Baada ya kuanza vema ligi kuu msimu huu kwa kuwachezesha kwata maafande wa Oljoro JKT jijini Arusha, Coastal Union ipo tayari kukutana na Yanga siku ya jumatano wiki hii.
Tayari mwalimu na viongozi wameshazungumza na wachezaji wanasema kuna uwezekano mkubwa timu ikafanya vizuri kutokana na morali waliyoanza nayo.
Kwa sasa timu ipo mahala salama wakifanya mazoezi ya nguvu ili kuhakikisha ile azma ya kushinda kila mechi inatimia kwa asilimia 100.
Hata hivyo kwenye mitandao ya kijamii mechi ya Yanga na Wagosi imeonekana kuzua gumzo kubwa kiasi inaonekana mechi hiyo imeanza kuchezwa midomoni kabla ya timu kushuka dimbani. Hali hiyo inaonyesha wazi namna mashabiki wa timu zote walivyokuwa na hamasa ya mechi ya jumatano katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Hiyo itakuwa ni mechi ya pili kwa timu zote kwenye ligi kuu ambapo Coastal Union ya jijini Tanga waliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya JKT Oljoro wakati Yanga ya dar es Salaam ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya Ashanti United nayo ya jijini.
COASTAL UNION
25 AGOSTI, 2013
DAR ES SALAAM, TANZANIA
No comments:
Post a Comment