Sunday, February 9, 2014

Rhino Rangers Vs Coastal Union (0-1)



Baada ya ushindi wa leo katika mechi kati ya Rhino Rangers na Coastal Union kwenye uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora, ambapo Jerry Santo aliipatia Coastal Union bao la mapema dakika ya pili, sasa tumepanda mpaka nafasi ya tano.
Kwa mujibu wa msimamo wa ligi, Coastal Union kabla ya ushindi wa leo walikuwa na point 19 katika nafasi ya saba. Baada ya Mtibwa Sugar kupoteza mchezo wake dhidi ya Mbeya City, wameendelea kubaki na point 22, ambazo Coastal pia wamezifikia hivyo kuwafanya kushuka nafasi moja chini kutokana na tofauti ya mabao ya kushinda na kushindwa.
Hivyo habari njema kwa mashabiki wa Coastal Union, ni kuwa kwa sasa tunaendeleza wimbi la ushindi ili kujeweka katika nafasi nzuri hasa ikizingatiwa kocha ameamua kufanya mabadiliko ya kikosi chake ili kupata ushindi kila mechi inayokuja.
Anaeshika nafasi ya kwanza ana point 36, na sisi kutokana na mechi tisa tulizobakisha ikiwa tutashinda zote tutakuwa na jumla ya point 49. Kwa maana hiyo uwezekano wa kumaliza nafasi tatu za juu upo ikiwa tutafanya vizuri katika mechi tisa tulizobakisha ambazo ni dhidi ya:
Simba, Kagera Sugar, Azam FC, Mgambo JKT, JKT Ruvu, Ruvu Shooting, Ashanti, Mtibwa Sugar na Mbeya City.  
Ikumbukwe kuwa mechi tatu za awali kabla ya leo kukutana na Rhino Rangers tulivaana na JKT Oljoro (1-1), Yanga (0-0) na Tanzania Prisons (0-0).
Kikosi leo kilichokutana na Rhino Rangers kilikuwa hivi: Shaaban Kado, Mbwana Kibacha, Othman Tamim, Yusuf Chuma, Juma Nyoso, Jery Santo, Suleiman Selembe, Mohammed Sudi, Crispian Odula, Haruna Boban na Danny Lyanga.
Na huu ndio msimamo wa ligi Kuu Tanzania Bara baada ya mechi za leo jioni.

Top of Form
Bottom of Form
Pos.
Logo
Club
P
W
D
L
GF
GA
GD
Pts
1
Azam FC
16
10
6
0
29
10
19
36
2
Young Africans FC
16
10
5
1
34
12
22
35
3
http://www.azamfc.co.tz/sites/default/files/imagecache/team_logo_tiny/mbeya%20city.jpg
17
9
7
1
23
13
10
34
4
Simba SC
17
8
7
2
32
15
17
31
5
http://www.azamfc.co.tz/sites/default/files/imagecache/team_logo_tiny/Picture%204_0.png
17
4
10
3
11
7
4
22
6
Mtibwa Sugar FC
17
5
7
5
23
21
2
22
7
Kagera Sugar FC
17
5
7
5
17
18
-1
22
8
http://www.azamfc.co.tz/sites/default/files/imagecache/team_logo_tiny/shooting_0.jpg
15
4
7
4
16
16
0
19
9
JKT Ruvu Stars
15
6
0
9
13
19
-6
18
10
http://www.azamfc.co.tz/sites/default/files/imagecache/team_logo_tiny/Logo_Ashant%2011i.jpg
16
3
4
9
15
27
-12
13
11
JKT Mgambo
17
3
4
10
8
27
-19
13
12
http://www.azamfc.co.tz/sites/default/files/imagecache/team_logo_tiny/oljoro.jpg
16
2
6
8
10
25
-15
12
13
http://www.azamfc.co.tz/sites/default/files/imagecache/team_logo_tiny/JKT_0.jpg
16
2
5
9
9
20
-11
11
14
http://www.azamfc.co.tz/sites/default/files/imagecache/team_logo_tiny/Prisons_FC.jpg
14
1
7
6
6
16
-10
10

Coastal Union
9 Februari, 2014

Wednesday, February 5, 2014

Tanzania Prison 0-0 Coastal Union, Mbeya



Kwa mara ya tatu mfululizo Coastal Union ‘Wagosi wa kaya’, wametoka suluhu katika mechi za mzunguko wa pili Ligi kuu Tanzania bara, baada ya kukutana na Tanzania Prison mjini Mbeya.
Wagosi wametoka suluhu ya bila kufungana katika uwanja wa kumbukumbu ya Waziri Mkuu wa zamani Edward Moringe Sokoine mjini humo.
Itakumbukwa mechi ya ufunguzi mzunguko wa pili katika uwanja wa Mkwakwani Januari 25, Coastal Union walilazimishwa suluhu ya 1-1 na JKT Oljoro, baada siku nne baadae Januari 29 walitoka suluhu ya 0-0 na Yanga katika uwanja wa Mkwakwani.
Aidha mechi ya leo ilionekana kukaa vibaya kwa upande wa Wagosi kwani maafande wa magereza walionekana kupania kuondoka na point tatu muhimu katika uwanja wa nyumbani ambao waliugharamia kukukarabati mwezi uliopita.
Ilipofika dakika ya 29 kipindi cha kwanza, mashabiki wachache wa Wagosi, waliohudhuria kwenye mechi hiyo walipatwa na taharuki baada ya golikipa wao namba moja, Shaaban Kado kugaagaa chini baada ya kupata maumivu makali mchezo ukiendelea.
Mwamuzi wa leo alisimamisha mchezo kwa muda ili kutoa nafasi ya kugangwa kwa Kado, huku kocha Yusuf Chipo akitumia muda huo kuwaelekeza wachezaji wake kipi cha kufanya kuondokana na aibu hiyo ya suluhu.
Mpaka dakika 45 za awali zinatimia, ubao wa matokeo uliendelea kusomeka 0-0, hali iliyozidi kumtia hasira kocha Chipo ambae alizungumza maneno makali katika vyumba vya kupumzikia.
Mbali ya ukali huo lakini kipindi cha pili kilianza kwa kusuasua bila kuonyesha uhai wowote, mbaya zaidi timu ilikuwa ikishambuliwa sana hali iliyomfanya Chipo, kufanya mabadiliko kwa kumtoa Hamadi juma na kumuingiza Yusuf Chuma.
Baadae alitoka Jerry Santo na kuingizwa kijana mdogo Kipanga, halafu akatoka Abdi Banda akaingi Mohammed Miraji. Lakini bado hakuna kilichofanyika mpaka dakika tisini zinakamilika mbali ya Tanzania Prison kucheza pungufu baada ya mchezaji wao kuonyeshwa kadi nyekundu maada ya kucheza madhambi.
Kwa matokeo hayo Coastal Union imefikisha point 19 wakiendelea kung’ang’ania nafasi ya saba katika msimamo wa ligi huku wakiwa wamebakisha mechi kumi ambazo ni sawa na point 30 ikiwa watashinda zote.   
Baada ya mechi hiyo ya Mbeya, Wagosi watasafiri mpaka Tabora kumenyana na Rhino Rangers katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi siku ya Jumapili, Februari 9 mwaka huu.
Kikosi cha leo kilichoanza ni: Shaaban Kado, Hamadi Juma, Othman Tamim, Juma Nyoso, Mbwana Kibacha, Jerry Santo, Crispian Odula, Abdi banda, Kenneth Masumbuko, Danny Lyanga na Yayo Kato.
Wachezaji wa akiba walikuwa ni: Said Lubawa, Ayoub Semtawa, Yusuf Chuma, Kipanga, Mohammed Sudi na Suleiman Kassim ‘Selembe’.
Hizi ndizo mechi kumi zilizobaki kwa CUSC:
9 February (Tabora) Jumapili
Rhino Vs Coastal Union

15 February (Mlandizi) Jumamosi
Ruvu Shooting Vs Coastal Union

22 February (Tanga) Jumamosi
Coastal Union Vs Mbeya City

8 March (Tanga) Jumamosi
Coastal Union Vs Ashanti

12 March (Dar) Jumatano
Simba Vs Coastal Union

15 March (Dar) Jumamosi
Azam Vs Coastal Union

23 March (Morogoro) Jumapili
Mtibwa Vs Coastal Union

30 March (Tanga) Jumapili
Coastal Union Vs Mgambo

9 April (Tanga) Jumatano
Coastal Union Vs Jkt Ruvu

27 April (Tanga) Jumapili
Coastal Union Vs Kagera
COASTAL UNION
5 FEBRUARI, 2014



Sunday, February 2, 2014

Huu ndio msimamo wa Ligi ya Vodacom Tanzania Bara.




Rank
Team
Played
Won
Draw
Lost
Goal Diff
Points
1
AZAM FC
15
9
6
0
15
33
2
YANGA
15
9
5
1
20
32
3
MBEYA CITY
15
8
7
0
10
31
4
SIMBA SC
15
8
6
1
18
30
5
KAGERA SUGAR
15
5
6
4
3
21
6
MTIBWASUGAR
15
5
6
4
3
21
7
COASTAL UNION
15
3
9
3
3
18
8
RUVU SHOOTING
14
4
6
4
0
18
9
JKT RUVU
14
6
0
8
-5
18
10
RIHNO RANGER
15
2
6
7
-10
11
11
OLJORO JKT
15
2
5
8
-14
11
12
ASHANTI UTD
15
2
4
9
-15
10
13
T. PRINSONS
13
1
6
6
-10
9
14
MGAMBO JKT
15
2
3
10
-19
9