Tuesday, January 22, 2013

bao pekee la Coastal Union katika kombe la Mapinduzi Zanzibar lililofungwa na Jerry Santo laingia tano bora.

Nahodha wa Coastal Union Jerry Santo


Katika michuano ya kombe la Mapinduzi iliyokamilika tarehe 12 mwezi huu, kulipachikwa mabao 40. ktika mabao hayo kumechaguliwa mabao 5 ambayo yalionekana kungara kuliko yote.

Bao la kwanza ni la mchezaji wa Tusker Fc Khali Aucho, ambae alilifunga katika mechi dhidi ya Simba Sports Club. Zikiwa zimebaki dakika sita mpira kuenda mapumziko Aucho aliunganisha krosi ya Edwin Ombasa kwa kiki kali, nyavu za wekundu wa msimbazi zikatikisika.

Bao la pili kwa ubora ni la mchezaji wa Azam FC Jockins Atudo, katika mechi ya Azam dhidi ya Miembeni FC. Pia bao hili liliweka rekodi ya kuwa bao la mapema zaidi katika michuano hiyo ambapo alilifunga katika dakika ya kwanza ya mchezo kwa nia ya kichwa, Kumbuka Atudo pia ni Mkenya.

Bao la tatu liliingizwa kimiani na mchezaji Ally Mohammed ‘Gaucho’ wa Mtibwa Sugar kwa shuti kali eneo la penalt mpira ukajikunja mithili ya ndizi ukamuacha Juma Mpongo wa Coastal Union akishindwa kuminyana nayo.

Bao la nne kwa ubora kwenye michuano hiyo inayoadhimisha shererhe za mapinduzi ya Zanzibar mwaka 1964 liliingizwa kimiani na Kiggi Makasi wa Simba katika mechi yao dhidi ya Bandari kwa mpira wea adhabu ndogo ambao uliingia wavuni moja kwa moja bila ya kuguswa na mtu yeyote.

Goli hili hata mimi nasadikisha ni la uhakika na linafaa kuingia katika rekodi ya mabao mazuri, maana siku hiyo ya mechi nilikuwa sipigi picha nilikaa juu ya jukwaa kuu pembeni yangu alikuwepo kocha mkuu wa Mtibwa Sugar Mekky Mexime, ambapo tuikuwepo waandishi wengi tunapiga nae stori. Refa alipopiga filimbi kuashiria ni free kick na mpigaji akawa ni Kiggy Makasi, Mexime akasema hilo ni goli, na lisipoingia naondoka nakwenda kulala, sote tukabana pumzi kuona uchawi wa kocha Mexime, mara mpira huo wavuni huku golikipa akishangaa umempita vipi.

Jerry Santo nahodha wa Coastal Union ndie anakamilisha orodha hii ya wachezaji watano walioingiza kimiani mabao kwa ufundi katika mechi ya Coastal dhidi ya Mtibwa Sugar.
Santo ambae pia ni mkenya alipiga shuti la chini likaingia langoni mwa Mtibwa huku golikipa mahiri wa timu hiyo Hussein Shariff ‘Casillas’ akishangaa.

Kumbuka Coastal union katika michuano hiyo walishinda goli moja tu katika mechi tatu walizocheza na kufungwa goli moja tu.

Chanzo: Mwananchi tarehe 21 Januari, 2013 jumatatu. 

No comments:

Post a Comment