Saturday, September 28, 2013

Mbeya City Vs Coastal Union nguvu sawa.

 Hakika Mbeya City wanapendwa sana na mashabiki wao, hilo liliwasaidia kuwachanganya wachezaji wa Coastal Union.

 Crispian odula akitafuta mbinu za kuwatoka mabeki wa Mbeya City huku akiwa hana msaada wowote.

 Danny Lyanga akikokota mpira huku Othman Tamim na Marcus Ndeheli wakiwa tayari kumsaidia.

 Yayo Kato akikimbilia mpira huku mchezaji wa Mbeya City akihakikisha hafanyi madhara yoyote.

Marcus Ndeheli wa Coastal Union na Richard Peter wakionyesha kadi nyekundu baada ya kutaka kupigana uwanjani.

Timu kisiki ambayo imejizolea umaarufu katika Ligi Kuu, Mbeya City imetoka suluhu na Coastal Union kutoka Tanga baada ya Mwagane Yeya, aliyeingia kipindi cha pili kukomboa bao la mapema lililofungwa na Haruna Moshi katika dakika ya 10.

Katika mechi hiyo ambayo ilikuwa na upinzani wa hali ya juu, Wagosi wa Kaya walimaliza dakika tisini wakiwa pungufu baada ya wachezaji wawili kupewa kadi nyekundu katika kipindi cha pili cha mchezo.

Kadi ya kwanza ilitolewa kwa Marcus Ndeheli baada ya kupishana maneno na mchezaji wa Mbeya City, Richard Peter baada ya mwamuzi kutoa faulo ya utata hivyo kuleta mtafaruku uliosababisha mwamuzi wa leo Oden Mbaga, kutoa kadi nyekundu kwa wachezaji hao.

Kadi ya pili ilitolewa dakika tano kabla ya mchezo kuisha baada ya Haruna Moshi, kudaiwa kutoa maneno ya kashfa kwa mwamuzi wa pembeni hivyo mwamuzi wa kati alipoelezwa kuhusu hilo bila kufikiri akamwonyesha kadi nyekundu.

Aidha, bao la Coastal Union lilifungwa kwa ufundi mkubwa baada ya Mbwana Kibacha kupiga krosi nzuri iliyotua miguuni mwa Boban na kuitendea haki kwa kuitia wavuni akimuacha mlinda mlango wa Mbeya City Juma Mwambusi akiona uvivu kuuokota wavuni.

Nalo bao la Mbeya City lilifungwa kiufundi baada ya Mwagane Yeya kutumia vema makosa ya mabeki wa Wagosi ambapo ulipigwa mpira wa adhabu ndogo na Yeya akapiga kichwa kizuri kilichopita katikati ya mikono ya mlinda mlango wa Wagosi, Said Lubawa aliyeingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Shaaban Kado aliyeumia kabla ya kipindi cha kwanza kuisha.

Kutokana na matokeo hayo Wagosi wamevuna point 10 wakiwa wamecheza mechi sita wakitoa suluhu mechi nne na kushinda mechi mbili.

Aidha mechi nyingine ni dhidi ya Azam FC ambayo watakutana nayo siku ya jumamosi wiki ijayo katika uwanja wa Mkwakwani.

COASTAL UNION
MBEYA, TANZANIA

Mbeya yavamiwa na kigoma cha Coastal

 Shamrashamra zikianza katika mitaa ya Uyole leo asubuhi.

Mashabiki wa Coastal Union wakiwa katika stand kuu ya Mbeya.

Hapakutosha leo mjini Mbeya.
 Tofauti ya mashabiki wa Coastal Union na timu nyingine ni swala, hapa mashabiki ambao walikuwa wakitoka Tanga walishuka eneo la Mdaula kupata swala ya Ijumaa jana mchana.

Mashabiki wa Coastal Union wakiwa hotel waliyofikia jijini hapo.
Shabiki wa Coastal Union Maarufu anaekwenda kama "Nyang'au Dungumaro akiwa katika mishe mishe ndani ya Jiji la Mbeya.

Mwenyekiti wa K/Hamasa na Ushangiliaji Miraji Wandi akiwa na Mjumbe wa K/Tendaji ya Coastal Union Ndg. Salim Amir (Legend) pamoja na mshauri Mkuu wa Rais wa Coastal Union Ndg. Salim Bawazir wakiwa ndani ya Jiji la Mbeya.

COASTAL UNION
28/09/2013
MBEYA - TANZANIA

Thursday, September 12, 2013

Habari kamili kuhusu maamuzi ya mechi ya Yanga na Coastal Union.

Mwamuzi wa mechi ya Yanga na Coastal Union, Martin Saanya akiwa katika moja ya matukio ya mechi hiyo. kulia ni mchezaji wa Coastal, Crispian Odula ambaye siku hiyo alipewa kadi tata akatolewa nje bila kutenda kosa, aliyeipa mgongo Camera ni mchezaji wa Yanga, Mbuyu Twitte na kushoto ni mchezaji wa Coastal, Suleima Kassim 'Selembe'. Mechi hii iliisha kwa suluhu ya 1 kwa 1.
YANGA imemponza mwamuzi, Martin Saanya wa Morogoro aliyechezesha mechi yao na Coastal Union ambaye amefungiwa mwaka mmoja kwa kuchezesha mchezo huo chini ya kiwango.
Saanya amepewa adhabu hiyo ya kutochezesha mechi yoyote ya soka ndani ya kipindi hicho sawa na mshika kibendera namba moja wa mechi hiyo, Jesse Erasmo ambaye alishindwa kutoa uamuzi sahihi wa adhabu ya penalti waliyopewa Coastal ndani ya dakika za nyongeza kabla ya mpira kumalizika na kusababisha sare ya bao 1-1.
Penalti hiyo ndiyo ilisababisha vurugu ambazo zilifanywa na mashabiki wa Yanga ambao , walimshambulia mwamuzi kwa chupa za maji na kuvunja kioo cha basi la wachezaji wa Coastal na kumjeruhi kichwani beki wa timu hiyo, Hamis Hamad aliyelazimika kuwahishwa hospitali.
Adhabu hizo zimekuja baada ya Bodi ya Ligi kupitia taarifa ya kamishna wa mechi hiyo, Omary Walii kutoka Arusha.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Silas Mwakibinga aliliambia Mwanaspoti kuwa: “Saanya na Erasmo wamefungiwa mwaka mmoja kuchezesha mechi za ligi baada ya bodi kupitia ripoti ya kamishina wa mchezo huo.
Saanya ameadhibiwa kwa kuchezesha chini ya kiwango na alitoa adhabu ya penalti iliyofungwa na Coastal akiwa mbali na tukio,” alisema Mwakibinga na kufafanua kuwa posho za waamuzi wa mechi kwa sasa ni Sh 250,000 mbali na nauli na teksi tofauti na zamani walipokuwa wanalipwa shilingi 170,000.
“Kwa upande wa Erasmo ndiye alikuwa eneo la tukio ilipotokea penalti, lakini alishindwa kumsaidia mwamuzi wa kati na kubaki ameduwaa kama asiye na uhakika.”
Mwakibinga alisema mbali na adhabu hizo kwa waamuzi, Kamati imemfungia kocha wa makipa wa Coastal Union, Juma Pondamali muda wa miezi mitatu na faini ya Sh1 milioni kwa kutoa lugha ya matusi kwa mashabiki wanaodaiwa ni wa Simba.
Katika hatua nyingine, Coastal imetozwa faini ya Sh100,000 kwa kuchelewa kikao cha maandalizi ya mechi asubuhi kwa dakika 23 huku Yanga ikitozwa faini ya Sh1 milioni kwa mashabiki wake kurusha chupa uwanjani na pia kumvamia mwamuzi huku viongozi wakishindwa kuwadhibiti.
Kuhusu basi la Coastal hakukuwa na taarifa kwani tukio lilitokea nje ya uwanja.
SOURCE: GAZETI LA MWANASPOTI


Tuesday, September 10, 2013

Coastal Union ya miaka ya nyuma imerudi tena... Kikosi cha ushindani.

 Kikosi cha zamani cha Coastal Union, Kuanzia kushoto wa kwanza ni Ali Mwaliza nyuma yake ni Yassin Napili, wa Kati ni Mohammed Kampira, Ally Maumba, Aggrey Chambo na Kassa Mussa, na wa kwanza ni Ali Majeshi wa nyuma ni Said Kolongo! Kikosi hiki ni baada ya ubingwa wa 1988.

                                                                     Ally Maumba. 

Umepita muda mrefu bila kupata taarifa za timu, lakini ni kutokana na kusimama kwa ligi kupisha mechi ya kumaliza kufuzu kwa michuano ya kombe la dunia, ambapo Taifa Stars imemaliza vibaya kwa kuchapwa na Gambia mabao 2 kwa 0.

Ligi itaendelea tena jumamosi Septemba 14 katika uwanja wa Mkwakwani ambapo Wagosi wa Kaya watakutana na maafande wa Prison kutoka Mbeya.

Itakumbukwa mechi mbili za awali Coastal Union ilishinda mabao 2 kwa 0 dhidi ya JKT Oljoro ya Arusha katika uwanja wa kumbkumbu ya Sheikh Amri Abeid, na kutoa suluhu ya 1 kwa 1 dhidi ya Yanga jijini Dar es Salaam katika uwanja wa Taifa.

Baada ya hapo jumapili Septemba 8, timu ilicheza mechi ya kirafiki dhidi ya Mafunzo kutoka Zanzibar ambao nao ni askari magereza kama Prison, matokeo ilikuwa ni Coastal Union 1 na Mafunzo 0. Mfungaji akiwa ni mchezaji kutoka Uganda, Kato Yayo Lutimba.

Leo tunaendelea na kumbukumbu za wachezaji walioiletea mafanikio Coastal, ambapo jina la Ally Maumba ndilo linalopamba ukurasa wetu kwa leo, habari hii ilitolewa kwenye ukurasa wa facebook lakini wachangiaji ndiwo watakaoandika habari ya leo. Naleta maneno yao kama walivyoaandika kumzungumzia Legend huyu.

Dhulfikar Ashraf dogo alikua na uwezo wa ajabu lakini ni Coastal yote ilikua na uwezo kwakila mchezaji ukiacha Maumba Iddrisa Ngulungu naye alikua muhimu sana anajua kukaba kutoa pasi za mwisho alikua fundi sana kama Kasa Mussa, Juma Mgunda, Aly Ruga, Kasim Mwajek, Mohammed Kampira, Doglas Muhani, Abuu Napili, Joseph Lazaro, Razak Yussuph ‘Careca’ Agrey Chambo, Abubakari Hassani, Mohammed Mwameja,  Makena, Rifat Said, Kolongo, Mwaliza, Jangalu, na  Tamimu.

Abdallah Merey ALI MAUMBA pekee mara ya mwisho nilikutana nae Hong Kong 2009... niliongea nae na kumuuliza swali kwa nini aliacha mpira bongo na hali alikua hakuna kama yeye? alitakiwa acheze timu moja na akina Zidane... alinijibu kuwa hajuti na uamuzi aliofanya wa kuacha mpira ni sahihi kwake....

Selemani Mohamedi Mohamedi mh ALLY MAUMBA alikuwa mtu mwengine natamani anbgekuwepo sasa

Razak Careca Uwezo wa ally maumba haujawahi kutokea kwa sasa alipofika uturuki aliwai kufanya mazozi nazani ilikua fanabache na alikubalika ila alikua anapita tu anakwenda kutafuta maisha mbele hakutaka kukaa hapo maumba anayumba kulia na kushoto mbele yuko nyuma yuko mashine mtoto wa chumbangeni historya haitofutika maisha hongera coastal 1988

Ally Kiraka Ni mchezaji pekee aliyetoka daraja la 4 na kuja kupandishwa 1kwa1 daraja kwa kwanza kipindi hicho ilikua hamna premier leaque!na alitokea maumau ya chumbageni!hii ni kwa uwezo wake alojaaliwa na mungu.

Ally Kiraka Azizi peti na salim buma ndo walikua viongozi wa mau mau na walikubali kumpeleka COASTAL UNION 1kwa1 kwa kua wao walijua uwezo wa ALI MAUMBA anafaa kucheza ligi kubwa!na alikua na kipaji,hata ahmed amasha alikua ni midifield bora tanzania lakini alikua akisema m2 ninaemuogopa hata kumsogelea ni ali maumba anapokua na mpira anaweza kukufanya jambo lolote la mshangao anapokua na ball!

Razak Careca Halo kiraka wajua sikuile coastal walipoifunga simba goli 4 refa akakubali 2 mimi na maumba hatukuepo tulikua tuko shellsheli na timu ya vijana ya tanzania wenzetu tuliokua nao walikua wanatuonea wivu sisi kwasababu yakua timu nzuri timu bora hata cochi wetu mohamed msomali akawa anaipenda coastal kwahiyo sizani kama coastal ya maumba mwakuluzo mwameja mgunda kasa kolongo doglas lazaro kolongo napil jangalu mwaliza agrey abubakari
Ally Kiraka Alipoondoka tanzania aliamua kwenda ulaya!na kwa sasa anaishi ITALY!na bado anaipenda coastal union!na niwaambiavyo yupo kwenye hii group ila ana2mia jina lingine!

Ally Kiraka Mechi pekee aliyowahi kufunga goli ali maumba ilikua ni bukoba alifunga goli la kichwa!hapo ni baada ya yassin napili kuachwa tanga na sentahafu akapewa mikoba abdallah tamimu mdaula.

Ally Kiraka Razak hiyo mecho 2lowapiga simba naikumbuka kama leo nilikuwapo!na refaree hadi leo nilimuhifadhi jina alikua ni abdul kawambwa,aliwabeba sana simba ila kwa uwezo walokua nao kina mgunda na mwakuluzo walikua hawashikiki,ilibidi edward chumila alivyoona simba sasa imezidiwa na ndipo alipomfuata refa na kumwambia kwani we refa huumalizi huu mpira?cc 2mechoka bwanaa!!FAT walimfungia refa abdul kawambwa,yaani kama leo yanijia ile mechi.

Razak Careca Maumba hawezi kusahaulika yeye ndio chachu ya ushindi alikua anajua sana mpira hatasijui nisemeje mana narudisha akili nyuma naona ni kama juzi naona jinsi anavyowapiga makanzu kina gagarino na kina athuman china ilikukua burudani ya ajabu sana hata ulaya hawana uwezo ule ila nikipaji alichopewa na mungu kwasasa hakuna tena
Ally Kiraka Ni mchezaji pekee aliyefananaishwa na farasi mweupe kwa maringo yake ya uchezaji mpira!kinanda alikua akiumiza kichwa sana akiambiwa maumba ni majeruhi na ndipo alipoamua ngulungu kumchezesha no.ya maumba na alikua akifit!
Razak Careca Simba walikua wanaomba mpira umalizike nakama mimi na maumba tungekuepo sijui ingekueje mana ingekua 10 . lakini pia kukosekana kwetu pia palikua hapaja aribika kitu kulikua na agrey chamba na kasimu mwajeki kwajula ilikua si timu ya kucheza ligi ya tanzania

Ally Kiraka Razak mpaka juzi nilikwenda kwa muchachu dar ya ya kupiga mishkaki ye akiiniita we coastal union!katika maongezi ananiambia coastal union walikua waki2tesa sana!nikamkumbushia hii mechi ya refa kukataa magoli kama mvua ananiambia ile ckuile ctaisahau k...

Razak Careca Hakuna kisicho wezekana timu tunayo nzuri sana kilichobaki ni umoja na mshikamano na kuwahamasisha wachezaji wetu majungu na masufuria yasiwe na nafasi mwenye majungu aende simba au yanga hapa coastal mbele kwa mbele akiingia yanga tuna mchapa simba ndio kabisa nyingi mwaka wetu asietaka ukweli aende yanga na simba hapa ni kufa kupona piga ua mungu ajaliapo watatukoma mwaka huu


COASTAL UNION
10TH SEPT,2013