Sunday, February 23, 2014

Mechi saba za Coastal Union zilizobaki.



Ikiwa hakutakuwa na mabadiliko yoyote kutoka Shirikisho la soka nchini (TFF), mechi saba za Coastal Union zilizobaki msimu huu zitakuwa ni dhidi ya Ashanti United Machi 8, 2014 uwanja wa Mkwakwani Ifikapo Machi 12 katika uwanja wa Taifa jiji Dar es Salaam Wagosi  wa Kaya watacheza na Simba, wakati Machi 15 katika uwanja wa Azam Complex Chamazi, Wagosi watakipiga na Azam FC katika mechi ya 22 ligi kuu ya Vodacom.
Aidha ifikapo Machi 23 mwaka huu Wagosi wa Kaya watasafiri mpaka Manungu kumenyana na Mtibwa Sugar, na Machi 30 Coastal Union itafunga mwezi dhidi ya Mgambo JKT katika uwanja wa Mkwakwani Tanga huku Wagosi wakiwa wageni wa Mgambo.
Ifikapo Aprili 14, 2014 Coastal Union itakutana na JKT Ruvu katika uwanja wa Mkwakwani huku ikikamilisha ratiba ya Ligi kwa mechi dhidi ya Kagera Sugar katika uwanja wa Mkwakwani tarehe 27 April, mwaka huu.
Mpaka sasa Coastal Union imecheza mechi 19 tangu ligi ianze, imeambulia point 25 katika nafasi ya sita nyuma ya Yanga point 38, Azam (36), Mbeya City (35), Simba (32) na Kagera Sugar (26).
MSEMAJI- COATAL UNION
TANGA, TANZANIA
FEB 23, 2014

No comments:

Post a Comment