Mke wa kocha mkuu
wa coastal Union B, Joseph Lazaro amefariki dunia alfajiri ya leo katika
Hospitali ya Bombo mjni Tanga baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Akitoa taarifa
hiyo kutoka Tanga mwenyekiti wa hamasa Coastal Union, Miraji Wandi amesema mke
wa Lazaro alikuwa akisumbuliwa na kiharusi (Stroke) kwa muda mrefu mpaka mauti
yalipomfika saa tisa usiku wa kuamkia leo.
Kocha huyo
ambaye amechukua mikoba ya aliyekuwa kocha wa timu B, Bakari Shime amesema
msiba utakuwepo nyumbani kwake Makorora Mzingani na maziko ya kumpumzisha mkewe
Bi Farida Mussa, yatafanyika leo saa kumi alasiri kwenye makaburi ya Maftah.
Joseph Lazaro
pia aliwahi kuichezea Coastal Union na kuwa chachu ya mafanikio yaliyowafanya
wana Mangush kuwa wafalme wa soka Tanzania Bara mwaka 1988.
Mungu ailaze
roho ya marehemu Farida Mussa mahala pema peponi Amin.
COASTAL UNION
AGOST 5, 2013
DAR ES
SALAAM, TANZANIA
No comments:
Post a Comment