Friday, February 8, 2013

Tulipofika uwanja wa CCM Kirumba ili kufanya mazoezi jioni tukakuta zengwe, Toto africa wanafanya mazoezi wakati John Tegete kocha wa Toto ni meneja wa uwanja huo anajua taratibu zote... ilikuwaje ingia ndani uone picha.

 Tulipokwenda kufanya mazoezi uwanja wa irumba tukakuta Toto Africa nao wanafanya mazoezi. Ilikuwa balaa mpaka wakaondoka baada ya kuwaeleza tuliwahi kuomba uwanja na pia kocha wa Toto ni meneja wa uwanja ina mana hajui taratibu za uwanja?

                                               Ila hatimae tukafanya mazoezi kibishi.

              Viongozi wa msafara wakitafakari jambo akati vijana wakipasha misuli moto.

 Kibacha akinyoosha viungo na Castro Mumbala, pembeni namuona Barbosa kwa jaaam.

                                                       Captain Santo akisprint.

                                                      Rajabu golikipa mzuri kumbe...

 Ally Kidi akiwatazama vijana wake wanavyonyoosha viungo wakati wa mazoezi jana.

                                                          Barbosa on the move.


                                 Shaaban Kado akifuliwa na Pondamali hayupo pichani.

                                             Barbosa na Sipi wakitunishiana misuli.

 Coastal Union tukawa maarufu ghafla, mara waandishi wa habari wakaanza kumiminika uwanjani wakati timu ikifanya mazoezi. Huyu ni mwanahabari anaitwa Wakuganda Issack kutoka Metro FM Radio ya Mwanza.
 Meneja Akida akiwa anamsikiliza mwalimu anavyowaasa vijana..


Danny akishangaa shangaa... ahahaaa hii picha nimeipenda sana.... aisee babaangu Danny hii si Moshi... ni Mwaa ni Mwaanza kweeli...

Uwanja wa ndege wa Mwanza mdogo ila unatua ndege kila baada ya saa moja.


 Hemed Morroco ameshazoea mambo haya halafu nimegundua hapendi picha angalia hapa anajaribu kunikwepa ahahaaa.... tichaaaaa.

                                          Vijana wakisubiri Bus tuelekee kambini. Airport Mwanza.

 Kutoka kushoto Aurora katikati katibutimu  wa Bawazir wa timu na kit manager katika uwanja wa ndege Mwanza.


Baadae tukakaribishwa Mwanza


Coastal Union kukabiliana na Toto africa kesho Mwanza. angalia picha za safari leo...

 Juma Pondamali kocha wa makipa akibadilishana mawazo na mzee wa timu katika msafara.

 Kushoto namuona Shaaban Kado, Ismail suma na Abdi Banda wakivuka barabara kwa Binslum.

 
 Ahahahaa miraji wandi akiiona hii picha atacheka sana, Hamad anapenda Basmat sana sasa leo Binslum aliamua kummaliza kabisa.

                         Vijana wa Coastal wakipata chakula cha mchana kabla ya safari.

 Mwenyekiti wa coastal Union Hemed Aurora akiwa na meneja wa timu akida Machai wakipata chakula.

Danny Lyanga akishuka katika gari mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Julius Nyerere.

                                         Barbosa akiwa na Phili uwanjani wakisubiri ndege.

 Walimu wote watatu Morroco, Ally Kidi na Juma Pondamali wakibadilishana mawazo uwanjani.

 Jembe na mimi nilikuwemo kwenye safara hapa nikiwa na jembe langu Selembe.

Nassor Binslum ambae ni mkurugenzi wa ufundi akitoa ahadi ya laki tatu kwa kila mchezaji ikiwa watarudi na point sita kutoka kanda ya ziwa. Yaani wakishinda mechi ya Toto Africa kesho na mechi nyingine dhidi ya Kagera Sugar tarehe 13 uwanja wa Kaitaba Bukoba. Lakini akawaambia wakishinda mechi moja kila mmoja atapata laki moja.

Monday, February 4, 2013

Usicheze na Coastal Union wamedhamiria mwaka huu. Jezi zina majina...

Ibrahim Hussein jina jingine anaitwa Messi, alitoka timu B. Coastal pia tunakuza vipaji taraa. Gabrel Barbosa anakuwa Mbrazil wa kwanza kucheza soka la ushindani Tanzania. Coastal Union bwanaaa ni kamaa maajii... lazima utayanywa tu.

Sunday, February 3, 2013

Morroco anasema tunampumulia simba mgongoni kwa tofauti ya Point moja tu.....

                                Kocha mkuu wa Coastal Union wagosi wa kaya Hemed Morroco.


Na Mwandishi maalum

Timu ya Coastal Union kutoka mjini Tanga leo imetoa suluhu tasa dhidi ya wajelajela Prison ya Mbeya katika uwanja wa mkwakwani na kuendelea kubakia katika nafasi ya nne katika msimamo wa ligi kuu chini ya wekundu wa msimbazi Simba inayoshikilia nafasi ya tatu.

Mchezo wa leo ulikuwa wa kukamiana kwani maafande wa Prison walitaka kurekebisha makosa baada ya kufungwa 3-1 katika mechi yao ya kwanza ya mzunguko wa pili dhidi ya Yanga  katika uwanja wa taifa Dar es Salaam, dakika za awali mchezaji wa Coastal Union Danny Lyanga aliipatia timu yake bao la kuongoza lakini refa akasema alikuwa ameotea ‘offside’.

Coastal Union ambayo langoni alikaa golikipa aliesajiliwa katika dirisha dogo kutoka mtibwa Sugar Shaaban Kado, wengine ni Ismail Suma, Othman Tamim, Bakari Kibacha, Philip Mugenzi, Jerry Santo, Lameck Dayton, Shango, Danny Lyanga, Suleiman Kassim Selembe na Mahundi.

Katika dakika za majeruhi kipindi cha pili kocha wa Coastal Union Hemed Morroco alifanya mabadiliko akamtoa Mahundi akaingia Mbrazil Gabriel Barbosa ambae amecheza kwa mara ya kwanza katika ligi kuu ya Tanzania Bara. Baadae akatoka Shango akaingia Castro Mumbala.

Mbrazil Barbosa ambae kwa kipindi kirefu alikuwa midomoni mwa mashabiki wa Coastal Union juu ya uwezo wake kisoka, leo alionyesha soka la hali ya juu katika dakika 15 za mwisho alizoingizwa. Alikosa magoli mengi lakini lile lililoamsha watu ni pale alipopga tick tack lakini golikipa wa Prison alikuwa imara na kumkosesha bao Barbosa.

Kwa matokeo hayo Coastal Union itaendelea kubakia nafasi ya nne ikiwa na point 26, chini ya Simba ambayo ina point 27 baada ya kutoka suluhu ya moja kwa moja leo dhidi ya JKT Ruvu katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Yanga wamebaki kileleni na point 33 ambao nao walitoka suluhu ya moja kwa moja dhidi ya Mtibwa Sugar jana kwenye uwanja wa Taifa jijini. Azam wao wapo nafasi ya pili wakiwa na point 30 baada ya kuwachabanga 3-1 Toto Africa katika uwanja wa Chamazi kwenye mchezo wao wa pili.

Ligi sasa imekuwa na upinzani mkali kwani timu nne za juu yaani Yanga, Azam, Simba na Coastal Union zinaonyesha upinzani mkubwa na macho ya watanzania wengi yamehamia katika timu hizo ingawa zipo timu kama Africa Lyon, Mtibwa Sugar na Kagera Sugar zinacheza mpira wa nguvu na wa kukamia.

Coastal Union itacheza tena mechi yake ya tatu tarehe 9 mwezi wa pili dhidi ya Toto Africa katika uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza na watabaki hukohuko kanda ya ziwa wakisubiri mechi yao nyingine tarehe 13 mwezi wa pili mwaka huu dhidi ya Kagera Sugar katika uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.

Coastal Union
Dar es Salaam, Tanzania
3/2/2013



Saturday, February 2, 2013

Coastal Union kukwea pipa safari yao ya Mwanza tarehe 9/02/2013 kucheza na Toto Africa uwanja wa Kirumba.

Uwanja wa mkwakwani unaingiza mashabiki 10,000 kwa wakati mmoja. Kwa muda mrefu wakati Coastal Union ilipokuwa nje ya michuano ya ligi kuu bara haukuwa ukijaza watu namna hii. Coastal inazidi kuwapa raha watu wa Tanga, nasi hatuna budi kuwapa raha kwa kuwaonjesha raha za ndege kwa safar za mbali kama Bukoba na Mwanza.


COASTAL Union ya Tanga itapanda ndege kwa mara ya kwanza baada ya miaka 24 wakati itakapoondoka Februari 8 kuelekea Mwanza kucheza mechi ya Ligi Kuu Bara. 

Habari za ndani ya klabu hiyo zinaeleza kuwa timu hiyo itafanya safari hiyo ikitokea Dar es Salaam kwa ndege ya Shirika la Ndege la Fast Jet kwa ajili ya kucheza mechi ya 
ligi dhidi ya Toto African itakayopigwa Februari 9 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza. 

Timu hiyo itarejea Dar es Salaam, Februari 14 baada ya kucheza na Kagera Sugar, Februari 13 kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba. 

Coastal Union ikirudi itaelekea Tanga ili kujiandaa na mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi JKT Oljoro itakayofanyika Februari 20 kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga. 

Mara ya mwisho kwa Coastal Union kupanda ndege ilikuwa mwaka 1989 wakati ilipokwenda Msumbiji kwenye mashindano ya Kombe la Washindi barani Afrika. 

Coastal Union ilikwenda huko kukabiliana na Costo Do Sol kwenye mechi ya marudiano ya mashindano hayo na ilifungwa 2-1 kwenye mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa Machava mjini Maputo. 

Katika mchezo wa kwanza baina ya timu hizo uliochezwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga, Coastal Union ililala 2-0. 

Hata hivyo, kabla ya kwenda Msumbiji, pia walipanda ndege kwenda Nairobi, Kenya kwenye mashindano ya Klabu Bingwa katika mwaka huo wa 1989. 

Siku hizi ni nadra kwa timu za Ligi Kuu hasa zile za mikoani 
kupanda ndege kutokana na gharama kubwa na kudorora kwa soka la mikoani. 

Katika miaka ya nyuma, ilikuwa si kitu cha ajabu kwa timu ya mkoani kupanda ndege mathalan timu kama Pamba ya Mwanza, Majimaji ya Songea, Bandari ya Mtwara na Mwadui ya Shinyanga zilikuwa na utaratibu wa kukwea ndege zinapokwenda kucheza mechi za ligi sehemu mbalimbali za Tanzania.

Chanzo: Mwanaspoti gazeti jumamosi tarehe 02-02-2013 .