Hemed morroco na Juma Pondamali wakishuka kuingia ndani ya Feri kuvuka kuelekea Mwanza.
Ally Kiraka nae alikuwemo katika msafara hapa akishuka kuingia katika feri.
Mwenyekiti hapa akiwa ndani ya feri anasema hajawahi kuona ziwa Victoria maana ni kubwa balaa.
Hapa vijana walishuka kuchimba dawa.
Hapa panaitwa Katoro, leo kulikuwa na vurugu kati ya Waislam na Wakristo ambapo inasemekana wamekufa watu zaidi ya watatu. Vurugu zenyewe zilisababishwa na Wakristo wa eneo hilo ambalo lipo Mkoa wa Geita kuchinja mbuzi na ng'ombe kwa ajili ya biashara kitu ambacho kilikataliwa kisheria.
Muleba hapa Selembe na Suma wakitembeatembea kuangalia mandhari na kushusha chakula.
Kutoka Mwanza kuelekea Bukoba ni kilometa 400, safari ilikuwa nzuri na tayari vijana wamepumzika tayari kwa mazoezi kesho asubuhi.
No comments:
Post a Comment