Thursday, January 23, 2014

A to Z picha za safari ya leo kutoka Oman.

 Jana kulikuwa na kikao cha kujadiloi mustakabali wa timu, baada ya kambi hapa tulikuwa tunafanya majumuisho. Ofisa wa Ubalozi Mussa Abdallah aliwauliza wachezaji waseme kinachowasibu ili wakishindwa wasiwe na sababu.

 Ofisa Ubalozi wa Tanzania nchini Oman, Mussa Abdallah (kushoto), akiwa na Mwenyekiti wa Coastal Union Hemed Hilal 'Aurora' katika kikao hicho cha majumuisho ya kambi ya wiki mbili nchini Oman.

 Mussa Abdallah, Hemedd Hilal wakiwa na Meneja wa Coastal Union, Akida Machai (wa tatu kutoka kushoto) katika kikao hicho jana adhuhuri katika hoteli ya Taj Mahal jijini muscat.

 Haruna Moshi 'Boban' akichangia mada katika kikao cha majumuisho ya kambi ya wiki mbili nchini Oman.

 Nahodha wa Coastal Union, Juma Said 'Nyoso' akichangia mada katika mkutano huo uliofanyika jana.

 Meneja Akida Machai, nae alitoa lake la moyoni.

 Mwenyeji wetu ambae alikuwa daktari wa timu ya Fanja SC na timu ya taifa ya Oman, Dk. Majid akichangia mada katika mkutano huo jana.

Suleiman Kassim 'Selembe' na Yayo Kato wakiwa uwanja wa ndege wa Sultan Qaboos jijini Muscat Oman, leo asubuhi kabla ya kupaa kurejea nyumbani tayari kwa mechi dhdi ya JKT Oljoro jijini Tanga siku ya Jumamosi Januari 25.
 Viongozi wa Ubalozi, na viongozi wa Fanja SC wakipata picha ya kumbukumbu na viongozi wa Coastal Union na wachezaji katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Sultan Qaboos Jijini Muscat Oman leo asubuhi.

 Msemaji wa Coastal Union Hafidh Kido (wa kwanza kulia) akiwa na golikipa wa Coastal Union Said Lubawa (katikati) na kocha msaidizi Ally Jangalu kabla ya kuruka na ndege ya shirika la Oman Air kurudi Tanzania leo asubuhi.

 Baada ya kutua Makamu Mwenyekiti Steven Mnguto (wa kwanza kulia), Meneja wa timu ndogo Abdulrahman Ubinde, Meneja msaidizi timu kubwa Abdi Masamaki na daktari wa timu Mzee Mganga katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa JK.

 Shabiki wa Coatal Union, Omar (kushoto) akiwa na Allya Nassor 'Ufudu', Yusuf Chuma na Mbwana Hamis 'Kibacha' katika uwanja wa ndege wa JK Nyerere.

 MzeeMnguto na Masamaki wakihakikisha mizigo yote inapatikana...

 Baada ya kutua vijana waligonga chakula halafu wakaanza safari kuelekea kambini jijini Tanga.

Hii ndiyo mitaa ya Mawaleh, mitaa ambayo vijana wa Coastal Union walijidai kwa wiki mbili jijini Muscat.

COASTAL UNION
23 JANUARI, 2014
DAR ES SALAAM, TANZANIA

Saturday, January 18, 2014

Dhifa ya chakula cha usiku iliyoandaliwa na kaimu Balozi nchini Oman.





 Mwenyekiti na kaimu balozi Abdallah Kilindi wakitafakari.


 Kocha wa timu ya taifa ya ufukweni Oman, Twalib Hilal akikabidhi jezi za wacezaji wa U20 Coastal Union, kwa mwenyekiti wa Coastal.

 Ofisa wa ubalozi ndugu Mussa akimkabidhi ngao ya kumbukumbu kwa mwenyekiti wa klabu ya Coastal Union, Hemed Aurora.

 Mwenyekiti wa Fanja SC, Seif El Sumry akizungumza mawili matatu katika dhifa ya leo.

 Mwenyekiti wa Coastal Union akiweka chakula.

 Kutoka kushoto kaimu balozi wa Tanzania nchini Oman, Abdallah kilindi na mwenyekiti wa Fanja SC, Seif El Sumri wakijiwekea chakula leo usiku.

 Dokta Francis Mganga, akiitendea haki dhifa ya leo.

 Nahodha msaidizi wa Coastal Union, akitoa maneno ya shukurani kwa viongozi wa ubalozi na Fanja Sc, kutokana na kufanikisha ziara yetu nchini hapa.

Viongozi wa ubalozi, viongozi wa Fanja SC wakiwa katika picha ya pamoja na mwenyekiti wa Coastal Union, Hemed Hilal 'Aurora', baada ya dhifa ya kuagana leo.

COASTAL UNION
JANUARI, 2014
MUSCAT, OMAN

Seeb Club 0-0 Coastal Union uwanja wa Seeb Club.






Coastal Union ‘Wagosi wa Kaya’, leo wametoka suluhu tasa dhidi ya Seeb SC inayoshiriki ligi kuu ya Oman.
Mechi ya leo ambayo ni ya kirafiki imeisha kwa matokeo ya 0-0 ambayo inakuwa mechi ya nne tangu kuwasili nchini hapa Januari 9, kwa ziara ya wiki mbili kujiandaa na ligi mzunguko wa pili Tanzania Bara.
Coastal Union, imeonyesha uhai katika kipindi cha pili ambapo kipindi cha kwanza walishindwa kuonyesha makeke yao baada ya wachezaji wa Seeb, kujazana katikati hali iliyowafanya Wagosi kushindwa kumiliki mpira.
Aidha, golikipa wa Wagosi, Shaaban Kado alipoiona kasoro hiyo akawa anatumia muda mwingi kupiga mipira katikati kila inapomjia kwa lengo la kuamsha mashambulizi ili viungo wake wachangamke.
Kipindi cha kwanza kiliisha timu zote kizitoka vichwa chini kutokana na kukosa nafasi za kuonyeshana uwezo waliofundishwa na walimu wao.
Kipindi cha pili Seeb Club, walifanya mabadiliko kwa kutoa wachezaji wawili wa ndani na mlinda mlango. Coastal Union waliendelea kucheza bila kufanya mabadiliko.
Katika dakika za awali kipindi cha pili Seeb walionyesha uhai na kulisumbua sana lango la Wagosi, lakini kufuli za Juma Nyoso na Othman Tamim ziliendelea kuwa imara kuulinda mlango wa Shaaban Kado.
Aidha ilipofika dakika ya 76, kocha Yusuf Chipo alifanya mabadiliko ya haraka haraka kwa kutoa wachezaji wane na kuingiza wane ndani ya dakika 15 zilizosalia.
Alianza kutoka Othman Tamim akaingia Abdi Banda, baadae akatoka Danny Lyanga akaingia Mohammed Miraji. Halafu zikiwa zimesalia dakika chache mchezo kuisha alitoka Atupele Green akaingia Suleiman Kassim Selembe, halafu akamalizia mabadiliko kwa kumuingiza Abdullah Othman ‘Ustadh’ akatoka Yayo Kato.
Listi ya leo ilikuwa: Shaaban Kado, Hamadi Juma, Othman Tamim, Juma Said ‘Nyoso’, Mbwana Kibacha, Jerry Santo, Ally Nassor ‘Ufudu’, Danny Lyanga, Atupele Green, Haruna Moshi ‘Boban’, na Yayo Kato.
Coastal Union tangu iwasili Oman imeshacheza mechi nne, imeshinda mechi mbili kati ya Oman Club na Al Mussannah kwa mabao 2-0 kila mechi. Halafu ikafungwa bao 1-0 na Fanja Club, leo imetoka suluhu ya bila kufungana na Seeb Club.
COASTAL UNION
18 JANUARI, 2014
MUSCAT, OMAN

Mechi ya leo Seeb Club Vs Coastal Union



COASTA Union Wagosi wa Kaya, Wagosi wa Ndima, leo watashuka dimbani dhidi ya timu ngumu inayoshika nafasi ya nne katika ligi kuu ya Oman, Seeb Club.
Seeb SC, ambao wamecheza mechi 12 wameshinda mechi sita kutoa suluhu tano na kupoteza mchezo mmoja hivyo kuambulia point 23, wakiwa wamepishana point mbili na timu inayoongoza ligi, Al Nahda Club ambayo ina point 25 ikiwa imecheza michezo 12, kushinda minane, kupoteza mitatu na kutoa suluhu moja.
Aidha katika mechi ya leo Wagosi watahakikisha wanacheza kwa umakini ili kuondoka na jina zuri nchini Oman, ambapo mpaka sasa klabu nyingi zinatuma maombi ya kutaka kucheza na Wagosi baada ya kupata taarifa ya ushindi wa mfululizo katika mechi mbili za awali dhidi ya Al Mussannah inayoshika nafasi ya saba katika ligi kuu na Oman Club iliyo daraja la kwanza.
Mechi ya leo itachezwa saa kumi alasiri katika uwanja wa Seeb Club, jijini Muscat ingawa mratibu wa mechi za Coastal Union nchini hapa Twalib Hilal, ametoa maelezo kuwa kutakuwepo na mechi ya tano kabla ya kuondoka Januari 23, kujiandaa na mechi ya ufunguzi mzunguko wa pili dhidi ya JKT Oljoro katika uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga.
Itakumbukwa Coastal Union tangu iwasili nchini Oman, januari 9 mwaka huu kwa ziara ya wiki mbili, imeshacheza mechi tatu dhidi ya Al Mussannah Club, Oman Club na Fanja SC. Ambapo wameshinda mechi mbili kwa mabao 2-0 kila mechi na kupoteza mchezo mmoja dhidi ya Fanja SC kwa bao 1-0.
Kwa mujibu wa kocha mkuu wa Coastal Union, Yusuf Chipo timu yake imepata mambo mengi ambayo yamemsaidia katika mafunzo yake.
“Mbali ya utulivu kwa wachezaji lakini nimejifunza mambo mengi kutoka klabu za hapa, kuanzia ubora wa viwanja, serikali inavyopenda soka na vifaa vya kufundishia. Naamini vijana wangu wamejifunza mambo mengi vilevile na mzunguko wa pili utakuwa mzuri tusubiri,” alisema.
Kikosi cha leo kitakachoanza dhidi ya Seeb Club ni, Shaaban Kado, Hamadi Juma, Othman Tamim, Juma Said ‘Nyoso’, Mbwana Kibacha, Jerry Santo, Ally Nassor ‘Ufudu’, Haruna Moshi ‘Boban’, Atupele Green, Danny Lyanga na Yayo Kato Lutimba.
Wengine 12 waliobakia wanaweza kuingia kutokana na upungufu utakaojionyesha wakati mchezo ukiendelea.
COASTAL UNION
18, JANUARI 2014
MUSCAT, OMAN
+986 97695911

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI




Kuna taarifa zimeanza kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu suala la wachezaji watatu wa Coastal Union, kutaka kuchukuliwa na klabu moja hapa nchini Oman.
Nikiwa msemaji wa Coastal Union, ambae nimeambatana na timu nchini hapa naweka wazi kuwa taarifa hizo hazina ukweli. Hakuna kitu kama hicho.
Nimezungumza na mwenyekiti wa Coastal Union, Hemed Hilal ‘Aurora’ ambae pia yupo hapa Oman, na ameonyesha kusikitishwa sana na taarifa hizo na mtoa taarifa aliwahi kumuuliza na alimpa majibu hayohayo kuwa hakuna kitu kama hicho.
Vilevile imedaiwa kuwa uongozi umeshaanza mazungumzo na klabu hiyo inayotaka kuwachukua wachezaji watatu, hakuna kitu kama hicho uongozi haujafanya mazungumzo yoyote na klabu nchini hapa.
Aidha ikiwa kitu kama hicho kipo si vibaya, kwani inaonyesha ni namna gani wachezaji wa Coastal Union wanacheza soka la kuaminika, lakini kuzungumza mambo kwa hisia hiyo ni kinyume na taaluma ya uandishi wa habari.
Hivyo ibaki kuwa mpaka sasa hakuna mchezaji yeyote alietakiwa na klabu, lakini ikiwa kuna klabu imeonyesha kuridhishwa na kiwango cha mchezaji yeyote klabu inaweka wazi milango yake kufanya mazungumzo kwani hiyo ni kawaida na ni bahati kwa mchezaji na klabu.
HAFIDH KIDO (Msemaji)
COASTAL UNION
MUSCAT, OMAN
+986 97695911

Friday, January 17, 2014

Dhifa ya chakula cha usiku kasri la Masoud Esry leo usiku

Dk. Francis Mganga akicheza na farasi
 Msemaji wa Coastal Union, Hafidh Kido akipozi kwa picha kwenye banda la farasi, usiku wa leo.

Golikipa Shaaban Kado, Said Lubawa na Abdullah Othman 'Ustaadh' wakipozi na farasi.
 Wachezaji, kocha na wenyeji wetu katika jumba la Masoud Esry, mjomba wa Salim Esry mwanachama wa Coastal Union nchini Oman, wakiangalia mandhari ya kasri hiyo usiku huu.


Masoud Esry, wa kwanza kushoti akiwa na mmoja wa wanafamilia ya Esry katika chakula cha usiku alichowaandalia wachezaji wa Coastal Union, usiku wa leo.


Wachezaji pia walipata muda wa kuangalia soka, ambapo wanafamilia ya Esry wametengeneza uwanja wa soka ndani ya kasri hilo hucheza soka kila wamalizapo shughuli za kutwa nzima.
 Haruna Moshi 'Boban', akiwa na Othman Abdullah 'Ustaadh'.

 Kaka yake Salim Esry, Khalid Esry wa kwanza kulia akishughulika kuandaa chakula pamoja na wanafamilia ya Esry usiku huu.

 Kutoka kushoto, Dk. Francis Mganga na Kit Manager Mohammed wakipakua chakula katika dhifa hiyo.

Shaaban Kado kushoto akiwa na mwenyeji wetu mjomba wa Salim Esry, Mzee Masoud Esry wakipakua maakuli.
                                 Nahodha wa Coastal Union, Juma Nyoso akipiga vitu vyake.

                                           Aaaaahhhh hamadi Juma 'Basmat' akishughulika...


 Kutoka kulia Salim Esry, Boban na Ustadh wakiwa katika harakati za kupakua maakuli usiku huu.

                                  Suleiman Kassim 'Selembe' akifanya mambo ndani ya 18.

 Mahmoud Zubery 'BinZubery' (mwenye jacket jeusi, aliekaa) mmiliki wa blog ya Bongostaz, akifanya mambo katika blog yake baada ya dhifa.

 Kibacha na Nahodha wake Nyoso wakitendea haki dhifa ya leo.

Suala zima la 'self service' lilihusika sana. (kurudia imo).
Baada ya chakula mchezaji wa Coastal Union, Othman Abdullah 'Ustaadh' alipiga dua ya shukurani.

COASTAL UNION
17 JANUARI, 2014
MUSCAT, OMAN