Thursday, January 10, 2013

Dharau za Simba zawatoa katika michuano ya Mapinduzi....


 Azam wakishangilia baada ya kuwarambisha ice cream Simba watoto... jana usiku kwa mikwaju ya penalt 5-4.

 David Mwantika wa Azam akiminyana na Mkipalamoto (huyu kijana alishiriki Uhai Cup akawa mfungaji bora) sasa amepandishwa Simba kubwa.

Uhuru Suleiman kulia na Ibrahim Mwaipopo kushoto wakimdhibiti Ibrahim Singano 'Messi' nae alipanda kutoka Simba B iliyoshiriki Uhai Cup. Huku kocha msaidizi wa Simba Jamhuri Kihwelu 'Julio' akitazama kwa majonzi namna jahazi linavyosama kutokana na dharau ya viongozi wake kuipeleka timu Oman wakati michuano haijaisha.

Simba walitolewa kwa mikwaju ya penalt baada ya dakika 120 kuisha 2-2... kwa hivyo Azam wanasubiri mshindi wa leo usiku kati ya Miembeni na Tusker ili kuweza kujua siku ya tarehe 12 januari nani na nani watacheza nao katika fainali.

Azam ndiwo mabingwa watetezi wa kombe hili linalofanyika kila mwaka mwezi januari kuadhimisha mapinduzi matakatifu ya mwaka 1964.

Coastal Union ya Tanga ambayo ilitolewa katika hatua ya makundi bila kufungwa mechi hata moja, ilipata suluhu tatu mbili za bila magoli na moja ya goli 1-1 dhidi ya Mtibwa Sugar. Coastal Union ilishiriki michuano ya Mapinduzi kwa mara ya mwisho mwaka 1988 ambapo African Sports ya Tanga walikuwa washindi.

No comments:

Post a Comment