Kocha Yusuf Chipo akisisitiza jambo kabla ya mechi leo asubuhi.
Mtu mzima Boban, akitafakari namna atakavyowanyamazisha Wanyakyusa.
" Lazima mucheze kwa kujiamini tupo nyumbani baanaaa.."
Kocha wa magolikipa Adam Meja na kocha msaidizi Ally jangalu wakifuatilia darasa la Mwalimu Chipo.
KOCHA wa Coastal Union, Yusuf Chipo amesema mechi ya leo ni
ngumu haina matokeo lakini watakaoleta matokeo ni wachezaji baada ya kuamua
kucheza kwa kujituma.
Chipo, ameongeza kuwa amesikia Mbeya City ni timu ngumu,
lakini yeye hajui hilo kwasababu alipokuwa darasani akifundishwa ukocha ncini
ujerumani, aliambiwa timu zote zinakuwa na wachezaji kumi ndani na golikipa
mmoja.
“Sitegemei kuona kitu kipya kutoka kwa Mbeya City, bali
nataka kuwaona nyinyi mnacheza kitimu na kujituma, sitaki mtu akae nyuma
pelekeni timu mbele sisi tupo nyumbani tunataka ushindi. Kinachowasaidia Mbeya
City kupata sifa ni kujituma, na hicho naamini hata nyinyi mnaweza,” alisema.
Baada ya hapo alitaja kikosi cha leo na kuwaambia macho ya
mashabiki wa Coastal Union, kwenye mchezo huu wa Ligi Kuu Tanzania bara yapo
miguuni mwenu, mkifanya vizuri ama mkifanya vibaya ni kwa mustakabali wa maisha
yenu kisoka.
Kikosi cha leo kitakachoanza: Shaaban Kado, Mbwana Kibacha,
Abdi Banda, Yusuf Chuma, Juma Nyoso, Jery Santo, Danny Lyanga, Ally Nassor ‘Ufudu’,
Ayoub Semtawa, Crispian Odula na Haruna Moshi ‘Boban’.
Wachezaji wa akiba: Mansour Alawi, Suleiman Kassim ‘Selembe’,
Yayo kato, Mohammed Miraji, Ayoub Masoud, Behewa Sembwana na Kenneth Masumbuko.
Coastal Union inashuka dimbani kumenyana na Mbeya City,
wakiwa na point 22 nafasi ya saba katika msimamo wa ligi, ushindi wa leo dhidi
ya Mbeya City utamaanisha vitu viwili, kupata uhakika wa kumaliza ligi nafasi
nzuri na kuweka heshima kwa kuwafunga Mbeya City wanaotajwa kuwa wagumu
kufungika.
HAFIDH KIDO
MSEMAJI CUSC
TANGA- TANZANIA
FEB 22, 2014
No comments:
Post a Comment