Danniel Lyanga akitafuta mbinu za kumpita wajina wake Daniel Agu wa 3 Pillars kutoka Nigeria leo wakati wa mechi ya kirafiki iliyokutanisha timu hizo kwenye uwanja wa Mkwakwani. Matokeo ni 0-0.
Abdi Banda akijiandaa kufyatua bunduki kwa guu lake la kushoto huku mchezaji wa 3 Pillars akifikiria namna ya kumzuia asifanye balaa hilo.
Danniel Lyanga akiutazama mpira uliopigwa juu kabla haujatua huku mchezaji wa 3 Pillars akiusubiri kwa hamu. Kwa mbali Jerry Santo akiwa tayari kumpa msaada Danny.
Hapa ni baada ya kupigwa mpira wa adhau ndogo na mchezaji wa 3 Pillars, Kibacha, Danny na Razak wakimwangalia golikipa wa leo Said Lubawa kama ataweza kuuzuia.
Crispian Odula akiwa katika harakati za kumpa mwili beki wa 3 Pillars.
Wanaume kazini Danny Lyanga akitanguliziwa mpira na Razak Khalfan. Mechi ya leo iliisha suluhu ya 0-0.
COASTAL UNION
10 AUGUST, 2013
TANGA, TANZANIA
No comments:
Post a Comment