Wednesday, July 29, 2015

MESSI WA SIMBA ATUA COASTAL UNION,ASEMA AMEAMUA KURUDI NYUMBANI.


KATIBU MKUU WA COASTAL UNION,KASSIM EL SIAGI AKIANGALIA NAMNA WINGA MPYA WA KULIA WA TIMU HIYO,IBRAHIM TWAHA "MESSI" ANAYOSAINI MKATABA WA MIAKA MIWII WA KUITUMIKIA TIMU HIYO KUSHOTO ANAYESHUHUDIA NI MENEJA WA COASTAL UNION AKIDA MACHAI.



MENEJA WA TIMU YA COASTAL UNION,AKIDA MACHAI KUSHOTO AKIMKABIDHI JEZI WINGA WA KULIA MPYA WA COASTAL UNION,IBRAHIM TWAHA "MESSI"MARA BAADA YA KUSAINI MKATABA WA MIAKA MIWILI WA KUITUMIKIA TIMU HIYO


Monday, July 27, 2015

NAMNA WANACHAMA WA TAWI LA MNARANI JIJINI TANGA WALIVYOWAPONGEZA WAJUMBE WA KAMATI YA UTENDAJI WAPYA WA COASTAL UNION

 MWENYEKITI WA TAWI LA MNARANI JIJINI TANGA,SHABENGA AKIZUNGUMZA KABLA YA KUMKARIBISHA KATIBU WA COASTAL UNION,KASSIM EL SIAGI
KATIBU MKUU WA COASTAL UNION,KASIM EL SIAGI AKIZUNGUMZA WAKATI WA HAFLA YA WANACHAMA WA COASTAL UNION TAWI LA MNARANI KUWAPONGEZA WAJUMBE WA KAMATI YA UTENDAJI WALIOTOKA KWENYE TAWI HILO KULIA NI KATIBU MSAIDIZI SALIM BAWAZIRI

KATIBU MSAIDIZI WA COASTAL UNION,SALIM BAWAZIRI AMBAYE PIA NI MWENYEKITI WA KAMATI YA USAJILI NA MWENYEKITI WA BARAZA LA WAZEE LA KLABU HIYO AKIZUNGUMZA KATIKA HALFA HIYO
MENEJA WA KLABU YA COASTAL UNION,AKIDA MACHAI AKIZUNGUMZA WAKATI WA HALFA HIYO YA KUWAPONGEZA WAJUMBE WALIOCHAGULIWA KUTOKA TAWI LA MNARANI JUZI
KATIBU WA TAWI LA MNARANI YENYE MASKANI YAKE MABANDA YA PAPA AKIZUNGUMZA KABLA YA KUANZA SHEREHE HIZO ZA KUWAPONGEZA WAJUMBE WA KAMATI YA UTENDAJI WALIOCHAGULIWA KWENYE UCHAGUZI MKUU ULIOPITA.




MWENYEKITI WA COASTAL UNION AKUTANA NA KAMATI MBALIMBALI

MWENYEKITI WA COASTAL UNION,DR.AHMED TWAHA AKIZUNGUMZA NA KAMATI ZA KLABU HIYO MWISHONI MWA WIKI KULIA NI KATIBU MKUU KASSIM EL SIAGI NA KUSHOTO NI MAKAMU MWENYEKITI SALIM AMII

MWENYEKITI WA COASTAL UNION DR.AHMED TWAHA AKIONGEZA MPANGO MKAKATI WA KLABU HIYO UTAKAOTUMIKA KATIKA KIPINDI CHA UONGOZI WAKE




MENEJA WA KLABU YA COASTAL UNION,AKIDA MACHAI AKISISITIZA JAMBO KWENYE MKUTANO HUO AMBAO ULIMUISHA KAMATI ZOTE ZILIZOUNDWA NA MWENYEKITI HUYO
WAJUMBE WA KAMATI MBALIMBALI WAKIMSIKILIZA MWENYEKITI WA COASTAL UNION,DR.AHMED TWAHA WAKATI WA KIKAO HICHO

\PICHA YA PAMOJA MWENYEKITI WA COASTAL UNION NA WAJUMBE WA KAMATI MBALIMBALI


     MWENYEKITI WA KLABU YA COASTAL UNION,DR.AHMED TWAHA AKIWA KWENYE PICHA YA PAMOJA NA KAMATI YA MIPANGO NA FEDHA.



UONGOZI wa Klabu ya Coastal Union umeitaka kamati ya ulinzi na usalama kuhakikisha inatimiza wajibu wake ipasavyo ikiwemo kuhakikisha vitendo vitakavyoweza kuigharimu timu hiyo wakati wa michuano ya Ligi kuu soka Tanzania bara vinazibitiwa.


Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa kikao baina ya Kamati ndogo ndogo zilizoundwa,Mwenyekiti wa Klabu ya Coastal Union,Dr.Ahmed Twaha alisema kuwa kumekuwa na vitendo vingi ambavyo vinajitokeza kwenye michuano ya Ligi kuu Tanzania bara na kuigharimu timu yetu na kulazimika kulipa faini ambayo ingeweza kufanya mambo mengine ya maendeleo.
Alisema kutokana na kuwepo kwa tatizo hilo ndio sababu pekee iliyopelekea kuundwa kamati hiyo ili kuweza kukabiliana na vitendo vinayoweza kuisababisha hasara ndani ya klabu hiyo kwani vinakwamisha juhudi za kupiga maendeleo.
   “Ukiangalia msimu uliopita tulipata hasara ya shilingi milioni 3 kwa makosa ya uwanjani na hii inasababishwa na mashabiki kitendo ambacho kinaharibu sura ya mkoa hivyo lazima kamati hii italisimamia suala hilo “Alisema Mwenyekiti huyo.
Aidha Mwenyekiti huyo aliitwisha mzigo mengine kamati ya Nidhamu na Maadili kuhakikisha watu wanaotukana kwenye mitandaa ya kijamii ikiwemo Facebook, Twiter na mengineyo watachukuliwa hatua kali za kisheria ili kukomesha vitendo hivyo.
Hata hivyo alisema kuwa kamati hiyo itakuwa na jukumu kubwa la kuhakikisha ulinzi na usalama unaimarishwa wakati wa timu hiyo itakapokuwa ikicheza mechi zake kwenye michuano ya Ligi kuu soka Tanzania bara.
 “Lakini pia zamani wapo watu walikuwa wakitengeneza vitabu vya tiketi na kufanya mapato kuwa madogo licha ya uwepo wa watu wengi hivyo huu ndio mwisho wao kamati hii pia itasimamia suala hilo kwani hali hii iliifanya klabu kukosa mapato “Alisema Mwenyekiti huyo.
Mwenyekiti huyo alisema kuwa wameweka mipango mizuri ya kuhakikisha timu hiyo inafungua matawi kwenye mikoa yote timu hiyo itakapokuwa ikienda kushiriki michuano ya Ligi kuu hapa nchini.

Thursday, July 23, 2015

HIVI NDIVYO MWENYEKITI MPYA WA COASTAL UNION,DR.AHMED TWAHA ALIVYOFURAHIA USHINDI WAKE NA WANACHAMA WA COASTAL UNION

MWENYEKITI WA KLABU YA COASTAL UNION,DR.AHMED TWAHA AKIWA NA WANACHAMA WA KLABU HIYO MARA BAADA YA KUMALIZIKA UCHAGUZI MKUU AMBAPO ULIMCHAGUA KUONGOZA KLABU HIYO





MWENYEKITI MPYA WA COASTAL UNION DR.AHMED TWAHA KUSHOTO AKISHIKANA MKONO NA MAKAMU MWENYEKITI WAKE,SALIM AMIRI KULIA NI MJUMBE WA KAMATI YA COASTAL UNION

MWENYEKITI MPYA WA COASTAL UNION DR.AHMED TWAHA AKINYANYULIWA JUU NA WANACHAMA WA TIMU HIYO MARA BAADA YA KUIBA KIDEDEA KWENYE UCHAGUZI HUO


MWENYEKITI MPYA WA COASTAL UNION DR.AHMED TWAHA AKIFUATILIA MATUKIO YA MKUTANO HUO





COASTAL YAMNASA KIPA KUTOKA VILLA SC YA UGANDA”



 UONGOZI wa Klabu ya Coastal Union umeingia mkataba wa miaka miwili na aliyekuwa mlinda mlango wa timu ya Villa SC ya nchini Uganda, Jackson Sabweto ili kuitumikia timu hiyo katika msimu mpya wa Ligi kuu soka Tanzania bara utakaoanza mwezi Septemba mwaka huu.

Utiliaji saini huo ulifanyika juzi makao makuu ya klabu hiyo yaliyopo barabara kumi na moja jijini Tanga na kushuhudiwa na viongozi mbalimbali akiwemo Katibu Mkuu, Kassim El Siagi.

Akizungumza , Katibu wa Coastal Union, Kassim El Siagi alisema kuwa nia ya kumsajili kipa huyo ni kuimarisha nafasi hiyo kwenye timu hiyo kabla ya kuanza michuano ya Ligi kuu soka Tanzania ili waweze kushiriki kwa mafanikio makubwa na tija.

El Siagi alisema kuwa usajili ambao umefanywa na klabu umepanga kuhakikisha msimu ujao kombe la Ligi kuu linatua kwenye viunga vya mitaa ya barabara ya kumi na moja jijini Tanga ili kurudisha historia yao ya muda mrefu tokea walipotwaa kombe hilo mwaka 1988.

   “Niseme tu usajili tulioufanya ni nzuri na utakuwa chachu ya kurejesha makali yetu ya mwaka 1988 wakati tulipochukua Ubingwa wa Ligi kuu hapa nchini “Alisema El Siagi.

Hata hivyo aliwataka wachezaji ambao hawajawasili mkoani hapa kuungana na wenzao kwenye mazoezi yanayoendelea kwenye viwanja vya shule ya sekondari Popatlaly chini ya Kocha Mkuu, Jackson Mayanja kuhakikisha wanawasili haraka iwezekanavyo.

NAMNA COASTAL UNION ILIVYOINGIA MKATABA NA KOCHA MKUU MAYANJA NA KOCHA WA MAKIPA FREDY LUMU


KOCHA WA MAKIPA WA COASTAL UNION,FREDY LUMU AKISAINI MKATABA WA KUWAFUNDISHA MAKIPA WA TIMU HIYO HIVI KARIBUNI KULIA NI KATIBU MKUU WA COASTAL UNION,KASSIM EL SIAGI


KATIBU MKUU WA COASTAL UNION,KASSIM EL SIAGI AKIMUONYESHA SEHEMU YA KUSAINI KOCHA MPYA WA COASTAL UNION,JACKSON MAYANJA MARA BAADA YA KUTUA MKOANI TANGA TAYARI KUKINOA KIKOSI HICHO.





KUSHOTO NI KOCHA MKUU MPYA WA COASTAL UNION,JACKSON MAYANJA AKIMKABIDHI MKATABA WAKE KATIBU MKUU WA COASTAL UNION MARA BAADA YA KUUSAINI TAYARI KUITUMIA TIMU HIYO

Sunday, April 6, 2014

Coastal Union 0-2 Mgambo Shooting.

 Danny Lyanga akiminyana na wachezaji wa Mgambo Shooting katika game ya jana uwanja wa Mkwakwani Tanga ambapo Mgambo waliibuka na ushindi wa mabao 2-0.

 Hamadi Juma akimimina majaro langoni mwa Mgambo Shooting jana.

 Mohammed Miraji wa Coastal Union akitafuta mbinu za kumchomoka mchezaji wa Mgambo jana.

 Yayo Kato Lutimba akiwa katikati ya wachezaji wa Mgambo jana uwanja wa Mkwakwani.

 Yayo Kato akiwa katika harakati zake.

 Suleiman Kassim 'Selembe' akiwania mpira na chezaji wa Mgambo katika uwanja wa Mkwakwani jana.

 Danny Lyanga jana alikuwa na jezi ya peke yake haina tangazo la Pembe... Why?

Danny Lyanga akicheza pembezoni mwa chaki huku mchezaji wa Mgambo akitafuta mbinu ya kumuibia mpira.

Kwa matokeo hayo Mgambo wamesogea kidogo kujiepusha na kushuka daraja, na Coastal Union imebaki na point 29 ikiwa nafasi ya 8 katika msimamo. Mechi mbili zilizobaki za nyumbani ni kati ya JKT Ruvu na Kagera Sugar.

COASTAL UNION
7 APRIL, 2014
TANGA TANZANIA