Friday, August 30, 2013

MECHI 11 ZA COASTAL UNION ZILIZOBAKI MZUNGUKO WA KWANZA.



RATIBA YA MECHI ZA COASTAL UNION MZUNGUKO WA KWANZA LIGI KUU TANZANIA BARA MSIMU 2013/14



JUMAMOSI
-:- September 14, 2013 Coastal U – Prisons (TANGA)

JUMATANO
-:- September 18, 2013 Coastal U – Rhino (TANGA)

JUMAPILI
-:- September 22, 2013 Coastal U – R.Shooting (TANGA)

JUMAMOSI
-:- September 28, 2013 Mbeya City – Coastal U (MBEYA)

JUMAMOSI
-:- October 5, 2013 Coastal U – Azam FC (TANGA)

JUMAPILI
-:- October 13, 2013 Ashanti Utd – Coastal U (DAR ES SALAAM)
JUMAMOSI
-:- October 19, 2013 Kagera S – Coastal U (BUKOBA)

JUMATANO
-:- October 23, 2013 Coastal U – Simba SC (TANGA)

JUMAMOSI
-:- October 26, 2013 Coastal U – Mtibwa S (TANGA)

JUMATANO
-:- October 30, 2013 Mgambo – Coastal U (TANGA)

JUMAMOSI
-:- November 2, 2013 JKTRuvu – Coastal U (PWANI)

COASTAL UNION
30 AGOSTI, 2013
DAR ES SALAAM, TANZANIA

Thursday, August 29, 2013

Coastal Union na Yanga zaingiza mil 152.

                                                         Hemed Moroco kazini jana...

Ally Mustafa ' batez' golikipa wa Yanga akijaribu kumhadaa nahodha wa Coastal Union, Jerry Santo kabla hajapiga penati ya jana. Yanga na Coastal Union walitoka suluhu ya 1-1, bao la Yanga ilifungwa na Didier Kavumbagu dakika ya 64 kipindi cha pili baada ya kuunganisha krosi iliyopigwa kutoka winga ya kushoto. Bao la Wagosi lilifungwa kwa njia ya penati dakika ya 90 baada ya Luhende wa Yanga kuushika mpira eneo la hatari.




MECHI ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Yanga na Coastal Union iliyochezwa jana (Agosti 28 mwaka huu) katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza Sh. 152,296,000.

Watazamaji 26,137 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo namba 14 ya VPL msimu wa 2013/2014 iliyomalizika kwa sare ya bao 1-1.

Viingilio katika mechi hiyo vilikuwa Sh. 5,000, Sh. 8,000, Sh. 15,000 na Sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa Sh. 36,947,427.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni Sh. 23,231,593.22.

Mgawo mwingine ni asilimia 15 ya uwanja Sh. 18,786,827.52, tiketi Sh. 3,818,890, gharama za mechi Sh. 11,272,096.51, Kamati ya Ligi Sh. 11,272,096.51, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) Sh. 5,636,048.26 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) Sh. 4,383,593.09.


Boniface Wambura
Ofisa Habari TFF
29 AGOSTI, 2013
DAR ES SALAAM, TANZANIA

Wednesday, August 28, 2013

Bus la wachezaji Coastal Union lavunjwa vioo na mashabiki wa Ynaga, Hamad apasuliwa.

Sikuwepo wakati tukio hili linatokea, lakini niseme wazi kuna upendeleo mkubwa unafanywa kwa Yanga. Kuanzia vyombo vya ulinzi mpaka viongozi wa soka. Ninavyojua timu ngeni ndiyo inayopewa ulizinzi kabla na baada ya mechi. lakini leo imekuwa kinyume, limeanza kutoka gari la Yanga likiwa na ulinzi mkali wa FFU. Gari la Coastal Union lilitoka bila ulinzi, kufika maeneo nje kidogo ya wauanja wa Taifa likaanza kushambuliwa kwa mawe, watu kadhaa wameumia na aliyeumia zaidi ni Hamad Juma 'Basmat', ambaye alikuwa mwiba leo upande wa kushoto. Amepasuliwa kichwani na ameshona nyuzi kadhaa.

Nakumbuka mwaka jana mzunguko wa kwanza Yanga walikuja Mkwakwani wkatufunga 2-0, lakini kabla ya mchezo kuanza walirusha mawe mengi sana kwa mashabiki wa Coastal Union, baada ya mchezo kuisha wakaendelea kufanya vurugu hatimaye waliondoka uwanjani wakiwa na ulinzi. Angalia tofauti, vurugu wameanzisha wao na ulinzi walipewa wao, leo sisi tumeondoka uwanjani kimya kimya lakini pia tumevamiwa tukiwa hatuna uliznzi. 

Je huu ni uungwana?

COATAL UNION
28 AGOSTI, 2013
DAR ES SALAAM, TANZANIA

Coastal Union mwanzo mwisho.....

                         Kikosi cha leo hiki kilichoanza dhidi ya Yanga uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Waamuzi wa leo wakiwa na manahodha wa timu zote mbili Jerry Santo wa Coastal Union na Nadir Haroub wa Yanga.
 Uhuru Suleiman akitafuta mbinu za kumtoka mchezaji wa Yanga kwenye mechi ya leo iliyoisha kwa suluhu ya 1-1.

Haruna Moshi 'Boban' professional player...
 Kimenukaaaaaaaa mashabiki wa Wagosi wa kaya kutoka Tanga moja kwa moja mpaka uwanjani, na kutoka uwanjani moja kwa moja mpaka Tanga. Ama kweli waja leo waondoka leo.

  
Hamad Juma akitafuta mbinui za kumtoka mchezaji wa Ynga, Mbuyu Twite huku Crispin Odula akiahidi kumsaidia.
                   Hapa Nadir Haroub akijaribu kumdhibiti 'toto tundu' Yayo Kato lakini alishindwa.

Abdi Banda kati kati ya wachezaji wa Yanga.
                             'Selembe' Suleiman Kassim akizongwa na Juma Abdul (12) wa Yanga.

Kulitokea tafrani kidogo wachezaji wa Yanga na Coastal Union, hatimaye mwamuzi akatoa kadi nyekundu kwa wachezaji wawili Odula (Coastal Union) na Simon Msuva (Yanga).
 Hii ndiyo penalt aliyofunga Jerry Santo dakika ya 90 baada ya David Luhende wa Yanga kuunawa mpira eneo la hatari.

                                                             
                                                                   Ushangiliaji ulihusu.

woooyyooowoooyoooo.... 
                      Yanga wa maaajiii. hilo toto lao la sanamu sijui walilibeba vipi maana lilikuwa zito balaa.

     Kocha wa Yanga Ernst Brants alisema 'refaree was the man of the match, he was totally unfair.'

COASTAL UNION
AGOSTI 28, 2013
DAR ES SALAAM, TANZANIA

Tuesday, August 27, 2013

Kidi: Kwa sasa hatuzungumzi tena kuhusu mechi ya Yanga.

KOCHA msaidizi wa Coastal Union, Ally Mohamed 'Kidi' amesema kwa sasa hakuna tena mazungumzo wala majibishano kuhusu mechi ya kesho dhidi ya Yanga bali wanasubiri vitendo tu.

Mechi hiyo ya Ligi Kuu Vodacom inawakutanisha Wagosi na Yanga wote wakiwa wameshinda kwenye mechi zao za ufunguzi ambapo kocha wa Yanga Ernest Brandist amesema hiyo itafanya mechi kuwa ngumu kwani timu zote zitashuka dimbani zikiwa na matumaini ya kuendeleza ubabe katika ligi.

 
Kocha msaidizi wa Coastal Union, Ally Mohamed 'Kidi' aliyekaa akimwangalia mchezaji Othman Abdullah (kulia) akimwelekeza kitu kocha mkuu wa timu hiyo Hemed Moroco (katikati), jijini Arusha kabla ya mechi dhidi ya JKT Oljoro.

Aidha kwa mujibu wa Kidi, wagosi wa kaya wapo vizuri kila idara kuanzia ulinzi, viungo mpaka safu ya ushambuliaji.

"Sisi tupo vizuri bob, kila idara imekamilika we mwenyewe unajua hatuna haja ya kuzungumza sana tunasubiri kesho kutumbukiza mabao tu."

Hata hivyo vyombo vya habari kwa mara ya kwanza vimeripoti hofu ya kocha wa Yanga kwa Coastal Union ambapo alipohojiwa kwenye mazoezi jana katika uwanja wa Loyola, amesema: "Mechi ya kesho ni ngumu, Coastal Union wamesajili vizuri na kwakuwa walishinda mechi ya kwanza lazima wachezaji watakuwa na morali ya mchezo. Haruna Moshi na yule mchezaji wa Uganda 'Yayo Kato' ni wachezaji wazuri." liliripoti moja ya gazeti la kila siku nchini.

Katika mechi ya ufunguzi Coastal Union walishinda mabao 2-0 dhidi ya JKT Oljoro katoka uwanja wa kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha. Yanga nao walipata ushindi mnono wa mabao 5-1 dhidi ya timu iliyorudi ligi kuu msimu huu Ashanti United 'Watoto wa Ilala' katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

 COASTAL UNION
27 AGOSTI, 2013
DAR ES SALAAM, TANZANIA

Sunday, August 25, 2013

Mechi ya Agosti 28 jumatano Yanga Vs Wagosi, uwanja wa Taifa.

Baada ya kuanza vema ligi kuu msimu huu kwa kuwachezesha kwata maafande wa Oljoro JKT jijini Arusha, Coastal Union ipo tayari kukutana na Yanga siku ya jumatano wiki hii.

Tayari mwalimu na viongozi wameshazungumza na wachezaji wanasema kuna uwezekano mkubwa timu ikafanya vizuri kutokana na morali waliyoanza nayo.

Kwa sasa timu ipo mahala salama wakifanya mazoezi ya nguvu ili kuhakikisha ile azma ya kushinda kila mechi inatimia kwa asilimia 100.

Hata hivyo kwenye mitandao ya kijamii mechi ya Yanga  na Wagosi imeonekana kuzua gumzo kubwa kiasi inaonekana mechi hiyo imeanza kuchezwa midomoni kabla ya timu kushuka dimbani. Hali hiyo inaonyesha wazi namna mashabiki wa timu zote walivyokuwa na hamasa ya mechi ya jumatano katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Hiyo itakuwa ni mechi ya pili kwa timu zote kwenye ligi kuu ambapo Coastal Union ya jijini Tanga waliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya JKT Oljoro wakati Yanga ya dar es Salaam ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya Ashanti United nayo ya jijini.

COASTAL UNION
25 AGOSTI, 2013
DAR ES SALAAM, TANZANIA

Saturday, August 24, 2013

Morocco: Hizi ni salamu za yangu Jumatano ijayo....

 Mashabiki wa Coastal Union.... kuna mtu namfananisha hapa sijui ni nani... Kwa jaaaam.

                                               Morocco kama Mourinho vile...

                                           Jamani Kado muda si mrefu atarudi timu ya Taifa.

                                        Haruna leo alijitoa mhanga sana.... Kaupiga mwingi.

 Huyu Marcus Ndehele akisalimiana na kocha wake wa zamani wa Oljoro JKT, Fikiri Elias.

           Said Lubawa naye akisalimiana na afande mwenzie wa zamani baada ya mchezo kuisha.


Hatimaye vijana wa Coastal Union wamefanya walichoagizwa na mwalimu wao Hemed Morocco baada ya kuwatandika Oljoro JKT mabao 2-0.

Katika mchezo huo ambao kwa upande mmoja unaweza kusema Oljoro hawakuwa tayari kucheza ama walilazimishwa kwa namna walivyokuwa wanapoteana dimbani mpaka kuruhusu mabao mawili ambapo moja limetokana na makosa ya golikipa na la pili ni kosa la beki.

Hata hivyo wana Mangush walishindwa kutumia vema nafasi walizopata baada ya kukosa mabao takriban manne kwa vipindi vyote ambapo Selembe peke yake amekosa mabao mawili, Yayo amekosa bao moja na Odula pia amekosa moja.

Abdi Banda ndiye aliyeanza kuipa furaha Coastal Union ndani ya dakika ya 11 baada ya kupokea pasi kutoka kwa Selembe akiwa umbali mdogo tu kutoka mstari wa kati ya uwanja winga ya kushoto, akamwangalia golikipa amekaa upande gani akafanya kama anapiga krosi mpira ukatumbukia moja kwa moja wavuni.

Baada ya hapo JKT Oljoro walibadilika kidogo wakafanya mashambulizi ingawa hayakudumu sana, Coastal Union wakaanza kujipanga upya na kuendeleza jaramba. Ilipotimia dakika ya 35 ulipigwa mpira wa adhabu kuelekea langoni mwa Oljoro baada ya Hamad Juma kuchezewa madhambi, mchezaji wa Oljoro akawa anajaribu kuokoa lakini mpira ukambabatiza usoni Crispian Odula ukatumbukia wavuni katika dakika ya 36.

Mpaka mwamuzi wa leo Jacob Adengo kutoka Mwanza anapuliza kipyenga kuashiria mpira ni mapumziko matokeo yalisomeka Coastal Union 2-0 Oljoro JKT.

Kipindi cha pili kilianza kwa kusomana timu zote mbili mpaka dakika ya 50 ambapo Wagosi waliendelea kulisakama lango la maafande hao bila huruma. Lakini wagosi bahati haikuwa yao kwani waligosi amabao mengi sana ya wazi. Hata hivyo golikipa Shaaban Kado aliokoa michomo mingi sana.

Ilipofika dakika ya 21 kipindi cha pili kocha Morocco alifaya mabadiliko ambapo alimuingiza Masumbuko Keneth akamtoa Uhuru Suleiman. baadaye dakika ya 35 kipindi cha pili alitolewa Selembe akaingia Pius Kisambale na ilipofika dakika ya 44 muda mchache kabla ya kipyenga cha mwisho kupulizwa alitoka Crispian Odula akaingia Mohammed Sudi.

Kocha Morocco anasema hizi ni salamu kwa wana jangwani jumatano wiki ijayo atakapokutana nao uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.

Kikosi cha leo ni: 
1. Shaaban Kado.
2. Hamad Juma.
3. Abdi Banda.
4. Marcus Ndehele.
5. Juma Nyoso.
6. Razak Khalfan.
7. Uhusu Suleiman.
8. Haruna Moshi.
9. Kato Yayo.
10. Crispian Odula.
11. Suleiman Kassim ‘Selembe’.

Sub: Said Lubawa, Mbwana Kibacha, Othaman Tamim, Pius Kisambale, Masumbuko Keneth, Yusuf Chuma na Mohammed Sudi.


COASTAL UNION
24 AGOSTI, 2013
ARUSHA, TANZANIA


Mechi ya leo JKT Oljoro Vs Coastal Union katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

 Mwenyekiti wa Coastal Union Hemed Hilal 'Aurora' akisalimiana na Yayo Kato, kabla ya mpira kuanza.

                                         Kikosi cha leo hiki kilichoanza dhidi ya Oljoro JKT.




                         Yayo Kato akituliza mpira mbele ya Majaliwa Mbaga wa JKT Oljoro.

 Mashabiki wa Coastal Union waliuteka uwanja wa Sheikh Amri Abeid leo. Watu wote mazungumzo ni kigoma hiki.

 Yusuf Machogote wa JKT Oljoro akijaribu kukimbilia mpira na Suleiman Selembe leo.

 Hiki ni kipindi cha pili Selembe alikosa bao la wazi yeye na golikipa. Na hili lilikuwa bao la pili kukosa baada ya kipindi cha kwanza kupewa pasi murua na Yayo akabaki na golikipa akapiga kichwa mpira ukatoka nje.

 Uhuru Suleiman akijaribu kutafuta mbinu za kumtoka mchezaji wa Oljoro leo.

 Selembe akimpongeza Abdi Banda baada ya kufunga bao la kwanza ndani ya dakika 11 ya mchezo.

 Hapa Banda akiwa anarudi kutoka kufurahia na mashabiki wa Coastal Union waliofurika uwanjani leo.

 Mwamuzi wa leo kutoka Mwanza Jacob Adengo akimwonyesha kadi ya Njano Banda kwa kutoka nje ya uwanja wakati mpira ukiendelea.

 Shaaban Kado leo alikuwa nyota ya mchezo baada ya kuopoa michomo mingi ambayo iliyawacha watu mdomo wazi.

 Hapa mashabiki wa Oljoro wakiingia uwanjani kipindi cha pili baada ya kupigiwa simu waje kuongeza nguvu maana kigoma cha Wagosi kiliwazidi nguvu.

                                                 Morocco akisisitiza jambo uwanjani.

                                                         Doctoooor au basi......

               Haruna Moshi Boban leo alivutia watu wengi kutokana na style yake ya kucheza.

 Hamad 'Basmat' akikokota mpira bila wasiwasi wowote, leo alipiga beki nzuri hakuna mchezji aliyethubutu kumsogelea.

                                                Selembe akituliza mpira kwa ufundi mkubwa.

                         Haruna Moshi 'Boban' akituliza mpira mbele ya wachezaji wawili wa Oljoro.


              Mashabiki wa Coastal Union baada ya mpira kuisha ilikuwa raha tu mwanzo mwisho.

Nassor Binslum, Akida Machai na Heme Hilal wakiwa katika viunga vya jiji la Arusha baada ya mechi kuisha kwa ushindi 2-0.

COASTAL UNION
24 AGOSTI, 2013
ARUSHA, TANZANIA