdi Banda, Mohammed Miraji, Kenneth Masumbuko, Ayoub Semtawa na Behewa
Sembwana.
COASTAL
UNION
16 FEBRUARI,
2014
No comments:
Post a Comment