Timu ya Coastal
Union kesho itashuka dimbani dhidi ya maafande Ruvu Shooting kusaka point tatu
muhimu zitakazoipandisha mpaka nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi kuu ya
Vodacom Tanzania
bara.
Wagosi wa kaya
wanacheza mchezo wao wa sita katika uwanja wa nyumbani wa Mkwakwani wakiwa na
historia ya kupoteza mchezzo mmoja tu dhidi ya Kagera Sugar kwa kufungwa goli
moja bila majibu katika uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
Hata hivyo
mgambo hao wa wanaotoka mkoa wa Pwani wameshaanza mizengwe kwa kukimbilia TFF
wakidai mchezo uliopita katika uwanja wa Mkwakwani walifanyiwa vurugu na
mashabiki wa wagosi wa kaya hivyo waliwasilisha malalamiko hayo kwa njia ya DVD
wakionyesha tukio la vurugu kwa njia ya video, hivyo kuitaka TFF kuchezesha
mchezo huo wa kesho bila mashabiki.
Hata hivyo
shirikisho hilo la mpira wa miguu Tanzania haikutilia maanani malalamiko hayo
hivyo mchezo wa kesho utakuwepo kama kawaida na tunawataka wapenzi wa Coastal
Union kujitokeza kwa wingi ili kushuhudia timu yao ya nyumbani ikifanya maajabu
na kuendeleza ubabe wa soka kutoka mkoa wa Tanga uliokuwepo kabla ya kupatikana
uhuru wa Tanganyika.
Kwa kuthibitisha
kuwa Coastal Union inawajali mashabiki wake wa nje ya mkoa wa Tanga mchezo huo
wa kesho utarushwa moja kwa moja ‘live’ kwenye radio ya Kiss FM; pia kupitia
ukurasa wetu wa facebook vijana wetu watakuwa wanaleta matangazo ya moja kwa
moja kutoka uwanjani.
Coastal Union
mpaka sasa imeshacheza michezo 18, na imebakisha michezo 8 ili kukamilisha
michezo yote 26 ya ligi kuu. Na maombi ya viongozi na wanachama ni kuhakikisha
wagosi wa kaya wanachukua taji hili ambalo wana uchu nalo kwa miaka 25 sasa
tangu kulichukua kwa mara ya mwisho mwaka 1988.
Viongozi wa Coastal Union wakishuhudia timu yao ikipigwa 1-0 na Kagera Sugar uwanja wa Kaitaba Bukoba mkoani Kagera.
Aidha wagosi wa kaya wana point 30 kibindoni waking'ang'ania nafasi ya nne wakati Yanga anaeshika nafasi ya kwanza ana point 39, Azam FC walio nafasi ya pili wana point 36 na Simba wana point 31 wakiwa nafasi ya tatu.
ifuatayo ni michezo iliyobakia:
27/02/2013 Mkwakwani (Tanga) Coastal Union Vs
Ruvu Shooting.
2. 10/03/2013 Uwanja wa Taifa (Dar es Salaam ) Simba Vs Coastal Union .
3. 16/03/2013 Manungu (Morogoro) Mtibwa Sugar Vs
Coastal Union .
4. 30/03/2013 Azam Complex (Dar es Salaam ) African Lyon
Vs CoastalUnion .
5. 10/04/2013 Mkwakwani (Tanga) Coastal Union Vs
JKT Ruvu.
6. 27/04/2013 Mkwakwani (Tanga) Coastal Union Vs
Azam FC.
7. 01/05/2013 Mkwakwani (Tanga) Coastal Union Vs
Young African.
8. 18/05/2013 Jamhuri (Morogoro) Polisi morogoro Vs
Coastal Union.
No comments:
Post a Comment