Sunday, January 20, 2013

Coastal Union Vs African Sports hakuna mbabe uwanja wa Mkwakwani leo.

                                                 Kikosi cha kwanza cha Coastal Union leo.

                                     Kibacha kama kwaida yake hakutaka utani, Beki hasifiwi bwana.

                                                         Kikosi cha African Sports hiki

 Mishemishe langoni mwa African Sports lakini mishe zote hizi hazikuzaa matunda. Ati wameroga. ahaha

 Cha kufurahisha ni kuwa African Sports hawakuja na Daktari, Hivyo daktari wetu ndiyo akawa anawatibu wachezaji wao.



 Kocha wa African Sports John William 'Del Pioero' akiwapa maelekezo wachezaji wake baada ya kuona jahazi linaweza kuzama muda wowote.
Kama kawaida daktari wetu alikuwa akiwatibu wachezaji wao bila hiyana. Hapa golikipa wa African Sports aliumia.

Hemed Morroco kocha wa Coastal Union baada ya mechi kuisha akiwa haamini kilichotokea.
Morroco na Del Piero wakiwa wamekumbatiana kuonyesha fair play baada ya mchezo kuisha.


African sports wamerogaaaa African Sports wamerogaa African Sports wamerogaaa… hayo ndiyo maneno yaliyotapakaa kwa upande wa mashabiki wa Coastal Union baada ya dakika tisini kuisha kwa suluhu ya bila kufungana.
Jaramba la dakika ya 85 mpaka 90 lililokuwa likielekezwa langoni mwa African Sports ndilo lililowawacha midomo wazi mashabiki wa Coastal Union mpaka kuamini wapinzani wao wamekwenda kwa mganga ili wasifungwe.
Maana mnamo dakika ya 89 ya mchezo mshambuliaji wa coastal Unuon Danny Lyanga alipokea mpira akabaki yeye na nyavu hata goli kipa hakuwepo langoni lakini akapaisha. Kitendo kile kiligongolea msumari wa mwisho katika jeneza la lawama za kuwa wapinzani wa Coastal Union wameroga.
Kabla ya hapo dakika ya 35 kipindi cha kwanza mchezaji Mohammed Miraji au Muddy Magoli alipiga chenga safu yote ya ulinzi ya African Sports lakini alipotaka kufunga akautoa mpira nje mita chache.
Kiufupi kwa mchezo wa leo Coastal Union wanapasa kujilaumu maana wameshusha hadhi yao ya kushiriki ligi kuu maana wamechezewa mpira wa maudhi na timu iliyo ngazi ya mkoa TFF. Hivyo imeonyesha wazi wameshindwa kutamba mbele ya timu ndogo katika idadi ya timu za Tanzania bara.
Hata hivyo kilichokuwa kikichezwa leo siyo wachezaji, bali unazi wa timu mbili hizi za zamani katika ramani ya soka ya Tanzania bara.
Itakumbukwa Coastal Union na Aftrican Sports zilikuwa miongoni mwa timu tano za mwanzo ndizo kuanzisha michuano ya ligi kuu ya Tanganyika mwaka 1961.
Kikosi cha leo cha Coastal Union ni:
1.Rajab kaumbu
2.hamad hamis
3.abdi banda
4.nzara ndaro
5.bwana kibacha
6.castory mumbala
7.Lameck dayton
8.razak khalfan
9.mohamed
10.suleiman selembe
11.ibrahim twaha
Ambacho kilidumu mpaka mapumziko na wakaingia wachezaji Dani lyanga, mahundi, jerry santo,M ohammed Sudi na pius kasambale. WaKatoka Mohammed Miraji ‘mudi magoli’, Castro,Ibrahim Twaha ‘ messi’, Razack Khalfan na lameck Dayton.
Kikosi cha African Sports walikuwa ni:
1.Ramadhan Omary
2. Ayubu Masudi
3. Rashidi Hassan
4. Yusuph Kimanda
5. Saidi Abdallah
6. Shekuwe Salehe
7. Gidato Akunaay
8. Said Wambuje
9. Thabiti Mgoha
10. Ally Ndondo
11. Ramadhan Mwanzomgumu
Coastal Union
Tanga, Tanzania


No comments:

Post a Comment