Sunday, March 31, 2013

Hasira zimeshaniisha naendelea na picha mechi ya jana...

 Manahodha wa Lyon na Wagosi Obina Salamsasa na Mbwana Kibacha wakisalimiana na waamuzi kabla ya mechi.

 Benchi la wagosi wa kaya likiwa na tafakuri wakati kipyenga kinapulizwa kuashiria mchezo umeanza.

 Wanazi wa Coastal Union wakifuatilia kwa makini mchezo wa jana hapa kila mtu alikuwa na matumaini.

 Danny Lyanga aliniudhi sana jana, amekosa magoli mengi sana akiwa na golikipa tu, hapa akijilaumu.

Ohahaaa ohahaaa ehhaaa Doctor... au basi.. Daktari wa timu huyu Coastal Union siku za usoni nitawaletea historia yake hapahapa katika blog yetu. Alianza akiwa mchezaji wa Coastal Union, baada ya kuumia akashauriwa awe Daktari... yote hayo utayapata hapahapa. Kwa udhamini wa Binslum company Limited.

 Huyu Golikipa wa Lyon ni mzuri sana ila amejaa vituko ambavyo vitamsababishia kuharibu kipaji chake.

 Siku ya jana aliingia mpaka uwanjani na kumchezea madhambi Joseph Mahundi wa Coastal Union, hapa mwamuzi anataka kumpa kadi ya njano ndiyo anapiga magoti. Kumbe hiyo ilikuwa ni kadi yake ya tatu katika msimu hivyo atakosa mechi ijayo.

 Makamu Mweneyekiti wa Coastal Union Steven Mnguto akiingia uwanjani na mke wa mchezaji wa kibrazil Gabriel Barbosa. Kwa jaaam namuona Ally Mmahara au Kiraka mzee wa rally.


 Benchi la ufundi la African Lyon likiongozwa na kocha Charles Otieno wa kwanza kuanzia kushoto mwenye miwani meusi.

 Pius akiongoza kigoma uwanja wa Azam Complex Chamazi jana.

 Mwenyekiti Hemed Aurora, Meneja wa timu Akida na kocha wa timu B Bakari Shime wakiangalia vijana.

 Waanazi wa coastal Union wakiwa na matumaini makubwa ya ushindi wakati mchezo unaanza jana.

Eddy, Baba Willy (dereva wa Coastal Union katikati), na mzee Ally pembeni mshabiki mwingine wa Coastal Union wakifuatilia mchezo wa jana hapa ni baada ya kufungwa moja.

No comments:

Post a Comment