Kikosi cha Coastal Union ‘Wagosi wa Kaya’ kitaondoka jijini
Tanga kuelekea mji msafi kuliko yote Tanzania, Moshi kwa ajili ya kuweka kambi
ya siku kadhaa kabla ya kukutana na JKT Oljoro kwenye mechi ya ufunguzi ligi
kuu ya Vodacom Tanzania bara msimu ujao jijini Arusha.
Kwa mujibu wa mkurugenzi wa ufundi Nassor Ahmed Binslum, timu
imeamua kuelekea Moshi kutokana na hali ya hewa ya Mji huo kufanana na ya Arusha
hivyo itasaidia wachezaji kuzoea hali ya baridi.
Kitu kingine alichozungumza Binslum ambapo walishauriana na
kocha mkuu wa Wagosi, Hemed Morocco ni kuwafanya wachezaji kutoka nje ya mkoa
wa Tanga kwani tangu walipoanza kukaa kambini hawajawahi kucheza nje ya mkoa
huo mbali ya kufanya vizuri kwenye mechi zote za majaribio kitaifa na
kimataifa.
Kwa maelezo ya kocha inabidi wachezaji wakae mbali na
mashabiki ili kuona uwezo wao pindi wakicheza mechi za ugenini hasa
ikizingatiwa ligi kuu itazitaka timu kucheza nyumbani na ugenini. Pindi
watakapocheza nyumbani watapata mashabiki wengi lakini wakiwa nje ya Tanga
watakutana na kelele za mashabiki wa timu pinzani zitakazowachanganya.
Mpaka sasa timu imepangiwa kuondoka Jumatatu ambapo jumamosi
itaelekea Mombasa kucheza mechi moja ya kirafiki na kuelekea Moshi moja kwa
moja.
“Timu itaelekea Mombasa jumamosi hii kucheza mechi moja ya
kirafiki, halafu itaelekea Moshi itakapoweka kambi mpaka tarehe 24 mwezi huu
watakapoingia Arisha kucheza na JKT Oljoro kwenye mechi ya ufunguzi,” alisema
Binslum.
Kutokana na usajili wa mwaka huu wapenzi wengi wa soka
Tanzania wamekuwa wakiitabiria kufanya vizuri Coastal Union kwani timu nyingi zimeshindwa kutumia vema nafasi
ya kusajili wacezaji wenye uwezo. Coastal Union imefanikiwa kunasa wachezaji
wawilai kutoka Simba SC, wawili kutoka JKT Oljoro, mmoja ktoka Jamhuri ya
Pemba, mmoja kutoka Polisi Morogoro, mmoja kutok URA ya Uganda na mmoja kutoka
Bandari ya Mombasa wakati mwingine ametoka Azam FC.
Mungu ibariki Tanga, Mungu ibariki Coastal Union.
COSTAL UNION
16 AGOSTI, 2013
DAR ES SALAAM, TANZANIA
No comments:
Post a Comment