Tuesday, December 31, 2013

Boban ni mchezaji halali wa CUSC

 Kikosi cha maangamizi cha CUSC....

 Hiki ni kipande cha gazeti la leo Jumatano Januari 1,2014 gazeti Mtanzania kuhusu habari za Boban.



Haruna Moshi, akimiliki mpira katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha wakati akiitumikia CUSC kwenye mechi yake ya kwanza ligi kuu na Wagosi wa Kaya. Ilikuwa ni mechi dhidi ya Oljoro JKT, ambapo CUSC iliibuka na ushindi wa mabao 2-0.
 
Ndugu zangu,
WIKI hii kumekuwa na habari za upotoshaji juu ya kutimuliwa kwa kiungo mshambuliaji wa Coastal Union ‘Wagosi wa Kaya’, Haruna Moshi ‘Boban’.
Ninaziita habari za upotoshaji kwasababu hazina ukweli, na mara nyingine mtu anaweza kuenda mbali zaidi na kufikiri kuwa kuna hujuma zinafanyika dhidi ya timu yetu ili wachezaji wasicheze kwa moyo wakati wa mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Tanzania Bara, unaotarajiwa kuanza Januari 25 mwaka huu.
Gazeti moja la michezo, jina tunalihifadhi limeripoti likimnukuu kiongozi mmoja wa Wagosi wa Kaya, jina pia tunalihifadhi kutokana na heshima yake; kuwa Coastal Union haina mpango wa kumuongezea mkataba ‘Boban’ baada ya kumalizika miezi sita ijayo kwasababu za utovu wa nidhamu.
Habari hizo hazina ukweli kwasababu hakuna kikao kilichokaliwa kujadili mustakabali wa mchezaji huyo. Ni kweli Boban, hajaripoti kambini mpaka sasa; lakini uongozi wa juu akiwemo meneja wa timu unazo taarifa za mchezaji huyo.
Kuwa na nidhamu ama kutokuwa na nidhamu, kumtimua ama kumuacha mchezaji, wanaoamua hayo ni uongozi wa juu kupitia kamati zake ndogondogo kama za mashindano, usajii na nidhamu. Na si mtu mmoja mmoja.
Hivyo kwa niaba ya Mwenyekiti wa Coastal Union, Hemed Hilal ‘Aurora’ timu inaomba radhi wanachama wa CUSC, kutokana na kuumizwa kwa namna moja ama nyingine na taarifa hizo za upotoshwaji.
Wagosi wa Kaya, bado wana mkataba wa miezi sita na Boban, kuongezewa ama kutoongezewa mkataba suala hilo litajadiliwa kati ya mchezaji na viongozi pale utakapofika ukingoni.
HAFIDH A. KIDO
MSEMAJI CUSC
JANUARI 1, 2014
DAR ES SALAAM, TANZANIA

No comments:

Post a Comment