Tuesday, April 23, 2013

Mchezaji wa Coastal Union Ibrahim Twaha 'Messi' aitwa timu ya Young Taifa Stars.

 Ibrahim Twaha (kulia) alipokuwa uwanja wa Manungu wakati Coastal Union ikipambana na Mtibwa Sugar.

Aliyempa jina la Messi hajakosea, mtoto huyu ana uwezo mkubwa wa kuondoka na kijiji na katibu tarafa wake.


Kocha wa Taifa Stars, Kim Poulsen ametangaza timu ya pili ya Taifa (Young Taifa Stars) atakayoitumia kuangalia wachezaji ambao baadaye anaweza kuwajumuisha kwenye timu ya wakubwa.

Akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam jumanne Aprili 23, Kim amesema timu hiyo ni sehemu ya mpango wa maendeleo wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) uliozinduliwa Aprili 4 mwaka huu ukilenga kuendeleza wachezaji.

“Huu ni mpango wa kuendeleza vipaji Tanania na timu hii inajumuisha wachezaji ambao wamepita umri wa kuchezea timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes) na wakubwa ambao hawajapata fursa ya kuingia Taifa Stars, lakini nitatumia Young Taifa Stars kuangalia uwezo wao.

“Timu hii ni kiungo kati ya vijana na wakubwa. Wengi wa wachezaji watakuwa vijana, lakini wakubwa wachache watapata fursa ya kuwemo ili kuangalia uwezo wao hata kama huko nyuma waliwahi kuchezea Taifa Stars. Lakini timu hii vilevile ni changamoto kwa wachezaji wa Taifa Stars kuwa wapo wanaosubiri wazembee ili wachukue nafasi zao,” amesema.

Young Taifa Stars yenye wachezaji 30 itakuwa na kambi ya siku tano jijini Dar es Salaam kuanzia Mei 2 hadi 6 mwaka huu.

Wachezaji walioitwa ni Aishi Manula (Azam), Hussein Shariff (Mtibwa Sugar) na Ali Mustapha (Yanga) ambao ni makipa. Mabeki ni Kessy Hassan (Mtibwa Sugar), Kennan Ngoma (Barnsley FC, Uingereza), Himid Mao (Azam), Ismail Gambo (Azam), David Mwantika (Azam), Miraji Adam (Simba), Mohamed Hussein (Kagera Sugar), Waziri Salum (Azam), Samih Nuhu (Azam) na Emily Mgeta (Simba).

Viungo ni Haruna Chanongo (Simba), Edward Christopher (Simba), Mudathiri Yahya (Azam), William Lucian (Simba), Jonas Mkude (Simba), Hassan Dilunga (Ruvu Shooting), Jimmy Shoji (JKT Ruvu), Abdallah Seseme (Simba), Ramadhan Singano (Simba), Farid Mussa (Azam) na Vicent Barnabas (Mtibwa Sugar).

Washambuliaji ni Hussein Javu (Mtibwa Sugar), Jerome Lambele (Ashanti United), Zahoro Pazi (JKT Ruvu), Twaha Hussein (Coastal Union), Abdallah Karihe (Azam) na Juma Luizio (Mtibwa Sugar).

Akizungumza na blog ya Coastal Union Ibrahim Twaha ‘Messi’ alisema anashukuru sana kuona juhudi zake zinatambuliwa na kocha Kim, kwani hakutegemea kabisa kuitwa katika kikosihicho cha wachezaji 30.

“Kwanza nimshukuru Mwenyezi Mungu kwa hatua niliyofikia, ni ndoto zangu za siku nyingi kucheza timu ya Taifa ya wakubwa, tayari nimeshachezea timu ya wadogo na sasa ni wakati wangu kuonyesha uwezo. Nitahakikisha nafanya vema na nitaingia rasmi timu ya wakubwa,” alisema Twaha.

Kutoka Coastal Union wawakilishi wa wachezaji chini ya umri wa miaka 20 walikuwa ni Ibrahim twaha na Ramadhan Shame ‘Batista’, lakini kwa bahati mbaya ‘Batista’ hajapata bahati ya kuingia kwenye kikosi hicho.

COASTAL UNION
APRILI 23, 2013
DAR ES SALAAM, TANZANIA
</

Mechi ya Coastal Union na Azam yarudishwa nyuma...



Shirikisho la soka Tanzania (TFF) limerudisha nyuma siku moja mechi kati ya Coastal Union na Azam iliyokuwa ichezwe jumamosi na sasa itachezwa ijumaa kwenye uwanja wa Mkwakwani Tanga.

Ofisa habari wa TFF, Boniface Wambura alisema awali mechi hiyo namba 168 ilikuwa ichezwe Aprili 27, lakini imerudishwa nyuma kwa siku moja ili kuipa nafasi Azam FC kujiandaa kwa mechi ya marudiano ya raundi ya pili ya kombe la shirikisho dhidi ya AS FAR Rabat ya Morocco itakayochezwa kati ya Mei 3, 4 au 5 nchini Morocco.

Katika mchezo huo wa ugenini Azam inahitaji ushindi wa aina yoyote au sare ya mabao kufuzu kwa hatua ya 16 bora katika michuano hiyo yenye heshima kubwa barani Afrika.

Katika hatua nyingine mechi ya pili ya Coastal Union itakayochezwa Mei 1, katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam dhidi ya Yanga, ndiwo mchezo utakaoamua hatma ya ubingwa wa Yanga kwa msimu huu baada ya kushinda mechi iliyopita dhidi ya JKT Ruvu na kujizolea point 56 hivyo kubakisha point moja tu kufikisha point 57 ambazo hakuna timu yoyote itakayoweza kufikisha point hizo.

Hivyo ili kulinda heshima ya timu kutogeuka daraja la kuwapa watu ubingwa lazima vijana wa Tanga kucheza mpira wa uhakika ili kuwanyamazisha Yanga kama walivyofanya Mgambo JKT kutoka Tanga wiki iliyopita uwanja wa Mwakwani.

Baada ya mchezo na Azam halafu Yanga, timu ya Coastal Union yenye point 33 katika nafasi ya sita itabakisha mchezo mmoja dhidi ya Polisi Morogoro utakaochezwa katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro mwezi wa tano.

COASTAL UNION
23 April, 2013

<

Thursday, April 18, 2013

Coastal Union kushuka dimbani kuumana na Azam FC Aprili 27 mwaa huu.



 Coastal Union itaikaribisha Azam kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga katika mechi itakayochezwa Aprili 27. Uwanja wa Taifa utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Simba na Polisi Morogoro itakayofanyika Aprili 28. mechi nyingine ya Coastal union tachezwa May 1, 2013 dhidi ya Yanga katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.


Yanga ambayo inafukuzia kwa karibu taji la Ligi Kuu ya Vodacom itapambana na JKT Ruvu katika mechi pekee ya ligi hiyo wikiendi hii itakayofanyika Jumapili (Aprili 21 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mbali ya mechi hiyo, nyingine zitakazochezwa mwezi huu ni kati ya African Lyon na JKT Ruvu itakayofanyika Aprili 24 kwenye Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam wakati Aprili 25 ni kati ya Ruvu Shooting na Simba kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

coastal union
Dar es Salaam, Tanzania
18 april, 2013



Tuesday, April 16, 2013

Sare ya bila kufungana kati ya Coastal Union na JKT Ruvu imeumiza wengi uwanja wa Mkwakwani leo.



Coastal Union ya Tanga imeshindwa kuutumia vema uwanja wake wa nyumbani Mkwakwani baada ya kulazimishwa sare ya bila kufungana na maafande wa JKT Ruvu kwenye ligi kuu ya sika ya Vodacom Tanzania bara.
 kikosi kilichocheza mechi ya leo ni kama kifuatacho:
1. SHABAN KADO
2. HAMADI JUMA
3. OTHMAN MANI
4. MBWANA KIBACHA
5. PHILLIP MUGENZI
6. RAZAKH KHALFAN
7. JOSEPH MAHUNDI
8. MOHAMED SOUD
9. PIUS KISAMBALE
10. SULEIMAN KASSIM SELEMBE
11. ATUPELE GREEN

Wachezaji wa akiba ni:

12. RAJABU KAUMBU (GK)
13. ISMAIL SUMA
14. ABDUL BANDA
15. DANNY LIANGA
16. MOHAMED HASSAN
17. SHAONGWE 
18. ALLY UFUDU

Kwa matokeo ya leo Coastal Union watakuwa wamejikusanyia point moja na kuendelea kubaki nafasi ya sita wakiwa na point 33.

kushindwa kungaa kwenye mechi ya leo imekuwa pigo sana kwa wagosi wa kaya kwani matarajio ya kumaliza nafasi nne za juu yanazidi kufutika kwani Kagera Sugar wenye point 37 na kushikilia nafasi ya tatu, Simba wanaoshika nafasi ya nne na Mtibwa Sugar wanaoshika nafasi ya tano wapo vizuri kushinda mechi walizobakisha hivyo kuna matumaini madogo kuwashusha.

COASTAL UNION
costalunion@gmail.com
16 April, 2013
Dar es Salaam, Tanzania

Saturday, April 13, 2013

Matatizo ya kiufundi yakwamisha Super Week. Maana yake Coastal Union watacheza mechi yao bila kurushwa LIVE na SuperSport.

Mechi tano kati ya sita za Super Week za Ligi Kuu ya Vodacom zilizokuwa zioneshwe moja kwa moja (live) na Kituo cha televisheni cha SuperSport cha Afrika Kusini sasa hazitaoneshwa kutokana na matatizo ya kiufundi.

Kwa mujibu wa Mtayarishaji Mtendaji (Executive Producer) wa SuperSport Kanda ya Afrika, Max Tshunungwa ambaye yuko nchini, wameshindwa kuonesha mechi hizo kutokana na matatizo ya kiufundi katika magari yao ya kurushia matangazo (OB van) yanayohudumia Afrika Mashariki- Kenya, Tanzania na Uganda.

Mechi hizo ni kati ya Azam na African Lyon, Yanga na Oljoro JKT, Azam na Simba, Coastal Union na JKT Ruvu na Mgambo Shooting na Yanga itakayochezwa Aprili 17 mwaka huu jijini Tanga.
Tatizo hilo pia limeathiri mechi za Ligi Kuu ya Kenya (KPL) ambazo hazitaonekana wikiendi hii. SuperSport ndiyo yenye haki za matangazo ya televisheni kwa ligi hiyo ya Kenya.

Tshunungwa amekutana na Sekretarieti ya TFF na Kamati ya Ligi kuelezea tatizo hilo. SuperSport kwa kushirikiana na Kamati ya Ligi na TFF watapanga mechi nyingine za Super Week kabla ya ligi kumalizika msimu huu.

Pia TFF, Kamati ya Ligi na SuperSport walikuwa na mkutano mfupi wa waandishi wa habari wakati wa mapumziko kwenye mechi ya leo kati ya Yanga na Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Taifa.


Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
13 April, 2013

Monday, April 8, 2013

Mechi ya Coastal Union na JKT Ruvu kuonyeshwa Live Super Sports.


MECHI SITA KUONEKANA SUPERSPORT ‘LIVE’ SUPER WEEK
Kituo cha televisheni cha SuperSport cha Afrika Kusini kitaonesha moja kwa moja mechi sita za Ligi Kuu ya Vodacom katika Super Week kati ya Aprili 11 na Mei 18 mwaka huu.

Mechi hizo ni kati Azam na African Lyon itakayochezwa Aprili 11 mwaka huu badala ya Aprili 10 mwaka huu kwenye Uwanja wa Azam Complex ulioko Chamazi, Dar es Salaam. Yanga na Oljoro JKT ambayo sasa itachezwa Aprili 13 mwaka huu badala ya Aprili 10 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Azam na Simba itakayochezwa Aprili 14 mwaka huu badala ya Aprili 13 mwaka huu Uwanja wa Taifa, na mechi kati ya Coastal Union na JKT Ruvu itakayochezwa Aprili 16 mwaka huu badala ya Aprili 10 mwaka huu.

Mechi nyingine ya Super Week itakayochezwa Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga ni kati ya Mgambo Shooting na Yanga itakayofanyika Aprili 17 mwaka huu badala ya Aprili 13 mwaka huu.

Pia mechi nyingine itakayooneshwa live na SuperSport ni kati ya Yanga na Simba itakayofanyika Mei 18 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kutokana na mechi za Super Week, mechi kati ya Mtibwa Sugar na Oljoro JKT iliyokuwa ichezwe Aprili 13 mwaka huu sasa itachezwa Aprili 17 mwaka huu Uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro.
 Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Aprili 8, 2013

Tuesday, April 2, 2013

TFF watambua mchango wa mchezaji wa zamani Coastalunion aliefariki juzi na kuzikwa jana Mkoani Tanga.


RAMBIRAMBI MSIBA WA BEHEWA SEMBWANA
Shrikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko kifo cha mchezaji wa zamani wa timu za Coastal Union, TPC na Taifa Stars, Behewa Ali Sembwana (72) kilichotokea jana usiku (Machi 31 mwaka huu) mkoani Tanga.

Msiba huo ni mkubwa kwa wadau wa mpira wa miguu kwani kwa nyakati tofauti Sembwana akiwa mchezaji, alitoa mchango mkubwa kwa timu mbalimbali alizochezea, hivyo mchango wake tutaukumbuka daima.

Sembwana aliyekuwa akicheza wingi ya kulia alidumu katika Taifa Stars kwa miaka kumi, kama ilivyokuwa kwa kombaini ya Mkoa wa Tanga (Tanga Stars) aliyoiwakilisha katika michuano ya Kombe la Taifa (Taifa Cup).

TFF inatoa pole kwa familia ya marehemu Sembwana, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Tanga (TRFA) na klabu ya Coastal Union na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito.

Maziko yamefanyika jana (Aprili 1 mwaka huu) kijijini kwake Lusanga, Wilaya ya Muheza mkoani Tanga. Mungu aiweke roho ya marehemu Sembwana mahali pema peponi. Amina
COASTAL UNION
costalunion@gmail.com
Dar es Salaam, Tanzania
2 April, 2013