Saturday, January 19, 2013

Haya tupo live uwanja wa Mkwakwani AFC dhidi ya Coastal Union

                                                                       Coastal hawa...






Mwenyekiti Hemed Aurora nae yumo.


Mpongo, Suma, Tamim, Kibacha, Mugenzi, Mahundi, Santo, Selembe, Razak, Gabriel Barbosa, sudi.
Hicho ni Kikosi cha Coastal Union ambacho kinaongoza goli 1-0 dhidi ya AFC ya Arusha leo katika uwanja wa Mkwakwani ikiwa ni moja ya mechi za kujipima nguvu kabla ya kuanza mzunguko wa pili wa ligi kuu Tanzania bara.
Mechi ya ufunguzi watacheza na timu ya nyumbani Mgambo katika uwanja wa Mkwakwani mwishoni mwa mwezi huu.
Goli la kuongoza dhidi ya AFC limefungwa na Mahundi kwa njia ya kichwa dakika ya 25 ya mchezo halikupokelewa kwa furaha sana kwani mashabiki wa Coastal wanaichukulia mechi ya leo kama moja ya mazoezi ya kesho ambapo watakutana na wapinzani wao wa jadi wa muda mrefu African Sports ya Tanga ambao hawajakutana nao kwa zaidi ya miaka kumi na tano.
Coastal leo wamemchezesha mchezaji wao kutoka Brazil Gabriel Barbosa ambae anawapa burudani wapenzi wa Coastal kila anapogusa mpira.

Coastal Union
0713 593894
Tanga, Tanzania

No comments:

Post a Comment