Saturday, January 5, 2013

Mechi ya leo Coastal Vs Mtibwa sukari.... iliisha kwa mabao 1-1.. tazama picha ndani.

 Kocha Hemed Morroco kushoto akiwa na swahiba wake katikati pamoja na daktari wa timu kulia...


                         Makky Maxime wa kwanza kulia kocha wa mtibwa Sukari akiongoza benchi lao...

 Hawa ni wazee wa fitna, wanakwenda na timu kila mahali mzee ally mwenye kofia pamoja na mchezaji wa zamani wa Coastal na timu ya Taifa Salim Amiri. wakiangalia pambano waliloliita gumu kati ya Coastal na Mtibwa leo uwanja wa Amaan.

 Kikosi cha Coastal Union kilichoivaa Mtibwa leo kikiongozwa na nahodha toka Kenya Jerry Santo alieiokoa timu yake kwa aibu leo baada ya kusawazisha bao dakika ya 81 ya mchezo.


                                                          Kikosi cha Mtibwa sukari hiki...


 Jerry Santo ninamkubali kitu kimoja, ana nidhamu ya hali ya juu. na muda wowote anafanya mambo yake kwa kujali muda. hapa wakimsubiri nahodha wa Mtibwa ili kuja kuzungumza na waamuzi. Hata katika kulala, kuamka, kwenda kula na mazoezini, kupanda bus wakati wa kuenda kwenye mechi yeye huwa wa kwanza kufika ingawa ni kiongozi.




 Eddy Shossi ndani ya nyumba akizungumza na kijana wake Mansour golikipa namba moja wa Coastal B. Panga pangua..

Othaman Tamim...naba tatu ya ukweli hii Coastal... hana kawaida ya kuchekacheka na maadui... akiwa uwanjani.
Kumbe uwanja wa Amaan ulifunguliwa na Nyerere mwaka  1970?

No comments:

Post a Comment