Wednesday, October 23, 2013

Simba yalazimisha suluhu Tanga na Coastal Union










Coastal Union wamelazimishwa suluhu katika uwanja wa nyumbani wa Mkwakwani walipokutana na wekundu wa Msimbazi Simba.
Katika kipindi cha kwanza Simba walionekana kuelemewa kiasi golikipa wa timu hiyo Mganda Abel Dhaira alishindwa kustahamili mikiki ya Mganda mwenzake wa Coastal union, Yayo Kato ambaye alikuwa hampi nafasi. Hivyo Dhaira akasalimu amri dakika chache kabla ya kipindi cha kwanz akuisha na nafasi yake ikachukuliwa na golikipa namba mbili wa Simba Abuu Hashim.
Mpaka dakiak 45 za awali zinakwisha hakuna timu iliyoona lango la mwenzake lakini kwa namna Wagosi walivyokuwa wakishambulia kwa kasi walifurahi sana mwamuzi alipopuliza kipyenga kuashiria ni mapumziko.
Kipindi cha pili Simba walianza kwa kasi ambayo iliwatisha mashabiki wa Coastal, lakini haikudumu kwa muda mrefu mambo yakaanza kuwabadilikia.
Baada ya kuona hakuna mtu wa kutumbukiza mipira katikati, kocha wa Wagosi Joseph Lazaro, ambaye amechukua nafasi ya Hemed Moroco aliyeachia ngazi alimuingiza Uhuru Suleiman na kumtoa Danny Lyanga, halafu akamtoa Keneth Masumbuko na kumuingiza Pius Kasambale.
Mbali ya mabadiliko hayo bado uhaba wa mabao uliendelea kuiandama Coastal Union huku Simba wakiomba mchezo uishe kutokana na kuelemewa kila idara.
Katika hatua nyingine wana kidedea waliokuwa wakipiga ngoma walishikwa na bumbuwazi wasijue cha kufanya kutokana na ugumu wa mechi.
Simba ambao wametoka suluhu ya 3-3 na Simba Jumapili iliyopita hawakufurahishwa na suluhu ya leo mbali ya kuja na uongozi wote kuanzia Mwenyekiti Aden Range, Makamu Mwenyekiti Mzee Kinesi na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili Hanspope.
Kutokana na suluhu hiyo Wagosi wa Kaya wamevuna point 12, huku wakiendelea kushikilia nafasi ya 9 katika msimamo. Baada ya hapo watakabiliwa na mechi dhidi ya Mtibwa Sugar na Mgambo JKT zote zitachezwa Mkwakwani. Baada ya hapo watatoka nje kucheza na JKT Ruvu katika uwanja wa Chamazi jijini Dar es Salaam.
COASTAL UNION
23, OKTOBA 2013
TANGA, TANZANIA

Tuesday, October 22, 2013

Simba hawatoki Mkwakwani: Kidi




Mwalimu msaidizi wa Coastal Union Ally Ahmed ‘Kidi’ ameweka wazi kuwa timu yake ipo vizuri kilichobaki ni kuangalia namna watakavyojituma uwanjani siku ya kesho dhidi ya Simba Sport Club.

Akizungumza na blogu hii Kidi, ameonyesha kujiamini kukabiliana na Simba wenye point 19 wakishikilia nafasi ya tatu chini ya Azam na Mbeya City.

Mechi hiyo itakayochezwa katika uwanja wa Mkwakwani Jumatano Oktoba 23, itaamua hatma ya Wagosi wa Kaya wanaosuasua katika ligi baada ya kupoteza michezo miwili mfululuzo kati ya Ashanti United na Kagera Sugar.

Wagosi ambao wamecheza mechi mbili nje ya Tanga na kupoteza zote, wameahidi kurudisha heshima ya soka mkoani humo kwa kuanza kampeni ya kushinda mechi zote tatu watakazocheza uwanja wa nyumbani wa Mkwakwani, ambazo ni kati ya Simba, Mtibwa Sugar na Mgambo JKT.

“Sisi tupo vizuri ingawa nafsi yangu haina raha baada ya kupoteza michezo miwili mfululizo, vijana wangu wapo vizuri wanacheza kwa kuonana lakini hata sijui sababu ni nini wanashindwa kufunga. Naamini wataamka katika mechi hii, najua Simba ni timu nzuri na kubwa, lakini sidhani kama vijana wangu watakubali kufungwa kirahisi,” alisema Kidi.

Katika hatua nyingine bado suala la Kocha Mkuu wa timu hiyo Hamed Moroco halijakaa sawa baada ya maneno mengi kuzungumzwa bila kupatikana muafaka.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa viongozi wa Wagosi, kocha huyo tayari amemaliza mkataba wake na bado wapo kwenye majadiliano ima kumuongezea mkataba ama kufanya mazungumzo na kocha mwingine. Wamewataka mashabiki kuwa wapole wakati mchakato wa kocha ukifanyika, wakaweka wazi kuwa baada ya kujiengua msemaji wa timu Edo Kumwembe, kwa sasa mwenye mamlaka ya kutoa taarifa zozote ni mwenyekiti tu Hemed Hilal ‘Aurora’.

Aidha Coastal Union ipo nafasi ya 9 ikiwa imecheza michezo 9 kati ya 13, wamejizolea point 11 wakiwa wameshinda michezo miwili, suluhu tano na kupoteza miwili.

Baada ya mechi dhidi ya Simba, Coastal Union watashuka dimbani dhidi ya Mtibwa Sugar katika uwanja wa Mkwakwani Oktoba 26 siku ya Jumamosi, Oktoba 30 dhidi ya Mgambo JKT uwanja wa Mkwakwani na kumalizia mzunguko wa kwanza wa ligi dhidi ya JKT Ruvu Novemba 2 siku ya Jumamosi katika uwanja wa Chamazi jijini Dar es Salaam.

COASTAL UNION

22 OKTOBA, 2013

TANGA, TANZANIA

Saturday, October 19, 2013

Kagera Sugar Vs Coastal Union















COASTAL UNION
20 OKTOBA, 2013
BUKOBA, KAGERA

Tumefungwa 1-0 Kagera




Bundi bado hajaondoka kwenye paa la Coastal Union baada ya jana kupoteza mchezo mwingine dhidi ya Kagera Sugar ya mjini Kagera, lilikuwa ni bao la mkwaju wa penati lililotiwa kimiani na Salum Kanoni dakika ya 58 kipindi cha pili baada ya beki wa Coastal Union kuunawa mpira eneo la hatari.
Kagera Sugar hawakuonekana kuwa na uhai katika kipindi cha kwanza lakini wachezaji wa Wagosi walishindwa kutumia vema udhaifu huo hivyo kutoka kipindi cha kwanza bila kufungana.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi ambapo mabeki wa Kagera Sugar walikuwa na wakati mgumu wa kuzui kasi hiyo, ingawa hakuna kilichofanyika mpaka ilipofikia dakika ya 58 kulipotokea tafrani kwenye lango la wagosi na kuzalisha penati iliyoonekana kuwa na utata.
Baada ya hapo wachezaji wa Coastal Union walizidishiwa nguvu na Mganda Yayo Kato, Masumbuko Keneth na Uhuru Suleiman ambapo walibadilishana na Suleiman Kassim ‘Selembe’, Mohammed Sudi na Abdullah Othman.
Kasi ya Coastal Union ilisumbua ngome ya Kagera Sugar lakini mchezo wa kujiangusha na kupoteza muda kuliwamaliza nguvu Wagosi.
Hali hiyo ilikwenda mbali zaidi hata wachezaji na mashabiki kuwakataza watoto wanaookota mipira ‘Ball Boys’ kuacha kuokota mipira na badala yake wachezaji wa Wagosi waokote wenyewe.
Mpaka mwamuzi kutoka Mara ambaye alichezesha kwa kufuata sheria zote 17 za mchezo huo anapuliza kipyenga cha mwisho matokeo yalisomeka 1-0, ambapo Kagera sugar walitoka kifua mbele.
Baada ya mchezo huo Coastal Union wamekuwa katika hali mbaya ambapo kuna hatihati ya kushuka nafasi mbili chini kutoka ya nane mpaka ya 10.
Baada ya mchezo huo, mchezo unaofuata ni dhidi ya Simba utakaochezwa Mkwakwani jijini Tanga, Mtibwa Sugar utakaochezwa Mkwakwani, halafu tutacheza na Mgambo JKt uwanja wa Mkwakwani na kumalizia mzunguko wa kwanza wa ligi dhidi ya Ruvu JKt uwanja wa Chamazi jijini Dar es Salaam.
COASTAL UNION
20 OKTOBA, 2013
BUKOBA, KAGERA

Friday, October 18, 2013

Coastal Union yawasili Bukoba Kimyakimya....

 Yusuf Chuma na Abdallah Othman 'Sheikh Dullah ' kabla ya kupanda kivuko.

 Dokta wa timu akisakata rumba kabla ya kupanda feri..






COASTAL UNION
18 OKTOBA, 2013
BUKOBA, KAGERA

Thursday, October 17, 2013

Coastal Union yatua Mwanza na kufanya mazoezi katika uwanja wa CCM Kirumba ili kujiweka fiti.

 Kocha Mkuu wa Coastal Union Hemed Moroco (mwenye kofia), akiwa na viongozi wa timu hiyo Abdul Ubinde wa kwanza kulia na Miraji Wandi wa pili kulia, wa kwanza kushoto ni Uhuru Suleiman, kiungo wa timu hiyo; katika uwanja wa kimataifa wa JK nyerere kabla ya kupanda ndege kuelekea Mwanza na baadaye Bukoba kwa ajili ya mechi ya Ligi Kuu kati yao na Kagera Sugar siku ya Jumamosi wiki hii.
.


 Meneja wa Coastal Union, Akida Macha akiwa na Kocha wa timu hiyo Hemed Moroco...













COASTAL UNION
17OKTOBA, 2013
MWANZA, TANZANIA