Wednesday, February 13, 2013

Yametimia Kagera Sugar 1- 0 Coastal Union, ligi kuu bara uwanja wa Kaitaba.

 Joseph Mahundi akikimbilia mpira huku mchezaji wa Kagera Sugar Julius Mrope akihakikisha Mahundi haupati.

 Golikipa wa Kagera Sugar Hannington Ralyesumbula, akidaka mpira huku Selembe akiwa chini.

 Mohammed Sudi wa Coastal Union akikwatuliwa na mchezaji wa Kagera sugar wakati akitaka kufunga.

 Mohammed Sudi akiambaa na mpira huku Selembe akimuhakikishia msaada.

 Ama kwa hakika leo Coastal Union walitepeta, hawakucheza mpira kabisaaaaaaaaa..

 Beki tatu wa Coastal Union Abdi Banda akiondoa hatari golini.

 Ibrahim Twaha 'Messi' akikokota mpira kuelekea langoni mwa Kagera sugar lakini hakuna kilichopatikana.

 Khamis Shengo alieingia kipindi cha pili akitafuta njia za kumtoka mchezaji wa Kagera Sugar Temi Felix ambae ndie alieipatia goli timu yake ila baadae alitoka nje kwa kadi nyekundu.

Jamani leo Sudi alikipiga vizuri sana maana alikuwa anaingia kila wakati....

Timu ya wagosi wa kaya kutoka Tanga leo waliendeleza uteja kwa timu za mkoa huo baada ya ndugu zao JKT Mgambo kufungwa goli moja kwa sifuri na Kagera Sugar wiki iliyopita kwenye uwanja huu huu wa Kaitaba mjini Bukoba.

dakika ya 58 kipindi cha pili mchezaji Felix Temi alietokea bench aliipatia goli la kuongoza timu yake kwa njia ya kichwa baada ya mabeki wa Coastal Union kujisahau na golikipa Shaaban Kado kuwategemea wao matokeo yake ikawa aibu kwa wagosi.

mpira wa leo uliandamwa na mazengwe ya kila namna hata kufikia refaree kutoa kadi mbili nyekundu moja kwa kila timu.

kadi ya kwanza ilikuwa ni njano mbili ambazo alipewa mfengaji pekee wa mchezo wa leo Felix Temi baada ya kuonyesha utovu wa nidhamu waku kujibishana na mwamuzi baada ya kukaa mbele ya mpiga mpira wa adhabu ndogo kinyume na taratibu.

kadi ya pili ilipatikana dakika ya 71 baada ya mchezaji wa Kagera Sugar Laban Kambole kumsukuma Gabriel Barbosa, lakini Barbosa alipoamua kujibu mashambulizi kwa kumsukuma mpaka kuanguka chini, mwamuzi wa pembeni alimwashiria mwamuzi wa kati ampe kadi nyekundu.

kitu hicho kiliamsha jazba uwanjani hasa ikizingatiwa Kagera Sugar walikuwa mbele kwa goli moja hivyo ilionekana ni hujuma dhidi ya Costal Union.

mechi nyingine zilizochezwa leo na matokeo yake ni: Yanga 4-0 African Lyon, Mgambo JKT 2- 0 JKT Oljoro, Mtibwa Sugar 0-0 Ruvu Shooting, Toto Africa 2-2 Polisi Morogoro.


 
 

Mechi inataka kuanza...


 Kikosi cha Kagera Sugar hiki kitakachovaana na Coastal Union leo katika uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba leo saa kumi na nusu jioni.
 
Hannington Ralyesumbula (GP).
Juma Nade                        
Salum Kanoni                   
Laban Kambole                    
Amandus Nesta                     
Malegesi Mwangwa                
Julius Mrope                            
Mecky Michael                           
Edmund Kashamila                      
Darlington Enyinna                      
Paul Ngwai                                    



 Kagera Sugar wakifanya mazoezi katika uwanja wa Kaitaba muda huu kabla ya mechi saa kumi na nusu alasiri.


 Coastal Union wakipasha misuli kabla ya mechi, umegundua kitu? Coastal wamevaa sox za African Sports, sababu kwenye pre match waliambiwa Kagera Sugar wanavaa sox nyekundu hivyo wao wabadili.


Sub ni:
Adam Oseja (GP)
Benjamin asukile    
Muganyizi Martin
Benjamin Effe
Temi Felix
Daudi jumanne
Wilfred Ammeh

Abdallah Kibaden (kocha)
Mrage Kabange    (kocha msaidizi)

Angalia list ya leo kikosi cha kwanza Kagera Sugar Vs Coatal Union.



Hiki ndicho kikosi cha kwanza cha Coastal Union kitakachokutana na Kagera Sugar leo kwenye uwanja wa Kaitaba; ligi kuu bara mzunguko wa pili.
 
Shaaban Kado, Ismail Suma, Abdi Banda, Philip Mugenzi, Mbwana Kibacha, Jerry Santo, Joseph Mahundi, Razak khalfan, Danny Lyanga, Mohammed Sudi na Suleiman Kassim ‘Selembe’.

Sub ni Rajabu Kaumbu (G), Hamad Juma, Gabriel Barbosa, Ibrahim Twaha ‘Messi’, Castro Mumbala, Gerald Lukindo ‘Sipi’, na Khamis Shengo.

wagosi wa kaya wanashuka dimbani wakiwa na point 27 nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi wenye timu 14.

Mechi nyingine za ligi kuu leo ni Toto Africa Vs Polisi Morogoro, Frican Lyon Vs Yanga, Mgambo JKT Vs JKT Oljoro, Mtibwa Sugar Vs Ruvu Shooting.

Msimamo kabla ya mechi za leo kuchezwa ni hivi:

Pos. Logo Club P W D L GF GA GD Pts
1 Young Africans FC Young Africans SC 15 10 3 2 28 12 16 33
2 Azam FC Azam FC 16 10 3 3 27 14 13 33
3 Simba SC Simba SC 16 7 7 2 25 14 11 28
4 Coastal Union SC 16 7 6 3 19 15 4 27
5 Ruvu Shooting Stars Ruvu Shooting Stars JKT 15 7 3 5 20 17 3 24
6 Kagera Sugar FC Kagera Sugar FC 16 6 6 4 17 15 2 24
7 Mtibwa Sugar FC Mtibwa Sugar FC 16 6 5 5 20 18 2 23
8 JKT Oljoro FC 16 5 6 5 19 18 1 21
9 Tanzania Prisons 15 4 6 5 10 12 -2 18
10 JKT Mgambo 16 5 3 8 11 16 -5 18
11 JKT Ruvu Stars JKT Ruvu Stars 15 4 4 7 14 22 -8 16
12 Toto African Toto African 17 2 7 8 13 24 -11 13
13 Polisi Moro 15 2 4 9 6 16 -10 10
14 African Lyon FC African Lyon FC 16 2 3 11 10 26 -16 9

Haya Coastal Mnataka nini tena. Hussein Chuse ananunua goli leo.

Hussein Chuse wa kwanza kutoka kulia mwenye miwani akiwa na mganga wa timu Eddy Shossi, Chuse leo ni siku yake ya kuzaliwa kwa kikoloni wanaita Birthday.

Ameiambia blog ya timu kuwa atanunua goli, kila mchezaji atakaefunga goli katika mechi ya leo dhidi ya Kagera Sugar itabidi akirudi Tanga amuone Chuse apewe mshiko wake. Ni hayo tu.

COASTAL UNION
KAGERA, TANZANIA
13 feb, 2013

Uwanja wa Kaitaba jamani ni mbovu balaaa... Haufai hauna hadhi ya kuchezewa ligi kuu. TFF waliangalie hili

 Angalia majukwaa haya, ati hili ndilo jukwaa kuu, si balaa hili. Maana mwanadamu ukiangalia mpira inabidi ukae na gogo aweza kutokezea nyoka pia.

 Bawazir huyu akiwa amefumba macho akiogopa kuumwa na nyoka. Maana nilimwambia kaa nikupige picha ili isiwe 'dead picture' naam kitaalam ukipiga picha bila kuwepo mtu inaitwa picha iliyokosa uhai. Lakini alikuwa akiogopa labda anaweza kuumwa na tandu.

 Hivi ni vyoo.. Ukitaka kuenda chooni mpaka mtu akusindikize unaweza kukutana na kenge bure.

 Jukwaa hili ndilo la wageni rasmi aka waheshimiwa, sasa ikiwa jukwaa la waheshimiwa lipo hivi huko kwengine kukoje?


Huu ni mlango wa upande wa kulia mwa uwanja, ni sehemu ya kukatishia tiketi angalia majani yalivyoota, hapo juu ya kibanda ukipanda maharage unavuna gunia zima.

Jamani eeeennnh kumbe mwenyekiti wa coastal Union mpira pia upo? Anaupiga balaaa... eeennhhh ingia ndani uone vitu vyake... Kaitaba hapo.








COASTAL UNION
13 FEB,2013

Tuesday, February 12, 2013

Tazama mazoezi ya timu leo asubuhi. Mwalimu anasema vijana wapo tayari kwa kutwaa point tatu muhimu kutoka kwa vibonde Kagera Sugar.

 Suleiman Kassim 'Selembe' akiingia uwanja wa Kaitaba Bukoba leo asubuhi kujifua na timu.

 Jana Sudi alimchana mwenzie Rajabu domo kwa mpira. Angalia alivyovimba maskini, ukimwambia aseme Pepsi anasema pepthiiii maskini wee domo noma.

 Mwalimu Morroco na Mwenyekiti wakiangalia vijana wakijifua..

 Gabriel Barbosa jana alikuwa akiumwa, kila akiulizwa analia anasema anataka akapimwe Malaria. Dr akamwambia huumwi ni uchovu tu akaambiwa siku ya jana alale tuu. Leo ameamka fiti na atapiga boli kama kawa.

 Mwalimu akiangalia wachezaji wakisprint, anasema hii inawasaidia kuondoa baridi na kuongeza nguvu za miguu.

 Morroco akisisitiza jambo kwa wachezaji, hawapo pichani.

 Jerry Santo akiongoza wenzie kufanya mazoezi ya kukaa na mpira muda mrefu au wakoloni wanaita ball contol. Mh jamani leo haponi mtu, vijana wana njaa ya ushindi balaa. Halafu naskia Binslum keshaweka mambo ubaoni. Mwachemwache hiyo... eeenhhhhh jogoo hana mtoto...

                                                                   Maaambooo hayoo...       
        
 Aurora ngado kwa ngado na wachezaji hataki mchezo.

                                           Sippi akinyoosha viungo wakati wa mazoezi.