Tuesday, January 1, 2013

Haya wadau karibuni Coastal Union Official blog...

 mashabiki wa Coastal Union wakiwa wamechanganyikiwa kwa furaha katika uwanja wa nyumbani Mkwakwani mjini tanga..... kigoma hiki hata Simba na Yanga wanakitamani.

                              Huyu ndie manyota mwenyewe Rais wa Coastal Hemed Hilal 'Aurora'


Hii ilikuwa fainali ya Coastal B uwanja wa Karume Coastal Vs Azam Fc kwa jaaam namuona mwenyekiti Aurora na mchezaji wa zamani wa Coastal Yanga Bwanga alievaa miwani.


Ndugu zangu,

Sasa dunia inaendeshwa kwa kutumia mitandao, kuna propaganda nyingi katika kila kitu kuanzia michezo, siasa na burudani.

Kwa kuzingatia hayo timu ya Coastal Union ‘wagosi wa kaya’ imeona haja ya kutengeneza blogu ambayo itaweza kukupa habari zote zinazohusiana na klabu. Kadhalika tutakuwa tunatoa picha za michezo wanayoshiriki kuanzia ngazi ya taifa na kimataifa lengo likiwa ni kukuleta karibu na timu yako.

Kwa msaada mdogo ambao blogu hii itakuwa inaupata kutoka kwa wadhamini wanaoitakia mema timu hii, blogu itakuwa inakwenda ama inaifuata timu kila inapokwenda.

Hasa ikizingatiwa katika michuano ya mpira wa miguu Tanzania bara timu inahitaji kusafiri katika baadhi ya mikoa hivyo blogu itahakikisha inafika kwa lengo la kupata kile kinachojiri.

Aidha blogu hii itakuwa suluhisho la kiu yako kuhusiana na baadhi ya taarifa zinazohusu wachezaji, mathalan umri, nafasi wanazocheza, historia fupi ya mchezaji na mambo mengine yanayowahusu.

Kadhalika blogu itajitahidi kupata historia ya klabu tangu kuanzishwa, itahakikisha inauliza wazee wa mjini Tanga ambao ima walisikia ama kuona harakati za timu hii ikianzishwa na ni kina nani waliamua kufanya kitendo hicho cha kishujaa kuanzisha timu mahiri kama Coastal Union.

Mafanikio ya timu pia kitakuwa kitu muhimu, tutajua kikosi kilichoipeleka timu Dar es Salaam kuchukua kikombe cha ligi kuu soka Tanzania bara mwaka 1988, baadae timu ikaenda Kenya katika Challenge Cup na kushika nafasi ya pili, yote hayo tutahakikisha tunaangazia kwa mapana yake.

Lengo la kufanya hivi ni kuwapa mwanga vijana wapya ambao wana mapenzi na timu lakini hawaijui Coastal Union ni timu ya aina gani. Wapo watu ambao wanaanza kushabikia mpira wa miguu miaka ya 2000 lakini wanaposikia jina la Coastal Union wanadhani ni timu mpya.

Lakini ukikutana na watu wanaojua historia ya soka Tanzania watakuambia Coastal ni timu ya aina gani.

Hivyo karibuni katika blogu hii na hakika hutovunjika moyo kwa kuitembelea kila siku maana timu yetu ya Costalunionblogspot itahakikisha inatoa kitu kipya kila siku kwa lengo la kuelimisha na kushawishi mashabiki wapya wanaopenda kujiunga na timu hii.

DAR ES SALAAM, TANZANIA
1/1/2013

3 comments: