Saturday, January 26, 2013

msimamo wa ligi baada ya mechi za leo ligi kuu mzunguko wa pili.


JKT Oljoro 3-1 Toto Africans
African Lyon 1-3 Simba 
Ruvu Shooting 1-0 Ruvu Stars 
Azam 3-1 Kagera Sugar 
Coastal Union 3-1 JKT Mgambo
Mtibwa 0-1 Polisi Morogoro

Habari picha, siweki maneno mengi picha zinajieleza...

 Wajeshijeshi walitutiiiisha kabla ya mechi kuanza... Angalia huyo kamanda alivyosimama wakati wa tizi.

 Jerry Santo akiwa na nahodha mwenzie wakati wa kuanza mechi hapa wanachagua timu gani ianze wapi.


                                                       Wandi kama kawaida na uhamasishaji..

                    Kama wewe kweli unawajua wachezaji wako unaweza kusema huyu ni nani?

                           aaaaaaa Asha Boko huyoooo.... Ambiwa hapa kuna shemeji yetu... Sitakiulizwa..


                                                             TD Bin Slum akiwa jukwaani.

                                Hawa ni maswahiba wakubwa majirani hawa Chuse na jirani yake Eddy.

 Viongozi wa Coastal hawa Aurora na Binslum, wakiwa na Chuse pamoja na Ubinde meneja huyu bila kumsahau kocha wa timu B Bakari Shime kwa jaaaam.

 Siagi Katibu wa Coastal huyu akiwa na viongozi wenzie makamu mwenyekiti Mnguto na kocha wa vijana Shime au kocha bora.


Tazama habari picha ushindi wa Coastal Union dhidi ya Mgambo JKT ligi kuu bara leo uwanja wa Mkwakwani.

                                         Jerry Santo na Selembe wakiwa wamewekwa mtu kati

                                                        Kikosi cha Mgambo hiki

                                                           Shango kwa jaaam akiminyana.

                                                        Ilikuwa kizaazaa kweli kweli.

 Kona hii ilizaa kona ya pili ambayo ndiyo ilifanya Philip akawainua mashabiki wa Coastal uwanja wa mkwakwani.

                                             Ally Kidi na Morroco wakitoa maelekezo.

                                       Huyu ndie Philip Mugenzi alieifungia Coastal goli la kwanza.

                                                           Kikosi cha Coastal Union hiki.


 Shaaban Kado mpaka mechi inakaribia kuanza kadi yake ilikuwa bado haijaidhinishwa na TFF mpaka mambo yalipowekwa sawa na Meneja Akida Machai.

                                  Tamim akimpongeza Danny baada ya kuweka wavuni bao la pili.

                                                    Benchi la Mgambo likiwa limevurugwa.

 Baada ya kuingia bao la tatu washabiki wa Coastal wakaanza kumwaga radhi. mmhhhhhh....

                                       Tamim akiambiwa na walimu wake umetufaahaaamm?

 Ushindi ilikuwa ni lazima tazama mwalimu Morroco alivyokasirika ingawa timu ilikuwa inaongoza.

                                  Morroco akizungumza na wanahabari baada ya mchezo kuisha.

 Kigoma hiki chini ya Miraji wandi na Nzori... Baadae si Nzori akasusa baada ya vuvuzela lake kuvunjwa? Wandi akataka kupigana na Nzori... mhhh..

                       Kampira kocha wa Mgambo akizungumza na wanahabari kiunyooongeee maskini.




Hapa maalim Unenge na Chuse wakimtuliza Nzori baada ya kukasirika kuona vuvuzela lake limevunjwa. Akaahidiwa atanunuliwa jipyaaa kutoka South Africa.



Na Mwandishi wetu
Leo katika uwanja wa mkwakwani vijana wa Coastal Union wamewaonea ndugu zao kutoka Handeni Tanga Mgambo JKT kwa kuwapigisha kwata ya mabao 3-1 huku mchezo ukiwa umetawaliwa kwa shangwe na umahiri wa kikosi cha kwanza cha Coastal Union.
Goli la kwanza la Coastal Union liliingizwa kimiani dakika ya 18 na Philip Mugenzi kwa njia ya kichwa baada ya kuunganisha mpira safi wa kona uliopigwa na Selembe.
Baada ya kipindi cha kwanza kuisha kwa Coastal Union Kuongoza goli moja, Mgambo walibadilika na kucheza mpira safi wa kuonana kiasi mashabiki wa Coastal walifungwa midomo kabla ya mshambuliaji hatari wa wagosi wa kaya Danny Lyanga mnamo dakika ya 77 ya mchezo kutumia vema makosa ya golikipa wa Mgambo Tonny Kavishe baada ya mpira kumponyoka na kutua miguuni mwa Danny akamramba chenga golikipa na kuutumbukiza mpira kwa kutumia guu lake la kushoto.
Hali ilizidi kuwa mbaya kwa upande wa Mgambo kwani mashambulizi ya kushtukiza kutoka kwa wagozi wa kaya yaliwazawadia bao la tatu lililofungwa na Mahundi mnamo dakika ya 80 baada ya kupokea pasi kutoka kwa Danny na kuutumbukiza mpira wavuni bila kutumia nguvu na kuwapa jeuri mashabiki wa Coastal Union kuimba ‘taaatu billaaa taaatuuu biillaaa’ huku wengine wakimwaga radhi uwanjani.
Lakini Peter Mwalianzi wa Mgambo aliharibu furaha ya wagosi wa kaya dakika tatu tu kabla ya mchezo kuisha baada ya kutumia vema makosa ya mabeki wa Coastal waliokuwa wameridhika na magoli matatu ambapo mpira ulimponyoka Othman Tamim na kufanya uvivu kugeuka hivyo ukawababatiza wachezaji wa Coastal waliokuwa ndani ya kumi na nane huku golikipa wa Coastal aliesajiliwa katika dirisha dogo kutoka Mtibwa Sugar alipokwenda kwa mkopo kutoka Yanga Shaaban Kado akiwa ametulia golini akisubiri nusura ya Mungu lakini Mwalianzi alinyoosha mguu wake na kuifuta machozi Mgambo JKT katika dakika ya 88 hivyo matokeo mpaka dakika 90 yakawa ni 3-1.
Kwa matokeo hayo Coastal Union imepata point tatu hivyo imefikisha point 25, na kushika nafasi ya nne katika msimamo ambapo nafasi ya kwanza inashikiliwa na Yanga, ya pili Simba, tatu ni Azam FC na nne ni Coastal Union Mtibwa Suga waliokuwa wakishikilia nafasi ya nne wameshuka nafasi moja chini baada ya jana kufungwa na Polisi morogoro katika uwanja wa manungu Turiani. Huu umekuwa mwanzo bora wa mzunguko wa pili wa ligi kuu bara kwa Wagosi wa kaya.
Kikosi cha Coastal Union ilikuwa ni: Shaaban Kado, Ismail Suma, Othman Tamim, Philipo Mugenzi, Mbwana Hamis, Hamis Shango, Joseph Mahundi, Mohammed Mtindi, Jerry Santo, Suleiman Selembe, Danny Lyanga. Baadae walitoka Selembe, Danny, Muddy Magoli kaingia Atupele, Twaha Messi  na Sudi. Na dakika ya 70 mchezaji Mohammed Sudi alipewa kadi ya njano baada ya kumchezea madhambi mchezaji wa Mgambo.
Kikosi cha Mgambo JKT ilikuwa ni: Tonny Kavishe, Salum Mlima, Yassin Awadh, Salum Kipanga, Bakari Mtama, Novat Lufunga, Chande Magoja, Peter Mwalyanzi, Issa Kanduru, Fully Maganga, Nassor Gumbo.
Coastal Union
Tanga, Tanzania
0713 593894

Tuesday, January 22, 2013

bao pekee la Coastal Union katika kombe la Mapinduzi Zanzibar lililofungwa na Jerry Santo laingia tano bora.

Nahodha wa Coastal Union Jerry Santo


Katika michuano ya kombe la Mapinduzi iliyokamilika tarehe 12 mwezi huu, kulipachikwa mabao 40. ktika mabao hayo kumechaguliwa mabao 5 ambayo yalionekana kungara kuliko yote.

Bao la kwanza ni la mchezaji wa Tusker Fc Khali Aucho, ambae alilifunga katika mechi dhidi ya Simba Sports Club. Zikiwa zimebaki dakika sita mpira kuenda mapumziko Aucho aliunganisha krosi ya Edwin Ombasa kwa kiki kali, nyavu za wekundu wa msimbazi zikatikisika.

Bao la pili kwa ubora ni la mchezaji wa Azam FC Jockins Atudo, katika mechi ya Azam dhidi ya Miembeni FC. Pia bao hili liliweka rekodi ya kuwa bao la mapema zaidi katika michuano hiyo ambapo alilifunga katika dakika ya kwanza ya mchezo kwa nia ya kichwa, Kumbuka Atudo pia ni Mkenya.

Bao la tatu liliingizwa kimiani na mchezaji Ally Mohammed ‘Gaucho’ wa Mtibwa Sugar kwa shuti kali eneo la penalt mpira ukajikunja mithili ya ndizi ukamuacha Juma Mpongo wa Coastal Union akishindwa kuminyana nayo.

Bao la nne kwa ubora kwenye michuano hiyo inayoadhimisha shererhe za mapinduzi ya Zanzibar mwaka 1964 liliingizwa kimiani na Kiggi Makasi wa Simba katika mechi yao dhidi ya Bandari kwa mpira wea adhabu ndogo ambao uliingia wavuni moja kwa moja bila ya kuguswa na mtu yeyote.

Goli hili hata mimi nasadikisha ni la uhakika na linafaa kuingia katika rekodi ya mabao mazuri, maana siku hiyo ya mechi nilikuwa sipigi picha nilikaa juu ya jukwaa kuu pembeni yangu alikuwepo kocha mkuu wa Mtibwa Sugar Mekky Mexime, ambapo tuikuwepo waandishi wengi tunapiga nae stori. Refa alipopiga filimbi kuashiria ni free kick na mpigaji akawa ni Kiggy Makasi, Mexime akasema hilo ni goli, na lisipoingia naondoka nakwenda kulala, sote tukabana pumzi kuona uchawi wa kocha Mexime, mara mpira huo wavuni huku golikipa akishangaa umempita vipi.

Jerry Santo nahodha wa Coastal Union ndie anakamilisha orodha hii ya wachezaji watano walioingiza kimiani mabao kwa ufundi katika mechi ya Coastal dhidi ya Mtibwa Sugar.
Santo ambae pia ni mkenya alipiga shuti la chini likaingia langoni mwa Mtibwa huku golikipa mahiri wa timu hiyo Hussein Shariff ‘Casillas’ akishangaa.

Kumbuka Coastal union katika michuano hiyo walishinda goli moja tu katika mechi tatu walizocheza na kufungwa goli moja tu.

Chanzo: Mwananchi tarehe 21 Januari, 2013 jumatatu. 

Sunday, January 20, 2013

Habari picha mechi ya leo Coastal Union Vs African Sports...

 Hiki ndicho kilichonifanya niamini timu ya African Sports walikuwa wanaendeshwa kwa nguvu za kiza. Maana timu yao iliingiza wachezaji watanowatano kila mlango, yaani upande wao wa Sports waliingia watano, Rasha wakaingia watano, jukwaa kuu wakaingia watano na hapa ni upande wa Coastal ati pia wameingia. Sijawahi kuona Sports wakatumia jukwaa la Coastal kuingia.

 Huyu ni meneja wa timu ndogo 'ubinde' akiwa na swahiba wake wa siku nyingi na shemeji yake kipenzi Eddy Shossi.

                                                               Barbosa on the move.

                                           Wachezaji wa Sports hawa wanazidi kujigawa.

                               Majembe ya timu B walio[anda timu kubwa Hamad kulia na Nzara....

                                                             Team Captain Jerry Santo


                                                         Haihitaji maelezo picha hii jamani au?

                                         Aurora akiwa wa mnazi wa African Sports Abdul Bosnia..

 Unajua hapa Bosnia na Aurora walikuwa wanabishana nini mbele ya marefa? Ati timu ziwe na sub ngapi nne au zaidi? Bosnia alikuwa anataka sub ziishie nne maana alikuwa anajua balaa la Coastal wana vikosi viwili na vyote moto.

 Nilisikitishwa na miundombinu mibovu ya uwanja, hapa ni baada ya mechi kuisha ati huo mpira ndiyo unamwagilia maji uwanja. Si maji yote yanatuama sehem moja na uwanja unaharibika kwa matope?

Hapa namuona meneja wa timu B 'Ubinde, akiwa na msaidizi wake Seif katikati na kocha Shime akiwa amekaa. Hawa ndiwo waioipeleka timu B afainali za Uhai Cup Dar es Salaam... taraaaa..

Coastal Union Vs African Sports hakuna mbabe uwanja wa Mkwakwani leo.

                                                 Kikosi cha kwanza cha Coastal Union leo.

                                     Kibacha kama kwaida yake hakutaka utani, Beki hasifiwi bwana.

                                                         Kikosi cha African Sports hiki

 Mishemishe langoni mwa African Sports lakini mishe zote hizi hazikuzaa matunda. Ati wameroga. ahaha

 Cha kufurahisha ni kuwa African Sports hawakuja na Daktari, Hivyo daktari wetu ndiyo akawa anawatibu wachezaji wao.



 Kocha wa African Sports John William 'Del Pioero' akiwapa maelekezo wachezaji wake baada ya kuona jahazi linaweza kuzama muda wowote.
Kama kawaida daktari wetu alikuwa akiwatibu wachezaji wao bila hiyana. Hapa golikipa wa African Sports aliumia.

Hemed Morroco kocha wa Coastal Union baada ya mechi kuisha akiwa haamini kilichotokea.
Morroco na Del Piero wakiwa wamekumbatiana kuonyesha fair play baada ya mchezo kuisha.


African sports wamerogaaaa African Sports wamerogaa African Sports wamerogaaa… hayo ndiyo maneno yaliyotapakaa kwa upande wa mashabiki wa Coastal Union baada ya dakika tisini kuisha kwa suluhu ya bila kufungana.
Jaramba la dakika ya 85 mpaka 90 lililokuwa likielekezwa langoni mwa African Sports ndilo lililowawacha midomo wazi mashabiki wa Coastal Union mpaka kuamini wapinzani wao wamekwenda kwa mganga ili wasifungwe.
Maana mnamo dakika ya 89 ya mchezo mshambuliaji wa coastal Unuon Danny Lyanga alipokea mpira akabaki yeye na nyavu hata goli kipa hakuwepo langoni lakini akapaisha. Kitendo kile kiligongolea msumari wa mwisho katika jeneza la lawama za kuwa wapinzani wa Coastal Union wameroga.
Kabla ya hapo dakika ya 35 kipindi cha kwanza mchezaji Mohammed Miraji au Muddy Magoli alipiga chenga safu yote ya ulinzi ya African Sports lakini alipotaka kufunga akautoa mpira nje mita chache.
Kiufupi kwa mchezo wa leo Coastal Union wanapasa kujilaumu maana wameshusha hadhi yao ya kushiriki ligi kuu maana wamechezewa mpira wa maudhi na timu iliyo ngazi ya mkoa TFF. Hivyo imeonyesha wazi wameshindwa kutamba mbele ya timu ndogo katika idadi ya timu za Tanzania bara.
Hata hivyo kilichokuwa kikichezwa leo siyo wachezaji, bali unazi wa timu mbili hizi za zamani katika ramani ya soka ya Tanzania bara.
Itakumbukwa Coastal Union na Aftrican Sports zilikuwa miongoni mwa timu tano za mwanzo ndizo kuanzisha michuano ya ligi kuu ya Tanganyika mwaka 1961.
Kikosi cha leo cha Coastal Union ni:
1.Rajab kaumbu
2.hamad hamis
3.abdi banda
4.nzara ndaro
5.bwana kibacha
6.castory mumbala
7.Lameck dayton
8.razak khalfan
9.mohamed
10.suleiman selembe
11.ibrahim twaha
Ambacho kilidumu mpaka mapumziko na wakaingia wachezaji Dani lyanga, mahundi, jerry santo,M ohammed Sudi na pius kasambale. WaKatoka Mohammed Miraji ‘mudi magoli’, Castro,Ibrahim Twaha ‘ messi’, Razack Khalfan na lameck Dayton.
Kikosi cha African Sports walikuwa ni:
1.Ramadhan Omary
2. Ayubu Masudi
3. Rashidi Hassan
4. Yusuph Kimanda
5. Saidi Abdallah
6. Shekuwe Salehe
7. Gidato Akunaay
8. Said Wambuje
9. Thabiti Mgoha
10. Ally Ndondo
11. Ramadhan Mwanzomgumu
Coastal Union
Tanga, Tanzania