Thursday, January 3, 2013

Jamani le Juma Mpongo katusaidia si haba......


Kocha wa Coastal Union Hemed Morroco amedhirisha usemi wake kuwa hakuna sababu ya kushindwa game ya leo, maana anaamini Azam hawana mpira wa kuwafunga baada ya kutoka suluhu ya bila kufungana na Azam.

Mechi ya pili ya kundi B iliyokutanisha Coastal kutoka Tanga na Azam kutoka Dar es Salaam katika kombe la mapinduzi imeisha bila kufungana tofauti na mechi ya awali ya kundi hilo iliyochezwa leo alasiri kati ya Miembeni na Mtibwa Sugar ambapo Mtibwa walichabangwa mabao 4 kwa ubuyu (4-0).

“mpaka sasa sijui kwanini wale jamaa walitufunga katika ligi kuu mzunguko wa kwanza, wabovu sana hawana mpira wa kutisha, huoni hata mgambo waliwafunga mkwakwani. Naamini tumecheza vizuri ila kuna matatizo kidogo katika safu yangu ya umaliziaji tumekosa magoli ya wazi sana yapo marekebisho tutayafanya tumeanza vizuri na tutamaliza vizuri watu wa tanga wasubiri tunakuja na mwari nyumbani,” alisema kocha mkuu wa Coastal Hemed Morroco.

Awali kabla ya mchezo blog hii ilipewa taarifa na kocha kuwa Solembe amekubaliwa kucheza na ataanza katika mchezo wa leo..

Coastal leo saa mbili usiku walishuka dimbani na Azam katika mechi yao ya kwanza ya kundi B mapinduzi cup. Kikosi cha coastal ni kama ifuatavyo:

Namba Juma mpongo,  mbili Ismail Suma, tatu Othman Tamim, nne Kibacha Bakari, tano Philip Mugenzi, sita Shengo Ally, saba Suleima Kassim ‘Solembe,’nane Jerry Santo tisa Mohammed Miraji kumi Mohammed Sudi  kumi na moja Daniel Lyaga.

Wachezaji wa akiba ni Rajab Kaumbu, Hamad Hamis, Abdi Banda, Lukindo Gerrard, Razak Khalfan,  Maundi petro na Hussein Ibrahim ‘messi’.
Leo Coastal walicheza soka la kuvutia ingawa walikosa magoli mengi hasa katika dakika ya 41 kipindi cha kwanza pale Mohammed Miraji alipomimina krosi nzuri ila ikamkuta Selembe amejisahau huku akiwa yeye na kipa tu mpira ukampita.

Hata hivyo kocha mkuu wa Azam FC Stuwart Hart alikiri kwamba Selembe ni mchezaji wa kiwango cha juu na haamini kama mchezo huo uliisha bila kufungana kwani Coastal walistahili ushindi.

Katika kipindi cha pili alitoka Selembe akaingia Hussein Ibrahim, pia akatoka akaingia Lukindo Gerald

Unguja, Zanzibar
0713 593894
3/1/2013

No comments:

Post a Comment