Wednesday, January 2, 2013

Coastal Union kutua Zanzibar leo usiku.....

 Hawa ndiwo vijana wa Coastal B waliopandishwa timu kubwa... wawili kati ya hawa ndiwo watakuwa wanakwenda kupewa uzoefu ila watano tayari wanaandaliwa mikataba yao na jezi kuandikwa majina yao....

 Hapa namuona Kassim Suleiman 'Solembe' wa kwanza kushoto, Twaha Ibrahim 'Messi' katikati na Mansour Mansour nyanda la kutumainiwa timu B.... wakisoma gazeti la michezo kuangalia mzunguko wa kombe la mapinduzi.

alalaaaaaaa kumbe kidojembe nae alikuwepo? Hapa akiwa na Mansour na mtoto Messi... alipokwenda kuwaaga bandarini kuelekea Zanzibar.



Timu ya Coastal Union kutoka Tanga leo imewasili Dar es Salaam katika safari yao kuelekea Zanzibar tayari kwa michuano ya Mapinduzi inayoanza usiku wa leo baina ya Simba na Jamhhuri ya Pemba.

Akizungumza na coastalunion blog kocha mkuu wa Coastal Union Hemed Morroco amesema timu yake ipo vizuri na tayari kwa michuano kwani timu walizopangiwa nazo zote anazijua aina ya uchezaji wao.

Coastal ambayo imepangwa kundi B itacheza na Azam Fc kesho usiku halafu katika mechi nyingine za makundi itacheza na miembeni na Mtibwa Sukari ya Morogoro.

Hata hivyo midfield ya kutumainiwa Kassim Suleiman ‘Solembe’ kuna hatihati asicheze katika michuano hiyo kutokana na suala la kuchukua pesa za mshindi wa tatu michuano ya Challenge iliyofanyika Kampala Uganda mwishoni mwa mwaka jana.

Akizungumza na Coastal Union Blog Solembe alisema “Mimi sijui chochote lakini nina uhakika nitacheza, maana timu yangu ya Coastal haijapewa barua yoyote kuhusiana na sakata hilo.

“Kikubwa ninachoweza kusema ni kuwalaumu viongozi wa mpira wa miguu Zanzibar ZFA kwani hawajui wanachokifanya maana hata katika timu ya taifa Zanzibar mimi niliitwa tu hata timu yangu ya Coastal haikushirikishwa. Maana yake hata kama ningeumia basi timu yangu ndiyo ingewajibika kunitibu,” alisema Solembe.

Akithibitisha kutoshiriki Solembe kocha Hemed Morroco alisema “Kassim hawezi kucheza hawawezi kumruhusu wale watu maana bado wana hasira zao. Ila nakuthibitishia wapo vijana ambao watachukua nafasi yake na watacheza vizuri tu hakuna shaka,.”

Katika hatua nyingine Coastal imepandisha wachezaji watano kutoka timu B ambao ni golikipa Mansour, Ibrahim Shekue ‘Messi’, Mohammed Miraji ‘Muddy Magoli’, abdi Banda na Nzara.

“Leo wataondoka wachezaji saba wa timu B lakini ambao wamethibitishwa kupanda moja kwa moja ni watano ila hawa wawili mwalimu amesema anataka wapate uzoefu, sitokutajia kwa sasa ni siri ya mwalimu,” alisema mkurugenzi wa ufundi wa timu Nassor Binslum alipozungumza nab log hii leo.

Makamanda wa coastalunion blog kesho wataungana na timu ili kuwaletea matukio yote na picha za uhakika.

Dar es salaam, Tanzania
0713 593894/ 0752 593894



No comments:

Post a Comment