Friday, January 11, 2013

Unadhani una kijana ambae anaweza kucheza soka la ushindani? Soma hii...

kutoka kulia upande wa nyuma ni Mohammed Miraji, Hussein Twaha 'Messi', Abdi Banda, Hamad Juma, Ally Nassor 'Ufudu', waliochuchumaa mbele ni Mansour Mansour na Ramadhan shame Batista. Hapa amepungua Nzara Ndaro hayupo pichani.

Na Mwandishi wetu
Uongozi wa timu ya Coastal Union B imefungua milango kwa vijana wanaotaka kujiunga na timu hiyo ya vijana chini ya miaka 20 kujitokeza ili kufanyiwa majaribio.

Akitoa taarifa hizo meneja wa timu ndogo Abdulrahman Mwinjuma ‘Ubinde’ mjini Tanga leo amesema kwakuwa timu ya Coastal Union B ilionyesha mafanikio makubwa katika michuano ya Uhai mwishoni mwa mwaka jana kwa kumaliza nafasi ya pili hivyo wachezaji wanane wamepata nafasi katika kikosi cha timu kubwa.

“Mazoezi yanaanza siku ya jumatatu asubuhi tarehe 14 Januari mwaka huu katika uwanja wa Gymkhana mjini hapa (Tanga), chini ya kocha wake mkuu Bakari Shime ambae pia alichaguliwa kuwa kocha mkuu katika michuano ya Uhai.

“Timu ina upungufu wa wachezaji wanane ambao walipandishwa kikosi kikubwa kinachojiandaa na mzunguko wa pili wa ligi kuu Tanzania bara, kijana yeyote ambae ana umri chini ya miaka 20 akitaka kufanyiwa majaribio awasiliane na mimi kwa namba (0654851612) ama aje katika klabu ya timu iliyo barabara ya 11 Tanga,” alisema Ubinde.

Wachezaji wanane ambao walipanda timu kubwa ambayo wiki iliyopita ilikuwa Zanzibar kushiriki michuano ya kombe la Mapinduzi na kutolewa katika hatua ya makundi ingawa haikupoteza mchezo hata mmoja ni;

Aliekuwa golikipa bora wa michuano ya Uhai Mansour Mansour, Abdi Banda, Ally Nassor, Hussein Twaha ‘messi’, Hamad juma, Nzara Ndaro, Mohammed Miraji ‘Muddy Magoli’ na Ramadhan Shame ‘Batista’.

No comments:

Post a Comment