Saturday, March 30, 2013

Tathmini mechi ya leo....


Mechi za leo ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara mzunguko wa pili ni Simba dhidi ya Toto African, Kagera Sugar dhidi ya Mtibwa sugar, Ruvu Shooting dhidi ya Azam FC, JKT Oljoro dhidi ya JKT Ruvu, Polisi Morogoro dhidi ya Yanga, na Coastal union dhidi ya African Lyon.


Kama tulivyotangulia kusema jana mechi ya leo ni ngumu na tunahitaji ushindi kwa hali na mali, kwasababu mahasimu wetu wote wanashuka dimbani leo, yaani Simba ambao wanacheza na Toto African mjini Mwanza, Kagera Sugar wanacheza na Mtibwa Sugar Bukoba uwanja wa Kaitaba.

Hivyo ili Coastal Union tukamate nafasi ya tatu ni lazima kushinda mechi ya leo hata kwa goli moja ili tupate point tatu muhimu zitakazotupatia point 37.

Hata hivyo lazima tuombe mabaya kwa Simba SC wafungwe au watoe suluhu mechi ya leo ili wabaki na point 34 hizohizo au 35. halafu Kagera Sugar wafungwe na Mtibwa Sugar wenye point 31 ama watoe suluhu ili wabaki na point 34 au 35.

Naam hili ni jambo la kawaida sana katika mchezo wa soka kuombeana mabaya, si dhambi bali ni kanuni za kisoka kukusanya point nyingi iwezekanavyo na kuomba mpinzani wako apoteze point nyingi iwezekanavyo.

Ligi bado ni ngumu kwani hata hao Yanga wanaotajwa kuwa mabingwa wakiwa na point 48 bado wana kazi ngumu ya kushinda mechi zote tano walizobakisha kwani hata Azam FC wenye point 40 wana nafasi kubwa ya kushinda mechi walizobakisha, ingawa Simba wanaojikongoja wameshapoteza matumaini ya kutetea ubingwa wao ndiyo maana tunaminyana nao katika nafasi ya tatu.

Mungu ibariki Tanga Mungu ibariki Coastal Union katika mchezo wa leo dhidi ya vibonde African Lyon uwanja wa Azam Complex Mbande jijini Dar es Salaam.

COASTAL UNION
30 March, 2013
Dar es Salaam, Tanzania



No comments:

Post a Comment