Friday, April 26, 2013

Daniel Lyanga wa Coastal Union atimiza bao la saba katika msimu huu.

Daniel Lyanga wa Copastal Union (kulia) aikokota mpira mbele ya mchezaji wa Azam FC.

SULUHU ya bao moja kwa moja katika mechi ya soka ligi kuu Vodacom Tanzania bara leo kati ya Coastal Union na Azam FC uwanja wa mkwakwani Tanga imesadia timu ya Yanga kutangaza ubingwa wakiwa na mechi mbili mkononi.

Yanga ambao wana point 56 walikuwa wanataka point moja tu waweze kutangazwa mabingwa wa soka Tanzania bara lakini kwa Azam FC kutoa suluhu ya 1-1 na Coastal Union leo kumewafanya wana lambalamba hao kuvuna point moja hivyo kupata idadi ya point 48 kitu ambacho kwa mech mbili walizobakisha hawawezi kufikia pont 56 ambazo Yanga tayari wanazo na hakuna timu yoyote yenye uwezo wa kuzifikia.

Mchezaji wa wagosi wa kaya Daniel Lyanga aliyeingia kipindi cha pili kwa kuchukua nafasi ya Suleiman Kassim 'Selembe' ndiye aliyelazimisha suluhu hiyo mnamo dakika ya 71 ya mchezo ambayo ilikuwa ni dakika moja tu tangu aingie dakika ya 70 ambapo mpira wa kwanza kuugusa ikawa shangwe kwa mashabki wa Coastal na kutimiza goli la saba kwa msimu huu.

Awali mwamuzi wa leo aliipatia Azam penati mnamo dakika ya 58 ya mchezo iliyoingizwa kimiani na Aggrey Morris baada ya mchezaji wa wagosi Yusuph Chuma kucheza madhambi eneo la hatari.

Kutokana na matokeo hayo Coastal Union watakuwa na point 34 wakiendelea kujikita katika nafasi ya sita nyuma ya Mtibwa Sugar walio nafasi ya tano wakiwa na point 36 wakati huohuo timu ya wekundu wa msimbazi Simba wanashikilia nafasi ya nne wakiwa na point hizohizo 36 na Kagera Sugar yenye point 40 inashikilia nafasi ya tatu.

Hivyo ili Coastal Union wajiweke katika nafasi nzuri ni lazima washinde mechi zote mbili kati ya Yanga Mei 1 katika uwanja wa Taifa jijini na mechi dhidi ya Polisi Morogoro Mei 18 katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro. Kwani hizo point sita ukizidsha na point 34 itakuwa ni point 40 ambapo hata tukiwa nafasi ya nne si mbaya kikubwa ni kuwaombea mabaya Simba na Mtibwa Sugar katika mechi walizosalia nazo.

COASTAL UNION
costalunion@gmail.com
26 April, 2013
Dar es Salaam, Tanzania

No comments:

Post a Comment